Fahamu aina tano za sumu ya Nyoka na matibabu yake

Fahamu aina tano za sumu ya Nyoka na matibabu yake

Jackson94

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2016
Posts
505
Reaction score
600
1474095432592.png

Hii ni sumu ambayo inatolewa na nyoka wakati wa kung'ata mtu, asilimia kubwa ya nyoka ambao wapo kwenye mazingira yetu hua hawana sumu yaani kimsingi ukiona mtu ameng'atwa na nyoka leo afu kesho ndio akaenda hospitali baada ya mguu kuvimba basi ujue nyoka yule haukua na sumu. Nyoka wenye sumu kama cobra na black mamba huua ndani ya dakika 20 baada ya kumng'ata mtu.hivyo ukingatwa na uko umbali wa mwendo dakika 20 kutoka hospitali ujue utakufa tu.

Aina za sumu ya nyoka:
cytotoxin poison;
hii hushambulia seli za juu za mwili na kuziharibu au kuleta kidonda.

haemotoxin;
hii husababisha damu iwe nyepesi sana na kuanza kuvuja ndani kwa ndani au damu kushindwa kuganda kama inamwagika kutoka kwenye kidonda, sumu husababisha sehemu muhimu za mwili kukosa damu na kufa kwa muhusika.

neurotoxins; hii aina ya sumu ambayo hushambulia mishipa ya fahamu, mgonjwa akiingiliwa na sumu hii hawezi kufanya chochote, hata kutikisa kidole hawezi na hufariki baada ya muda mfupi.

cardiotoxins; sumu hii hushambulia moyo wa binadamu na kuulazimisha kusimama hivyo kuleta kifo cha ghafla.

myotoxins; sumu hii hushambulia misuli yote ya binadamu na kuiharibu.


Dalili baada ya kuumwa na nyoka:
maumivu makali sehemu iliyoshambuliwa.ganzi.kuvimba sehemu husika.kidonda.kuvuja kwa damu[isipozuiliwa huweza kuua.

mishipa ya fahamu; nyoka huyu huweza kutoa sumu kali kwenye mishipa ya fahamu ambayo husimamisha shughuli ya upumuaji na kuua kabla ya matibabu. kabla ya kufa mgonjwa huanza na dalili za kushindwa kuona, kushindwa kupumua vizuri, ganzi na kushindwa kusema.

misuli; nyoka kama rusells vipers, nyoka wa baharini na cobra huweza kuharibu misuli kabisa na kuifanya isambae kwenye mishipa ya damu hivyo kusababisha kufa kwa figo mara moja.

damu; aina ya nyoka kwa jina la boomsling huzuia damu kuganda na kuifanya iwe laini sana, mgonjwa huvuja damu ndani kwa ndani au nje mpaka kifo.

macho; nyoka aina ya cobra hurusha sumu yake moja kwa moja kwenye macho ya binadmu na kuyaharibu au kuleta upofu kiabisa.

huduma ya kwanza:
hakikisha mgonjwa anapumua hata kama ni kidogo angalia kama kuna damu inavuja sehemuhakikisha anapaata hewa ya kutosha, asizungukwe na watu.mgonjwa asitembee kwani atasambaza sumu mwilini yaani abebwe palepale.usifunge kamba kwenye mguu kwani imeonekana haizuii chochote zaidi ya kuharibu kiungo husika.usichanje na wembe au kunyonya na kutema sumu kwani utaharibu mishipa ya damuusiweke barafu kwani hakuanushahidi kwamba inasaidia.piga simu kuomba msaada ili mgonjwa apelekwe hospitali.usiweke pombe kwani huongeza ukubwa wa mishipa ya damu na kusambaza sumu zaidi.kama nyoka amekufa nenda naye hospitali daktari amuone ili ajue kama ana sumu au hana sumu.

matibabu ya hospitalini:
kulingana na hali ya mgonjwa hupewa vifuatavyo:

huongezewa maji mwilini, hii husaidi kuongeza presha ya damu na kupunguza sumu. Hupewa dawa za kuua bacteria[antibiotics]huchomwa sindano ya tetenasihupewa dawa za maumivu.hushauriwa asiwe na wasiwaasi.kidonda huoshwa na maji mengi na kuondoa jino la nyoka kama lipo.

Mgonjwa atapewa dawa ya kuondoa sumu mwilini kama ikithibitika nyoka alikua na sumu ambayo inaitwa kitaalamu kama polyvalent antisera kama nyoka hana sumu mgonjwa hatapewa dawa hii.dawa ya kuondoa sumu hutakiwa utolewe ndani ya dakika 20 kama sio hivyo mgonjwa atafariki.

Jackson9

PIA SOMA:
= > Yajue mambo muhimu ya kufanywa pindi unapoumwa au kung'atwa na wadudu au viumbe wengine wenye sumu
 
sasa unajikinga vipi mbna hujaweka vitu kwa uhakika
 
Hawa nyoka hupatikana msituni na safari kutoka msituni mpaka hospital ni zaidi ya dakika 20 kwahiyo mgonjwa lazima afariki tu

Mpaka hapo solution bado haijapatkana
 
Hawa nyoka hupatikana msituni na safari kutoka msituni mpk hospital ni zaidi ya dakk 20 kwahyo mgonjwa lzm afariki tu

Mpk hapo solution bado haijapatkana
Mkuu inategemeana
 
niliumwa na nyoka, kufika dispensary wacha dokta anichanje chanje afu akanipaka split, malipo ananiambia 30,000 nlichokifanya nikatoka nje nkazuga naongea na cm kucheki hmn alyeniona acha niwaachie vumbi
 
Kwa wale mnaodharau tiba za kienyeji,yaani tiba mbadala, ndio tiba pekee ya uhakika ya kumtibu mtu aliegongwa na nyoka

mimi nikajua mtoa mada atatuambia jinsi ya kujitibu kiporipori yeye anatuletea mambo ya hospitali situngekuwa tumekufa wote tulionga'twa na nyoka
 
Mleta mada katuacha njia panda.
Unaumwa na Nyoka porini, kufika hospitali ni zaidi ya muda wa saa moja.
Yeye anasema mtu unakufa baada ya dakika Ishirini.
Sasa utajihudimiaje ili usife hadi ufike hospitali ?

Usianzishe mada kama huna utaalamu nayo.
Hujasema unafanyaje hadi usife ndani ya dakika ishirini ili ufike hospitali.

Huduma sahihi ya kwanza ipoje ?

Zungumza kitu ambacho una utaalamu nacho.
 
mimi nikajua mtoa mada atatuambia jinsi ya kujitibu kiporipori yeye anatuletea mambo ya hospitali situngekuwa tumekufa wote tulionga'twa na nyoka
tena huu ushauri umetolewa na madaktar bingwa duniani kuwa natural cure can only do the best kwa mgonjwa aliyegongwa na nyoka,na ndio wanaoweza kujua ni aina gani ya nyoka aliye kung'ata kwa kuangalia jino la nyoka lililobaki maana kila nyoka wana aina yake ya meno kulingana na sumu wanayotema
 
mimi nikajua mtoa mada atatuambia jinsi ya kujitibu kiporipori yeye anatuletea mambo ya hospitali situngekuwa tumekufa wote tulionga'twa na nyoka
tena huu ushauri umetolewa na madaktar bingwa duniani kuwa natural cure can only do the best kwa mgonjwa aliyegongwa na nyoka,na ndio wanaoweza kujua ni aina gani ya nyoka aliye kung'ata kwa kuangalia jino la nyoka lililobaki maana kila nyoka wana aina yake ya meno kulingana na sumu wanayotema
 
Nilidhani anatuelekeza njia ya kujinusuru ikiwa uko mbali na hospitali kumbe anatwambia mengine
 
Urithi safi kabisa
Makabila ambayo yako mbali na huduma za hospitali wanalitumia hilo jiwe.
Unakuta katika kijiji fulani Wazee wenye hilo jiwe wanajulikana, mtu akiumwa na na Nyoka wanakimbia kuliazima wanalitumia kadri ya maelezo yake na mwisho wa tiba wanamrudishia mwenye jiwe lake.
Hapo hakuna kuongezwa Maji wala kupigwa Sindano kazi huwa imekwisha.
 
Asante kwa elimu ndugu naomba namba yako nikupigie sahivi ninashida ya muhimusana 0753369296
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom