Fahamu A-Z kumhusu Yusuf Manji

Fahamu A-Z kumhusu Yusuf Manji

Wadau. Nimejiuliza sana huyu Yusuf Manji ni nani nikakutana na uzi huu mfandaoni. Embu nawe ongeza maarifa kidogo kumfahamu mfanyabiashara huyu mkubwa nchini.

=====

Nimesukumwa na haya yote yaliyokua yakiendelea kumzunguka Mfanyabiashara Yusuf Manji. Kukamatwa, kushtakiwa na sasa yuko huru, huyu bwana ameona yote tena kwa kipindi kifupi. Kama Mkenya nilibaki na sintofahamu, naandika mengi kuhusu mienendo ya biashara kwa nini sio kuhusu huyu bwana ambaye pia ni tofauti. Niliingia ndani sana ili kumjua yeye ni Nani. Wengine wanasema ni mjasiriamali mwenye mafanikio ingawa wafanyakazi kwenye kampuni zake wanamuona kama mungu. Kuna ambao wanamthamini kwa mchango wake hata nje ya Tanzania kama kwenye umoja wa Afrika alipochangia mfuko wa ebola, wakati kuna wengine wakimtuhumu kama anatumia madawa si tajiri aliyejipatia ndege binafsi.

Hadithi pia zilijitokeza kwenye suala la coco beach, quality plaza na Kiwanda cha samaki Mwanza na pia kuajiri wahamiaji bila vibali kamili. Ametawala vyombo vya habari na hadi kwenye mitandao. Kutaka kwangu kujua kulinifanya kufanya utafiti mkubwa na haya ni baadhi ya mambo yaliyonifanya nijiulize pande zake mbili vizuri

  1. Yusuf Manji ni jina lijulikanalo vizuri Africa baada ya kuchukua biashara za baba yake mwaka 1995 Dar Es Salaam na kuzisambaza duniani kote kwa kutengeneza utawala mkubwa wa Quality Group Limited
  2. Anajulikana kwa kuleta Tanzania majina makubwa ya biashara kama General Motors, ISUZU, Mahonia, Hertz na Bridgestone.
  3. Kampuni zake zimefanya biashara ya mazao ya baharini na ziwani na zaidi ya makampuni 30 barani Asia na Ulaya.
  4. Inasemekana amejenga mall ya kwanza ya kisasa nchini kwa jina la Quality Center na pia amezalisha mchele kwa njia za kisasa.
  5. Nchi inashuhudia ujenzi wa makazi ya kisasa yenye sifa zaidi ya mia moja ambao hakuna yoyote ameshawahi kufanya.
  6. Manji ameanzisha huduma za afya kwa jina la Quality Health na inasemekana inapatikana hadi vijijini na kwa bei nafuu sana.
  7. Kwa gharama zake Manji aliisaidia Tanesco, kanunua gazeti na pia kuanzisha biashara za kwenye mitandao .
  8. Pia ameanzia biashara ya boda boda kwa jina la fasta fasta. Unaweza kuagiza usafiri kwa njia ya simu popote ulipo.
  9. Kampuni yake ni moja ya kampuni za kwanza Afrika kushirikiana na serikali ya Ireland kwenye mradi wa viwanja vya ndege afrika mashariki. Pia alijaribu kuokoa ajira za watanzania kwa kununua Uchumi Supermarket baada ya kutaka kufungwa, ingawa ilishindikana kutokana na hila za hapa na pale hata hivyo alifungua American Supermarket kuokoa ajira hizo. Sasa anataka kununua Nakumatt na maduka yake (sidhani kama itawezekana kutokana na hila hizo na watanzania watapoteza ajira pamoja na pesa za wafanyabiashara)
  10. Inajulikana kua Yusuf Manji aliomba serikali kuchakata dhahabu ili kuwezesha serikali kupata faida ya kutosha, na pia kufungua kiwanda cha kuunganisha magari
  11. Kuikuza sekta ya madini, Manji anaongea na wataalamu wa madini kutoka India na sehemu mbali mbali, hii ikifanya kazi itaongea inchi mapato makubwa.
  12. Amejaribu kuanzisha maonyesho makubwa Hongkong yatakayoleta wadau wa kubwa wa usafiri Tanzania na pia kukusanya matamasha ya filamu kutoka Zanzibar kuonyesha vivutio vya Tanzania na kuamsha sekta ya usafiri na burudani Tanzania
  13. Kampuni zake zimetengeneza nafasi za biashara wa sanaa za vijijini kwa kuanzisha Duka kubwa la vinyago na sanaa kwa jina la Tanzania Center For Cultural Heritage (TCCH)
  14. Kwenye uwanja wa michezo Manji ameisadia sana Timu ya Yanga, alikua Mwenyekiti na amejaribu sana kuleta makocha bora, mafunzo na mipango ya safari kwa wanachama wake. Wakati Yanga ipo kwenye kilele cha mafanikio Yusuph alijiuzulu badala ya kung’ang’ania madaraka au kutaka kuinunua timu kama ambavyo ingekuwa kwa wengine wengi duniani.
  15. Pia Manji ana mpango wa kuwekeza kwenye kilimo morogoro. Hapa ana mpango wa kuajiri wazawa pekee kwemye viwanda vya sukari na mchele. Mpango wake ni kuifanya Morogoro kuwe kitovu kikubwa cha ajira Tanzania. Pamoja na huduma nzuri za elimu na afya hii itakua sehemu nzuri inayohitajika kwa wazawa kuishi. Ameonekana kwenye Tv akisaini mikataba na kampuni za kutengeneza matrekta kuweka kiwanda morogoro.
  16. Bila kutangaza amekua na madaktari wakitembelea vijijini mara mbili kwa wiki. Pia amekua akitoa huduma za elimu na afya bure kwa maelfu ya wanafunzi wa Mwanza ambako ana kiwanda kikubwa cha kusafirisha samaki.
  17. Watu waliofanya kazi na Yusuf Manji wanasema timu yake ya kazi ni ya ajabu, wanasimama nae hata kwemye matatizo. Mafanikio yake ni juu Yao.
  18. Yusuph Manji alitunukiwa kama 'Mmoja wa viongozi Africa' na pia ofisi yake ilipewa hadhi ya 'House of Lords' kwa kua na umiliki bora wa kibiashara.
  19. Kwa juhudi kubwa za kufanikisha Kata yake kama diwani wa CCM, amejenga miundo mbinu bora, huduma bora za afya, elimu na kuboresha maisha. Amejitoa sana kushiriki shughuli za kijamii.

Anafanya sana vizuri kwemye mitandao kwenye jamii yote ya wafanyabiashara. Sio tu Afrika lakini zaidi ya Asia, Mashariki ya kati na nchi nyinginezo.

Ninachodhani baada ya utafiti, Yusuf Manji hajawahi kupata sifa zake au kutambuliwa na media baada ya jitihada zote za kuleta biashara kubwa mpaka kufungua mall bora ya kwanza Quality Center. Kwa uhakika amebadilisha maisha ya wengi . Kwa ukubwa na ujasiri wake sidhani kama itafikia mwisho wa yeye kuongelewa ongelewa.

Licha ya heshima au ukubwa wake kwenye macho ya watu, Yusuf manji amefanya biashara Dar, mji wenye kasi ya ukuaji kiuchumi kwa njia bora za kibunifu na kutambulisha mengi, kuajiri maelfu na kusaidia maelfu wenye mahitaji. Nitakuachia wewe uamue unamuonaje
Naona umetumwa! Manji ni fisadi kama mafisadi wengine full stop!!
 
Aliiba au aliuziwa na waumini wa waislamu kwa matakwa yao wenyewe?! Na yeye ni dini gani?! Waislamu wana njaa sana sometimes
wanaweka njaa mbele mpaka wanakosa nidham kwa viongozi wao
 
kumbe na wewe unamkubali sana huyu jamaa. very good mkuu
 
JAMANI.....!!! Tumefika pabaya....! Hata fedha za waathirika wa UKIMWI tunazipora bila huruma?????? AIBU, AIBU, AIBU kubwa. Huu ni unyama.
 
Attachments

  • Job1.png
    Job1.png
    28.7 KB · Views: 56
Manji ni tapeli mkubwa acha kuleta upuuzi wako! li laghai, mwizi, dhulumati na mhuni mkubwa!

Manji ameshawahi kukuibia kitu gani wewe mlalahoi. Taja kimoja tuu alichoiba au kudhulumu uone ulivyo maskini wa fika na roho
 
Mbona mazuri yake tu? Mitandao ipi uliyofatilia umekuta mazuri yake tu?
Vipi alivyonunua mali za waislam bila huruma uku waisam(sio bakwata) wakisononeka.
Mtu anaposema mtandao sidhan km anamaanisha instagoogle twitface pekee...watu wake wanaomzunguka pia ni mtandao.
 
Nimefanyakazi kwenye mojawapo ya kampuni zake Quality motors ltd miaka mitatu na nusu namjua vizuri hana matatizo na wafanyakazi wake na wote wanampenda katika shida na raha, nakumbuka wakati wa mvutano wake na Reginald mengi alituita wafanyakazi wake makampuni yote pale Diamond jubilee na wote tulisimama upande wake
 
Wadau. Nimejiuliza sana huyu Yusuf Manji ni nani nikakutana na uzi huu mfandaoni. Embu nawe ongeza maarifa kidogo kumfahamu mfanyabiashara huyu mkubwa nchini.

=====

Nimesukumwa na haya yote yaliyokua yakiendelea kumzunguka Mfanyabiashara Yusuf Manji. Kukamatwa, kushtakiwa na sasa yuko huru, huyu bwana ameona yote tena kwa kipindi kifupi. Kama Mkenya nilibaki na sintofahamu, naandika mengi kuhusu mienendo ya biashara kwa nini sio kuhusu huyu bwana ambaye pia ni tofauti. Niliingia ndani sana ili kumjua yeye ni Nani. Wengine wanasema ni mjasiriamali mwenye mafanikio ingawa wafanyakazi kwenye kampuni zake wanamuona kama mungu. Kuna ambao wanamthamini kwa mchango wake hata nje ya Tanzania kama kwenye umoja wa Afrika alipochangia mfuko wa ebola, wakati kuna wengine wakimtuhumu kama anatumia madawa si tajiri aliyejipatia ndege binafsi.

Hadithi pia zilijitokeza kwenye suala la coco beach, quality plaza na Kiwanda cha samaki Mwanza na pia kuajiri wahamiaji bila vibali kamili. Ametawala vyombo vya habari na hadi kwenye mitandao. Kutaka kwangu kujua kulinifanya kufanya utafiti mkubwa na haya ni baadhi ya mambo yaliyonifanya nijiulize pande zake mbili vizuri

  1. Yusuf Manji ni jina lijulikanalo vizuri Africa baada ya kuchukua biashara za baba yake mwaka 1995 Dar Es Salaam na kuzisambaza duniani kote kwa kutengeneza utawala mkubwa wa Quality Group Limited
  2. Anajulikana kwa kuleta Tanzania majina makubwa ya biashara kama General Motors, ISUZU, Mahonia, Hertz na Bridgestone.
  3. Kampuni zake zimefanya biashara ya mazao ya baharini na ziwani na zaidi ya makampuni 30 barani Asia na Ulaya.
  4. Inasemekana amejenga mall ya kwanza ya kisasa nchini kwa jina la Quality Center na pia amezalisha mchele kwa njia za kisasa.
  5. Nchi inashuhudia ujenzi wa makazi ya kisasa yenye sifa zaidi ya mia moja ambao hakuna yoyote ameshawahi kufanya.
  6. Manji ameanzisha huduma za afya kwa jina la Quality Health na inasemekana inapatikana hadi vijijini na kwa bei nafuu sana.
  7. Kwa gharama zake Manji aliisaidia Tanesco, kanunua gazeti na pia kuanzisha biashara za kwenye mitandao .
  8. Pia ameanzia biashara ya boda boda kwa jina la fasta fasta. Unaweza kuagiza usafiri kwa njia ya simu popote ulipo.
  9. Kampuni yake ni moja ya kampuni za kwanza Afrika kushirikiana na serikali ya Ireland kwenye mradi wa viwanja vya ndege afrika mashariki. Pia alijaribu kuokoa ajira za watanzania kwa kununua Uchumi Supermarket baada ya kutaka kufungwa, ingawa ilishindikana kutokana na hila za hapa na pale hata hivyo alifungua American Supermarket kuokoa ajira hizo. Sasa anataka kununua Nakumatt na maduka yake (sidhani kama itawezekana kutokana na hila hizo na watanzania watapoteza ajira pamoja na pesa za wafanyabiashara)
  10. Inajulikana kua Yusuf Manji aliomba serikali kuchakata dhahabu ili kuwezesha serikali kupata faida ya kutosha, na pia kufungua kiwanda cha kuunganisha magari
  11. Kuikuza sekta ya madini, Manji anaongea na wataalamu wa madini kutoka India na sehemu mbali mbali, hii ikifanya kazi itaongea inchi mapato makubwa.
  12. Amejaribu kuanzisha maonyesho makubwa Hongkong yatakayoleta wadau wa kubwa wa usafiri Tanzania na pia kukusanya matamasha ya filamu kutoka Zanzibar kuonyesha vivutio vya Tanzania na kuamsha sekta ya usafiri na burudani Tanzania
  13. Kampuni zake zimetengeneza nafasi za biashara wa sanaa za vijijini kwa kuanzisha Duka kubwa la vinyago na sanaa kwa jina la Tanzania Center For Cultural Heritage (TCCH)
  14. Kwenye uwanja wa michezo Manji ameisadia sana Timu ya Yanga, alikua Mwenyekiti na amejaribu sana kuleta makocha bora, mafunzo na mipango ya safari kwa wanachama wake. Wakati Yanga ipo kwenye kilele cha mafanikio Yusuph alijiuzulu badala ya kung’ang’ania madaraka au kutaka kuinunua timu kama ambavyo ingekuwa kwa wengine wengi duniani.
  15. Pia Manji ana mpango wa kuwekeza kwenye kilimo morogoro. Hapa ana mpango wa kuajiri wazawa pekee kwemye viwanda vya sukari na mchele. Mpango wake ni kuifanya Morogoro kuwe kitovu kikubwa cha ajira Tanzania. Pamoja na huduma nzuri za elimu na afya hii itakua sehemu nzuri inayohitajika kwa wazawa kuishi. Ameonekana kwenye Tv akisaini mikataba na kampuni za kutengeneza matrekta kuweka kiwanda morogoro.
  16. Bila kutangaza amekua na madaktari wakitembelea vijijini mara mbili kwa wiki. Pia amekua akitoa huduma za elimu na afya bure kwa maelfu ya wanafunzi wa Mwanza ambako ana kiwanda kikubwa cha kusafirisha samaki.
  17. Watu waliofanya kazi na Yusuf Manji wanasema timu yake ya kazi ni ya ajabu, wanasimama nae hata kwemye matatizo. Mafanikio yake ni juu Yao.
  18. Yusuph Manji alitunukiwa kama 'Mmoja wa viongozi Africa' na pia ofisi yake ilipewa hadhi ya 'House of Lords' kwa kua na umiliki bora wa kibiashara.
  19. Kwa juhudi kubwa za kufanikisha Kata yake kama diwani wa CCM, amejenga miundo mbinu bora, huduma bora za afya, elimu na kuboresha maisha. Amejitoa sana kushiriki shughuli za kijamii.

Anafanya sana vizuri kwemye mitandao kwenye jamii yote ya wafanyabiashara. Sio tu Afrika lakini zaidi ya Asia, Mashariki ya kati na nchi nyinginezo.

Ninachodhani baada ya utafiti, Yusuf Manji hajawahi kupata sifa zake au kutambuliwa na media baada ya jitihada zote za kuleta biashara kubwa mpaka kufungua mall bora ya kwanza Quality Center. Kwa uhakika amebadilisha maisha ya wengi . Kwa ukubwa na ujasiri wake sidhani kama itafikia mwisho wa yeye kuongelewa ongelewa.

Licha ya heshima au ukubwa wake kwenye macho ya watu, Yusuf manji amefanya biashara Dar, mji wenye kasi ya ukuaji kiuchumi kwa njia bora za kibunifu na kutambulisha mengi, kuajiri maelfu na kusaidia maelfu wenye mahitaji. Nitakuachia wewe uamue unamuonaje
Tanzania haiwahitaji watu wa aina ya Yusuf Manji inahitaji wapiga dili wabobezi wajuao kujipendekeza na ambao wanatorosha mali toka ndani kwenda nje wakivuta 10% zao. Tanzania haihitaji wazalendo wa moyo bali wa maneno. Tanzania haihitaji kuona wasio na sisi wakifanya ambayo wenzetu yanawashinda. Tanzania haihitaji watu wenye fikra fikirishi wala wenye akili pembuzi, (Kauli dumazi za hawa ni wenzetu na wale si wenzetu). vimetupelekea kutohoji na wanaohoji wanahojiwa kwanini wanahoji!!! Tunahitajika kuwa mabubusa na viziwi ili mambo yaende kwa maana wako wanaostahili kujenga nchi na wengine watulizane!!!
Nchi inajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye meno.
Wakatabahu nakwenda kunywa maji mkojo upatikane!!
 
Manji ameshawahi kukuibia kitu gani wewe mlalahoi. Taja kimoja tuu alichoiba au kudhulumu uone ulivyo maskini wa fika na roho
Kinachosahaulika ni kwamba wako waliohitajika kuulizwa na si Manji! Je nani hajui viongozi wa Bakwata ndio waliouza na wanaendelea kuuza kama si kujimilikisha mali za waislamu? Badala ya kuhojiwa wauzaji anahojiwa mnunuzi. yaleyale ya badala ya kuhojiwa walioingia mikataba mibovu tunakamata mali za mteja aliyeuingia mkataba!!! Kibaya zaidi wengi wetu hatuna muda wa kutafiti na kuujua ukweli bali kufuata mihemko baada ya kuhemshwa kama sio kupiga vigelegele na nderemo baada ya kuhadithiwa!!!
 
Back
Top Bottom