Umenikumbusha mbali sana,nilikua naishi kwa baba mkubwa mke wake alikua na mtt wa kiume huyu dogo alikua anipendi hata kidogo chakula tulikua tunakula kwa pamoja ila yeye hataki kukaa karibu na Mimi hata kidogo na ninapopamba mboga hyo sehem yeye hapambi ilikua ni shida sana!
Dogo alikua na matusi sana kijana navumilia TU.
Siku Moja likizo tukaenda nyumbani kwetu Kijiji huko Mkoa X huko ndyo kwetu na ni chimbuko la wazazi wetu na wazazi wangu wote wapo huko na mama alikua maejifungua kadogo 2000's. Sasa yule Dogo akajichanganya eti anampiga yule Dogo ambaye tulimkuta anatambaa sijui sababu ilikua ni nini aisee nilimzibua Kofi Moja matata sana Hadi vidole vikajichora kwenye shavu lake nafikiri ingelikua ni hichinkipindi Cha utandawazi angepiga picha na kumpigia simu mama yake na baba mkubwa sizani kama ningendelea kuishi dogo alikua kutwa mzima na alizila kula mchana nikajisemea kimeumana.
Tulivyorudi nikawa na wasi wasi lakini baada ya masiku kupitia dogo akawa anarudia Tena upuuzi wake bi mkubwa ambaye mama yake akaniambia huyu usimchekee mzibue kama ulivyomzibua mkiwa kwenu, nikajisemea moyoni kumbe habari zilifikaaa.
Hivi sasa dogo tunafanya kazi wilaya Moja na ananizamu kubwa sana juu yangu hakuhi kuniamkia kipindi Cha utototl wake alianza baada ya kuja kufanya kazi huku nilipo na nilimpokea vizuri sana Hadi hivi sasa humwambi kitu kibaya kinachonihusu na akakuamini Hadi Hadi wazazi wake alienda kumwambia kaka ni mtu mzuri sana.
Siku Moja baba mkubwa ananipogia simu mdogo wako anakusifu ulimpokea vizuri! Aisee hyo siku nilibwabwaja nilimchana Mzee kinoma!
Nilimuliza kwa kwa hyo mulikua na wasisi kwa nini huyu ni mdogo wangu au mlikua na wasiwasi kwa matendo mliyonitendea mnazani na Mimi nitarudisha kwa huyu dogo!?
Dingi akasema acha kukumbusha hayo yalishapita nitakupigia baadae. Hyo siku nilitema nyongo.