Fact: How Kilimanjaro ended up in Tanzania

Dah hii storia mbona hupotoshwa sana, wazungu wa mwanzo kuja Kilimanjaro walikuwa wa German na wakaanza kuitawala Kilimanjaro, na Waingereza wao walikuwa tayari huko Kenya na walitaka iwe settler economy, na hata mipaka ilijulikana na ndio maana hata kipindi ma mangi walipokuwa wanakimbia ubabe wa kiutawala wa German ka adhabu walikuwa wanapewa hifadhi na Waingereza upande wa Kenya huko, pia hii migawanyo ilikuwa inatolewa kulingana na mzungu aliye wahi kufika eneo husika, so Germans walikuwa interested zaidi na Kilimanjaro maana waliwahi kufika na mipaka ilieleweka hivo.
Mpendwa, historia halisi ni kidogo tata zaidi.
Mzungu wa kwanza wa kufika karibu na Kili alikuwa Mjerumani Rebmann, aliyetoka Mombasa akiwa misionari katika utumishi wa CMS, shirika la kianglikana kutoka Uingereza. Baadaye wazungu mbalimbali walipita, zaidi Waingereza. Wamisionari walioanza kazi huko walikuwa Waingereza (bado hakuna Kenya wala DOA (=Deutsch Ostafrika = Afrika ya Mashariki ya Kijerumani).

Nchi iliyojaribu kuenea hapa ilikuwa Zanzibar maana walitaka kudhibiti njia za misafara na maziwa makuu. Lakini Zanzibar ilkuwa dhaifu mno. Kituo chao cha mwisho ilikuwa ngome karibu na Muheza.

Wakati Mjerumani Peters alianza kuzunguka barani (Usagara)1884 na kutafuta watu wanaosaini mikataba yake, balozi wa Uingereza huko Z'bar alitaka Sultani (ambaye Mwingereza alimthibiti) kueneza utawala wake barani hakupenda Wajerumani waenee zaidi. Hivyo alimtuma Johnston Kilimanjaro. Baadaye 1885 alituma kikosi cha jeshi la Zanzibar waliowahi tar 30 Mei 1885 kabla ya Wajerumani kupata mikataba na machifu wa Kilimanjaro, kama Mandara wa Moshi, Fumba wa Kilema, na Marealle wa Mamba , baadaye pia na Sina.

Wajerumani chini ya Bw Jühlke walifika 19 Juni 1885, na Mandara wa Moshi alifanya mkataba nao pia. Huo mkataba wa pili ulikuwa msingi wa madai ya Wajerumani kuhusu Kilimanjaro. Hivyo Jühlke alikuwa mkoloni Mjerumani wa kwanza kufika huko, baada ya Waingereza mbalimbali. (bado haikuwa eneo la koloni ya kiserikali ya Ujerumani, ilikuwa bado eneo la kampuni binafsi Deutsch-Ostafrikanische Gesellschaft)

1886 Wajerumani na Waingereza walianza kuwasiliana juu ya swali hili. Wajerumani hawakutaka kutambua Zanzibar kama nchi kamili na hivyo kukataa mikataba yake; Waingereza waliona Zanzibar ni dhaifu mno (na miaka mitatu baadaye waliamua kuichukua chini ya mamlaka yao kabisa), hasa walitaka mapatano kuhusu Uganda na Ulaya, hivyo waliamua kuacha mambo ya Kilimanjaro.

Yote yanapatikana, kwenye intaneti unapata taarifa ya Johnston na barua / mikataba bana ya serikali, nimeonyesha chanzo juu. Matokeo ni taarifa ya Johnston na mikataba yake na Taveta aliyouza baadaye kwa kampuni ya kiingereza kwa afrika ya mashariki. Hayo yooote miaka kabla ya wazo la "settler colony" halikuzaliwa.
Ukitaka elimu na habari halisi badala ya maneno matupu, kuna tasnia nzuri ya Gabriel Ekemodi (sasa profesa kwenye Chuo Kikuu cha Ife, Nigeria) kuhusu German Rule in North-East Tanzania, 1885-1914. PhD thesis. SOAS University of London. DOI: https://doi.org/10.25501/SOAS.00033905
Unafungua kwa link hiyo: https://eprints.soas.ac.uk/33905/1/11015630.pdf
 
hawawezijua hata kwann makao makuu ya Lutheran church yako Kilimanjaro! Wanasau missionaries walikuwa agents wa ukoloni!
 
Karl Peters alipita kabla ya 1884! 1884 ilikuwa conference on partition of africa Berlin!
 
Kaka mboni huulizi kama hujui? Au hujui kwamba hujui?
Mangi Rindi wa Moshi alialika wamisionari wa kwanza Moshi ambao walikuwa Waanglikana wa CMS (Church Missionary Society). Walifika 1885, kabla ya Wajerumani. (Rebman mwaka 1848 alikuwa pia misionari wa CMS). Waliendelea hadi 1893. Baadaye waliondoka wakakabidhi kazi kwa Walutheri wa misioni ya Leipzig. Sababu ilikuwa kwamba Wajerumani walipigana na Wachagga kijesi wakaona kwamba Wachagga wanaamini wamisionari Waingereza hivyo CMS walipaswa kuondoka. Hivyo Walutheri walifika Kilimanjaro hata baada ya Wakatoliki (1890) .

Unadhani kweli kwamba na machache unayokumbuka kutoka shule unaweza kubisha?
 
Karl Peters alipita kabla ya 1884! 1884 ilikuwa conference on partition of africa Berlin!
Jaribu kujisomea kidogo. Hupendi kujielimisha angalau kidogo kabla ya kuandika hapa na kumwaga maneno kama "ujinga"??
Soma Karl Peters - Wikipedia, kamusi elezo huru

Peters alipoandaa safari yake mataifa ya Ulaya yalikuwa yakiandaa mkutano wa Berlin kuhusu masuala ya Kongo. Mkutano huo, ulioanza Desemba 1884, ulisababishwa na juhudi za mfalme Leopold II wa Ubelgiji kujijengea himaya ya binafsi katika beseni la Kongo akigongana na shabaha za Ufaransa, Ureno na Uingereza.
Tarehe 10 Novemba 1884 Peters alifika Unguja pamoja na wanakamati wawili ili aendelee kuzunguka kwenye bara. Serikali ya Kijerumani ya Chansella Bismarck haikukubali mipango yake kwa sababu iliogopa vurugu kwenye mkutano ulioitishwa tayari. Hivyo Peters alipofika kwenye ubalozi wa Ujerumani mjini Zanzibar alipokewa kwa barua kutoka Berlin iliyosema ya kwamba hawezi kutegemea msaada wowote kwani juhudi zake ziko nje ya siasa ya nchi.

Peters akimwogopa Sultani pamoja na Waingereza alivuka kwa siri kutoka Unguja kwenda bara. Alifaulu kutembelea masultani au machifu kadhaa waliotia aina ya sahihi kwenye karatasi walizoonyeshwa na Peters. Karatasi hizo ziliandikwa kwa lugha ya Kijerumani zikisema ya kwamba chifu fulani aliweka eneo lake chini ya mamlaka ya shirika la Kijerumani pamoja na kulipatia shirika hilo haki ya kutumia maeneo na malighafi yote. ...

Kwa njia hiyo katika muda mfupi kati ya tarehe 23 Novemba na 17 Desemba 1884 Peters alipata hati kutoka watu alioita machifu wa Usagara, Nguru, Useguha na Ukami kwa ajili ya shirika lake, jumla eneo la km² 140,000.

Peters hakufika Kilimanjaro wakati ule (miaka baadaye tu). Wala hapakuwa na majadiliano kuhusu Kilimanjaro au kuhusu Afrika ya Mashariki kwenye Mkutano wa Berlin. Ukitaka kupinga, lete ushuhuda. Bila ushuhuda heri unayamaze au uombe kuelimishwa.
 
Mimi nina website ya archives za Kijerumani!
 
Safi! Mimi pia. Mimi nimekuonyesha tayari links ninazorejelea. Wapi links zako zinazothibitisha unachodai?
Karl Peters was in Tanganyika first in 1875!

Continued English disdain for Germany later gave rise to a great tale about Kilimanjaro. The well-known story goes that Kaiser Wilhelm wrote to QueenVictoria asking that Kili be assigned to German East Africa. He pleaded that the British Crown Colony already had one snow-capped peak in its Kenyan domain, while Germany had none. The Queen, in a typical English spirit of fair play, magnanimously assented, giving the mountain as a birthday gift to her grandson, the future Wilhelm II. It's a great yarn, one that has endured the test of time. But there is no truth to it. Carl Peters had sneaked into Tanganyika and persuaded various Chagga chieftains to sign treaties agreeing to cede their territories to his Society for German Colonization.
 
Karl Peters was in Tanganyika first in 1875!

Hakika Peters hakufika Afrika mwaka 1875!! Kama ungejisomea kidogo tu, ungetambua: Peters alizaliwa mwaka 1856. Kwa hiyo mwaka 1875 alikuwa na umri wa miaka 19. Mwaka ule alimaliza shule ya sekondari akajiandaa kwenda Chuo Kikuu cha Göttingen.
Kaka ulituahidi kuonyesha "archives za Kijerumani"?? Badala yake unaweka link kwa tovuti binafsi ya Mwingereza anayekusanya vitu vingi kuhusu Tanzania, lakini bila kuchungulia usahihi, anachukua chochote.
Wapi archives zako?
Lini utaanza kujieelimisha kwanza kabla ya kutangaza habari (na kutumia matusi kama "ujinga" ukikuta habari mpya??)

Ushauri: usiamini kitu kwa sababu ulikiona mahali fulani kwenye intaneti. Intaneti ni nzuri, kutumia google ni nzuri LAKINI unapaswa kulinganisha habari na kutumia akili. Jaribu tu!
 
Back
Top Bottom