Uchezaji wa timu ya simba ni wa kipumbavu Sana. Muda wote wachezaji wanaweza kurudisha mpira nyuma. Kiungo akipokea mpira hawazi kupeleka timu mbele, yeye anawaza kurudisha mpira Kwa mabeki.
Mabeki wakipata mpira hawapeleki mbele wanawaza kumrudishia kipa.
Kama ni mfumo wa kochaz, Basi kocha ni mpumbavu
Hili watu wengi wamelipigia kelele sana hapa jamvini lakini wachezaji wa Simba na benchi lao la ufundi wamegoma kubadilika. Hiki walichokivuna kumaliza msimu bila kombe hata moja ndio wanachostaili. Na mwakani wasipobadilisha mfumo wao wa uchezaji hawatapata kombe lolote. Halafu eti benchi la ufundi litakaa kabisa na uongozi kujadili kwa nini wameshindwa kupata kombe hata moja. Ukiangalia mechi karibu zote za Simba takribani dakika 50 mpaka 60 kati ya 90 za mchezo utakuta mpira ulikuwa unachezwa kwenye nusu yao halafu unategemea timu ibebe kombe labda kombe la kumiliki mpira.
Miaka mitatu/minne iliyopita timu ilikuwa inamiliki mpira huku ina "move" kutoka nyuma taratibu na kwenda mbele bila kupoteza umiliki wa mpira kirahisi. Sasa hivi daa mpira unaanzishwa na Camara unaguswa na mabeki wote wanne na kiungo mkabaji unarudi tena kwa Camara halafu wanarudia hivyo hivyo kama mara tatu hivi ndio baadae sana mpira unaenda mbele. Na usishangae mpira kufika kwenye kibendera cha kona wafungaji wanasubiri krosi golini kwa adui ghafla tu mpira unarudishwa tena nyuma mpaka kwa Camara. Na mbaya zaidi ni wachezaji wa Simba kuridhika na goli mbili/tatu na kuanza ule mchezo wao wakupigiana pasi fupi fupi wenyewe wakiwa wachezaji wawili wa Simba sehemu moja kama wanacheza rede iwapo wachezaji wa timu pinzani wapo mbali nao.
Kuliondoa hili ni lazima kamati ya usajili ya Simba chini ya Mzee wangu Magori kwanza wakubali kuwa hili ni gonjwa sugu kwa sasa pale Simba. Na wakitaka kuthibitisha hili waangalie uchezaji wa Ngoma wakati anakuja Simba na sasa hivi. Ile mipasi ya Ngoma yenye macho kwenda kwa washambuliaji inayouvuka mistari miwili/mitatu ya timu pinzani imekwanda wapi? Ghafla Ngoma naye kajikuta tu bila kujua kaingia kwenye mfumo wa ovyo wa sasa wa kuchezea mpira kwenye nusu yao na kipa wao. Kwa haraka tu ukikuta Simba wanacheza halafu haujaangalia ubao wa matokeo unaweza fikiri kuwa Simba anaongoza goli nane bila ukijatahamaki uangalie ubao unakuta Simba yupo nyuma kashatanguliwa kufungwa.
Ushauri wangu wa bure kwa Mzee wangu Magori na kamati yake ni kuwa katika dirisha hili Simba:-
1.Kwanza itibu ugonjwa sugu wa safu ya kiungo kwa kusajili viungo walau wawili wapya wenye kasi, wenye nguvu, wenye kaliba ya kushambulia/kugeukia mbele, wenye uwezo binafsi wa kupunguza wachezaji wawili/watatu, wenye utulivu hata wakipewa mpira mbele ya wachezaji wa timu pinzani na wenye kiu ya magoli hata kama timu inaongoza goli nyingi wao wanapeleka moto mwanzo mwisho.
2. Kuna beki mmoja wa kati pale Simba ni wa kuachwa tu pamoja na kucheza vizuri lakini yeye kila mechi lazima atoe maboka mawili/ matatu ambayo yameigharimu Simba pakubwa sana mwaka huu kimataifa na kwenye ligi ya ndani
3. Washambuliaji wa kati kama inawezekana waondolewe wote Ateba na Mukwala. Lakini ikishindikana maana kuvunja mikataba nayo inahitaji pesa basi walau mmoja aondolewe kwani wamekosa ufanisi kabisa. Yaani kuna krosi huwa zinapita pale kati ambazo zinahitaji tu mshambuliaji aweke tu kichwa au mguu mpira umgonge uingie ndani ya nyavu lakini hili nalo limewashinda.
Ni mtizamo tu.