fimboyaukwaju
JF-Expert Member
- Aug 3, 2020
- 5,608
- 7,167
Kwa watu mlioishi bukene miaka 45 iliyopita,mtakuwa mnamfahamu mtu huyu.Ni mbulushi ambae alikuwa tajiri sana na alikuwa ndio rais wa bukene.Wabulushi wa Tanzania nzima walikuwa wakimheshimu sana.Alisaidia sana watu wa bukene,kila mwenye shida alikuwa anaenda kwake.Alikuwa rafiki ya baba yangu na walikuwa wanatembeleana sana.Nami nilikuwa naenda kwake kutembea.Kuna wakati walikuwa wanafanya maongezi marefu sana na baba yangu huku wakiandika notes nyingi,japo sikuwa naelewa nini wanafanya.Alitoa misaada misikitini,makanisani,mashuleni na kwa wafanyakazi wake.Kama kuna mtu wa bukene humu anaweza kuongezea juu ya mtu huyu amba pia alitoa ajira kwa watu wengi,na kwa taarifa yenu huyu ndiye aliyempa mtaji baba yake rostam aziz kuanzisha duka kule mwisi,wilayani igunga