kisugujira
JF-Expert Member
- Aug 13, 2012
- 773
- 195
WanaJF,
Nchimbi ameng'atuliwa kutokana na kutowajibika ipasavyo! IGP Mwema bado anadunda japo ana kashfa kibao ikiwemo ya upotevu wenye utata wa upanga wa dhahabu wenye thamani inayokadiriwa kufikia shilingi milioni 600 mali ya kanda ya kipolisi kusini mwa Afrika!
Boss wa idara ya uhamiaji ambaye kutokana na yeye kutowajibika, waliochini yake kama waliochini ya IGP kiutendaji, wanapokea rushwa na kuruhusu wahamiaji kuingia na kufanya kazi nchini bila nyaraka zinazotakiwa na hivyo kuhatarisha usalama wa nchi!
Kuna wageni toka India,Pakistan na kwingineko wapo hapa nchini wakifanya kazi ambazo hazihitaji wataalamu toka nje katika makampuni ya kuuza bidhaa zitokazo haraka na kutumika majumbani (FMCG). Wageni hawa hujifanya wamekuja kutembea au kusalimu ndugu na mara muda wao wa kukaa nchini uishapo huondoka kwa muda na kurudi nchini!
Ni nani anayewalinda watu hawa?