Facts: Usiyoyajua kuhusu nchi ya Brazil (Kwa Kiswahili)

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
21,321
50,541
1 Oeresheni kubadili jinsia inafanyika bila malipo kwa hospital I zote za umma na hii iliwekwa kwenye mpango maalumu wa afya wa mwaka 2008

2:Serikali ya brazili husambaza maziwa ya mama (breast milk) bure kwa kina mama wasioweza kiuwanyonyesha watoto wao.

3:No ya pili kwa kuwa na viwanja vya ndege vingi baada ya vinara USA BABY

4: Kama wewe ni mfungwa Brazil basi una uwezo wa kiujipunguzia siku 4 kwenye kifungo chako endapo tu utasoma kitabu chochote na kukiandikia report na kumkabidhi bwana jela kisha mamlaka husika itachambua na utakuwa umepunguza siku 4 za kukaa ndani

5: Wakatoliki ni wengi sana Brazilian kuliko kote owe Spain au italy
64% ni wakatoliki

6:Mji wa Rio de jenero pekee una mashoga wengi sana kwani karibia 20% ya wanaume ni mashoga

7: Asilimia 35% ya wanaume wa maeneo ya vijijin Brazilia wameshawahi\hufanya mapenzi na wanyama

8: serikali ya Brazilian ilitumia $53 million kuandaa ujio wa papa Fransis mwaka 2013 kiasi ambacho wanaharakati walipinga na kulalmika sana

9: Kuna mito mikubwa minne chini ya mto Amazon kizungu inaitwa underground river na huu ni mirefu sana

10: Kwa Mara ya kwanza baran Amerika kusini watapata nafasi kuandaa michuano ya Olympics na itafanyika Brazil mwaka huu

11: Jamii kubwa ya wajapenese waishio nje ya Japan wanapatikanika huko Brazilian

12: 92% ya magari mapya huko brazili yanatumia ethanol kama fuel na inatokana na zao la miwa

13: Mji wa Brasilia una umbo la ndege kma ukiuangalia kutoka juu

14: Usisahau kama ni nchi ya tano kwa ukubwa duniani

15: Miaka ya nyuma Rio del jenero ilishawahi kuwa mji mkuu wa Portugal na kufanya kuwa mji mkuu wa kwanza kwa mabara tofauti

16: Mapinduzi yaliyopeleka brazili kuwa jamhuri hayakupangwa na ni mashahidi wachache tu walishuhudia hata aliyepnduliwa hakujua kinachoendelea unaeza sema ni kama bahati mbaya tu

17: KUDHIBITISHA KAMA KUPATA UTAJIRI NI JUHUDI NA SIO LINGINE BASI 2013 TAJIRI WA KIBRAZILI kwa wakati huo JINA NAMUHIFADHI Alikula hasara ya $30 million na kufilisika kabisa akaanza biashara zake upya na Leo tunavoongea ana utajiri wa $1 billion akishika nafasi ya 7 duniani

18: Simu za apple iPhone ni bei ghali sana brazili Mara mbili ya zinavouzwa marekani

19: Wakimbiaji riadha mwaka 1932 walikuwa na ukata na hela hivyo kipindi wanaenda kushiriki Marathon wakabeba namzigo mkubwa tu wa kahawa ili wawe wanauza njiani pindi wapo safarini ili kukidhi ile hela

20: 1958 rhinoceros aliruhusiwa kuwa mgombea wa kiti cha jumbo LA sao Paulo lakini alishindwa kwenye uchaguzi
 
Ahsante mkuu. Kuhusu hiyo namba 20 inayohusu faru kuwa mgombea katika uchaguzi wa jimbo la Sao Paulo usahihi kwa mujibu wa vyanzo vya taarifa vilivyopo ni kwamba faru huyo aliyekuwa na umri wa miaka mitano alishinda katika uchaguzi huo isipokuwa maafisa wa uchaguzi waliamua kufuta matokeo ya uchaguzi uliompa ushindi faru huyo maarufu. Badala yake wakaitisha uchaguzi mwingine uliofanyika wiki moja baadae.

Cha kujiuliza ni kwamba iweje faru ashiriki kwenye uchaguzi mkubwa kama huo? Jibu ni kwamba wakati huo wananchi wa jimbo hilo walikuwa wamechoshwa sana na hali ya rushwa iliyokithiri, uhaba wa chakula na pia hali ngumu ya maisha kwa ujumla. Hivyo kwenye uchaguzi huo wanafunzi wakaamua kuchapa karatasi nyingi za kura zikiwa na jina la faru aliyekuwa akiitwa Cacareco ambaye alikuwa ni maarufu jimboni humo na akiishi kwenye zoo. Siku ya kupiga kura wananchi wakawa wanatumbukiza karatasi zenye jina lake kwenye sanduku la kura na mwisho wa siku matokeo yakaonyesha kwamba alipata jumla ya 15% ya kura zote. Uvunaji wa kiasi hicho cha kura ulikuwa ni mkubwa kwani zilikuwa ni nyingi zaidi kuliko za wagombea wengine. Kuna baadhi ya wapiga kura wengine ambao waliamua kuweka maharage meusi badala ya karatasi za kura kwenye bahasha za kuwekea kura. Wapiga kura waliamua kufanya hivyo kwa vile waliona ni bora kumchagua huyo kifaru kuliko kumchagua mtu mpumbavu kuwaongoza.

Kingine ambacho kimenitatiza katika habari hii ni kwamba wakati kuna kumbukumbu zinazosema kwamba uchaguzi huo ulifanyika October 1958 pia kuna kumbukumbu zingine zinazoonyesha kuwa ilikuwa ni mwaka 1959.
 
17: KUDHIBITISHA KAMA KUPATA UTAJIRI NI JUHUDI NA SIO LINGINE BASI 2013 TAJIRI WA KIBRAZILI kwa wakati huo JINA NAMUHIFADHI Alikula hasara ya $30 million na kufilisika kabisa akaanza biashara zake upya na Leo tunavoongea ana utajiri wa $1 billion akishika nafasi ya 7 duniani
Hapa umeharibu utafanya nihisi kila ulichoandika ni uongo tu, kwasababu hata Tajiri wa 7 Africa hana utajiri mdogo kiasi hicho
 
17: KUDHIBITISHA KAMA KUPATA UTAJIRI NI JUHUDI NA SIO LINGINE BASI 2013 TAJIRI WA KIBRAZILI kwa wakati huo JINA NAMUHIFADHI Alikula hasara ya $30 million na kufilisika kabisa akaanza biashara zake upya na Leo tunavoongea ana utajiri wa $1 billion akishika nafasi ya 7 duniani
hii chai mabilionea 2000 duniani
Halafu 1$ billion uwe namba 7 :D

Mo Dewji ana 1.2 $ billion ni wa 1700 hivi
 
Hapa umeharibu utafanya nihisi kila ulichoandika ni uongo tu, kwasababu hata Tajiri wa 7 Africa hana utajiri mdogo kiasi hicho
Nashangaa kwa nini mleta mada aseme anahifadhi jina la huyo tajiri aliyefilisika na kuibuka tena kwenye utajiri. Kwa nini asiweke jina lake hadharani kama habari yenyewe ni kweli? Ni Eike Batista?
 
20%ya wakazi wa Rio De Janeiro ni machoko?huoni mji sio watu kukaanga huo.Ila nimewaelewa sana walipompigia kura kifaru haina tofauti na kura za maruhani za zenj waqt uleeee.
 
Back
Top Bottom