nyamalagala
JF-Expert Member
- Jun 5, 2016
- 744
- 673
Wakuu natumai nyote mu bukheri wa afya, Nianze kwa kuwasabahi.
Mimi nimekuwa nikisoma thread zenu pamoja na michango mbalimbali za wadau. Leo nabisha hodi kwa kuwashirikisha jambo hili la kihistoria japo najua wengi wenu mnafahamu lakini sio vibaya kujikumbusha ilikuwaje jina Tanganyika likachukuliwa kama jina la taifa la Tanganyika enzi hizo kabla ya kuitwa Tanzania kwa sasa.
Kipindi hicho chini ya utawala wa kijerumani Tanzania ya sasa ilikuwa ikiitwa "Deutsche Ost-Africa". Kuingia kwa waingereza kulipelekea juhudi za kutafuta jina lingine zianze. Awali mnamo mwaka 1920, majina kadhaa yalipendekezwa yakiwemo "Smutsland","Ebumea","New Maryland","Windsorland" na "Victoria". Hata hivyo majina hayo yote yalikataliwa na serikali ya uingereza kutokana na sababu mbalimbali. Baadaye serikali ya uingereza ilielekeza yapendekezwe majina ya kienyeji na kwa mwanya huo ndipo yakajitokeza mapendekezo ya majina ambayo ni "Kilimanjaro" na "Tabora"ambayo yalifikiriwa lakini hayakukubalika.
Hatimaye jina "Tanganyika protectorate" lilipendekezwa na msaidizi wa Waziri Wa Makoloni na likakubaliwa na serikali. Ifahamike kwamba kabla ya ujio wa wageni kutoka ulaya, wenyeji katika maeneo ya magharibi mwa nchi waliliita ziwa kubwa lilopo eneo hilo "ziwa Tanganyika".
Inaelekea kuwa hiyo ndiyo sababu kuu ya kuwafanya maofisa wa kiingereza kulikubali jina la Tanganyika kwa sababu lilikidhi matakwa ya Sera kwa kuwa lilitokana na majina ya kienyeji. Hatimaye baadaye neno "protectorate"liliondolewa kutoka jina rasmi la "Tanganyika protectorate" na badala yake likawekwa neno "territory".Kwa hiyo kuanzia mwaka 1920 hadi Uhuru nchi ilijulikana kama "Tanganyika Territory".wakati wa kuupigania Uhuru neno territory liliondolewa na Kubaki
"TANGANYIKA".
Chanzo_taarifa ya miaka hamsini ya Uhuru wa Tanzania bara 1961-2011.
Naomba kuwasilisha.