Mwanamkiwi
JF-Expert Member
- Mar 7, 2019
- 2,023
- 2,399
Mpendwa, historia halisi ni kidogo tata zaidi.Dah hii storia mbona hupotoshwa sana, wazungu wa mwanzo kuja Kilimanjaro walikuwa wa German na wakaanza kuitawala Kilimanjaro, na Waingereza wao walikuwa tayari huko Kenya na walitaka iwe settler economy, na hata mipaka ilijulikana na ndio maana hata kipindi ma mangi walipokuwa wanakimbia ubabe wa kiutawala wa German ka adhabu walikuwa wanapewa hifadhi na Waingereza upande wa Kenya huko, pia hii migawanyo ilikuwa inatolewa kulingana na mzungu aliye wahi kufika eneo husika, so Germans walikuwa interested zaidi na Kilimanjaro maana waliwahi kufika na mipaka ilieleweka hivo.
Mzungu wa kwanza wa kufika karibu na Kili alikuwa Mjerumani Rebmann, aliyetoka Mombasa akiwa misionari katika utumishi wa CMS, shirika la kianglikana kutoka Uingereza. Baadaye wazungu mbalimbali walipita, zaidi Waingereza. Wamisionari walioanza kazi huko walikuwa Waingereza (bado hakuna Kenya wala DOA (=Deutsch Ostafrika = Afrika ya Mashariki ya Kijerumani).
Nchi iliyojaribu kuenea hapa ilikuwa Zanzibar maana walitaka kudhibiti njia za misafara na maziwa makuu. Lakini Zanzibar ilkuwa dhaifu mno. Kituo chao cha mwisho ilikuwa ngome karibu na Muheza.
Wakati Mjerumani Peters alianza kuzunguka barani (Usagara)1884 na kutafuta watu wanaosaini mikataba yake, balozi wa Uingereza huko Z'bar alitaka Sultani (ambaye Mwingereza alimthibiti) kueneza utawala wake barani hakupenda Wajerumani waenee zaidi. Hivyo alimtuma Johnston Kilimanjaro. Baadaye 1885 alituma kikosi cha jeshi la Zanzibar waliowahi tar 30 Mei 1885 kabla ya Wajerumani kupata mikataba na machifu wa Kilimanjaro, kama Mandara wa Moshi, Fumba wa Kilema, na Marealle wa Mamba , baadaye pia na Sina.
Wajerumani chini ya Bw Jühlke walifika 19 Juni 1885, na Mandara wa Moshi alifanya mkataba nao pia. Huo mkataba wa pili ulikuwa msingi wa madai ya Wajerumani kuhusu Kilimanjaro. Hivyo Jühlke alikuwa mkoloni Mjerumani wa kwanza kufika huko, baada ya Waingereza mbalimbali. (bado haikuwa eneo la koloni ya kiserikali ya Ujerumani, ilikuwa bado eneo la kampuni binafsi Deutsch-Ostafrikanische Gesellschaft)
1886 Wajerumani na Waingereza walianza kuwasiliana juu ya swali hili. Wajerumani hawakutaka kutambua Zanzibar kama nchi kamili na hivyo kukataa mikataba yake; Waingereza waliona Zanzibar ni dhaifu mno (na miaka mitatu baadaye waliamua kuichukua chini ya mamlaka yao kabisa), hasa walitaka mapatano kuhusu Uganda na Ulaya, hivyo waliamua kuacha mambo ya Kilimanjaro.
Yote yanapatikana, kwenye intaneti unapata taarifa ya Johnston na barua / mikataba bana ya serikali, nimeonyesha chanzo juu. Matokeo ni taarifa ya Johnston na mikataba yake na Taveta aliyouza baadaye kwa kampuni ya kiingereza kwa afrika ya mashariki. Hayo yooote miaka kabla ya wazo la "settler colony" halikuzaliwa.
Ukitaka elimu na habari halisi badala ya maneno matupu, kuna tasnia nzuri ya Gabriel Ekemodi (sasa profesa kwenye Chuo Kikuu cha Ife, Nigeria) kuhusu German Rule in North-East Tanzania, 1885-1914. PhD thesis. SOAS University of London. DOI: https://doi.org/10.25501/SOAS.00033905
Unafungua kwa link hiyo: https://eprints.soas.ac.uk/33905/1/11015630.pdf