Fagio laanza kunukia: Mawaziri 13 kikaangoni

Fagio laanza kunukia: Mawaziri 13 kikaangoni

Mawaziri hao ni Prof. Joyce Ndalichako (Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi), Ummy Mwalimu (Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto), Prof. Makame Mbarawa (Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano) na Mhandisi Gerson Lwenge (Maji na Umwagiliaji).

Wengine ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene.

Wamo pia wasaidizi wa mawaziri hao ambao ni Mhandisi Stella Manyanya (Elimu), Dk. Hamis Kigwangalla (Afya), Edwin Ngonyani(Ujenzi), Mhandisi Isack Kamelwe (Maji), Selemani Jafo (Tamisemi) na Dk. Ashatu Kijaji (Fedha).

Chanzo: Nipashe
Sidhani kama unataka kujenga uadui kiasi hicho kwa sasa. Nipashe ni wachokozi.
 
Wamchukue na Makonda akareseat huu ndio wakati wa usajili. Kile cheti alichonacho Gwajima akikitia atakosa pa kuuweka uso wake.
Labda kama Makonda hakupata div 0 vinginevyo Gwajima hawezi kuwa na cheti cha Makonda chenye div 0 kwa sababu vyeti vya aina hiyo haviwezi kuwapo. Sana sana anaweza kuwa na matokeo ya darasa zima ambayo pengine yana namba na kwa hivyo siyo lahisi kujua namba aliyofanyia mtihani Mr. Mako.
 
If anything Selemani Jafo anatakiwa kuwa waziri kamili either Afya or TAMISEMI jamaa anatumia muda kufanya kazi yake na kuzielewa changamoto; tofauti na wengine ambao kutwa kupayuka mambo ambayo ya ovyo kweli.

Selemani Jafo ndio jembe linaloonekana kwenye serikari ya Magufuli.
 
Wenye hatihati ya kukalia kuti kavu ni Nape na Mwigulu, zilizobaki ni propaganda tu.
 
Labda kama Makonda hakupata div 0 vinginevyo Gwajima hawezi kuwa na cheti cha Makonda chenye div 0 kwa sababu vyeti vya aina hiyo haviwezi kuwapo. Sana sana anaweza kuwa na matokeo ya darasa zima ambayo pengine yana namba na kwa hivyo siyo lahisi kujua namba aliyofanyia mtihani Mr. Mako.
Leaving certificate itayotuonyesha alisoma Pamba Sec baada ya hapo matokeo ni hadharani.
 
Akiwatoa hao nani mwingine anafaa? Kwa wabunge waliobaki ccm hao ndio angalau, wengine ni urojo tu na hawafai kupewa wizara yoyote.
 
Hapo walioharibu kazi zaidi ni ndarichako,mpango na kariuki.

Sio mbaya akimtupa makonda kwenye kilimo tuone hizi fujo zake kama zitasaidia kuinua sector ya kilimo
 
Hizo ni habari za vijiweni ambazo mh Rais hawezi kuzifanyia kazi,zilianza kwa Makonda lakini mpaka leo Makonda bado ana dunda.
Issu ya MAKONDA naona kakausha kama alivyokausha kwenye issue ya Jesca ......................!!
 
Huu mchezo hauitaji hasira

Yan hapaa wametajwa vipenzi waaminifu kwa mkuu wameachwa wasiaminika

Hahaha huuuu mwaka Ngosha lazima aombe pooo
 
Tatizo wala siyo mawaziri...libashite likuu lenyewe ndo jipu!
 
Una uhakika hiyo mipango anapanga yeye mkuu?

Mimi nimeshawahi kupewa kamati ya ulinzi kwenye sherehe ya harusi, lakini hapo hapo kila baada ya dakika 10 atakuja kaka wa bwana harusi na kupita na watu wawili wasio na kadi.
Kazi ilikushinda.
 
Hhahahahhaa , umenikumbusha Mbaliiii lol ! Kamati hizi , Binafsi niliwahi kuwa kwenye kamati ya Vinywaji , lakini katikati ya shughuli niliamriwa na Mama wa Bwanaharusi kuhifadhi katoni tano za Heinken na kreti tano za soda !eti kwa ajili ya wageni waliotoka Mkoa , unaanzaje kubisha hapo ....
 
Back
Top Bottom