Ezekiel Malongo alisababisha niharibu Kanda ya TOT

Wazee wa Soka huyu Mwiraq Ezekiel Malongo mnamkumbuka? Alikuwa RTD miaka ya 2000.

Kiukweli alituvutia vijana wengi tukaupenda mpira. Alikuwa akiitangaza mechi ya Simba na yanga nilikuwa hata sitaki niangalie mechi kwa TV.

Akianza kukuchanganyia majina Joseph Kaniki Golota fagio la chuma.. I miss those days.

Yupo wapi huyu Legend. Alifanya nikarecord Kanda nzima ya TOT ya kifo cha Nyerere sauti ya kumwigilizia. Nilipokuwa nakua nilijua nisipotangaza mpira kama Malongo basi nitaimba kama Komba.

Huyu fundi yupo wapi?
Kafariki baada ya kuwa na msongo wa kusemwa eti alikuwa anajihusisha na mapenzi ya jinsia moja na alikuwa chakula ya mtu mzito sana hapa duniani Tanzania.
 
Nimemfaidi tu Mwameja tu mkuu.

Hivi tulishawqhi kupata Golikipa kama huyu?
Sijaona kama tumeshapata kipa kama MOHAMMED MWAMEJA tena. Jamaa alikuwa Kiongozi uwanjani, kule golini alikuwa mkali/mbabe kwa mabeki wazembe (sometimes aliwapiga makofi walipozingua), ikitokea kuna penati zinapigwa tulikuwa na uhakika wa 100% lazima kuna penati 1 au 2 atazificha, na lazima itakuwa hivyo.

JUMA KASEJA alijaribu na alifanya kwa kiwango kikubwa, ila hakufika kwa Mwameja. Huyu MUSA CAMARA naye yuko vizuri ila kwa Mwameja badooo saaana. Musa Pinpin Camara hazungumzi awapo golini na wala siyo aggressive kwa mabeki wazembe.

Mwaka 1993 kama siyo 1994 aliwakera Wasudani hadi wakazima taa za uwanjani na kumwangushia kipigo yeye na Wachezaji wenzake wa Simba. Walishonwa nyuzi kadhaa kutokana na kipigo kile. Hii Simba imesumbua Waarabu miaka mingi mno.
 
Wazee wa Soka huyu Mwiraq Ezekiel Malongo mnamkumbuka? Alikuwa RTD miaka ya 2000.

Kiukweli alituvutia vijana wengi tukaupenda mpira. Alikuwa akiitangaza mechi ya Simba na yanga nilikuwa hata sitaki niangalie mechi kwa TV.

Akianza kukuchanganyia majina Joseph Kaniki Golota fagio la chuma.. I miss those days.

Yupo wapi huyu Legend. Alifanya nikarecord Kanda nzima ya TOT ya kifo cha Nyerere sauti ya kumwigilizia. Nilipokuwa nakua nilijua nisipotangaza mpira kama Malongo basi nitaimba kama Komba.

Huyu fundi yupo wapi?

Umeishia kuwa mnenguaji kama Zuchu. Ndo maisha yalivyo hasa kama kuna one target.
 
Wazee wa Soka huyu Mwiraq Ezekiel Malongo mnamkumbuka? Alikuwa RTD miaka ya 2000.

Kiukweli alituvutia vijana wengi tukaupenda mpira. Alikuwa akiitangaza mechi ya Simba na yanga nilikuwa hata sitaki niangalie mechi kwa TV.

Akianza kukuchanganyia majina Joseph Kaniki Golota fagio la chuma.. I miss those days.

Yupo wapi huyu Legend. Alifanya nikarecord Kanda nzima ya TOT ya kifo cha Nyerere sauti ya kumwigilizia. Nilipokuwa nakua nilijua nisipotangaza mpira kama Malongo basi nitaimba kama Komba.

Huyu fundi yupo wapi?
Alisha danja kitambooo
 
Ila pia Majina ya wachezaji yalikuwa yanavutia saana.

Joseph Kaniki
Ali Mayai Tembele
Jembe Ulaya
Juma Kaseja
Kisha wakaja Kina Boniface Pawasa....
Said mwamba kizota
Said maulid SMG
Jerryson Tegete
Fred mbuna
Ulimboka mwakingwe
 
Kuna ile fainali ya Simba vs Stella Abdjan Kombe la CAF mwaka 1993 Watangazaji wa RTD walinikosha sana. Maandalizi na shamra shamra vilikuwa vya moto sana kuliko hata hiyo Jumapili ya Simba vs Berkane huko Zanzibar.

1.Golini yupo Tanzania One Mohammed Mwameja (Captain)
2.Kasongo Athumani Mhaya
3.Deo Mkuki

Oya hao niliowataja walikuwa balaaa haswaaa. Pale Simba, mbavu za kulia na kushoto, wamepita akina Ramadhani Wasso, Juma Jabu, Nassoro Masoud Chollo, nk. ila hao niliowataja mwanzo walikuwa balaaa haswaaa.

Apumzike salama Ezekiel Malongo.
Hii siku nitaikumbuka daima!
 
Acha kujitia aibu we kitoto cha 2000. Hao Akina Wasso, chollo n.k si wa jana tu?
 
Najitiaje aibu hapo? Mimi nimeonyesha full backs waliocheza baada ya Kasongo Athumani na DEO Mkuki (hata kama siyo kwa mtiririko mzuri) kwamba hawakufikia ubora wa hao niliowataja. Ningekuwa wa 2000 ningemuona Mrage Kabange au Twaha Hamidu wakicheza?
 
Ezekiel Malongo beki wa kupanda na kushuka alikuwa muongo sana, worldcup ya mwaka 2002 alitudanganya sana
wc 2002 umenikumbusha mbali sana, nilikua kuchunga siku hio na kiredio changu, mishale ya saa 4-6 asubuhi hivi senegal anapigwa na turkey goli la dhahabu.......

.....afrika kwaheri, afrika bye bye, afrika nje........

ezekiel malongo alikua mwongo sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom