Hawa jamaa mimi wameshawahi niumiza.
Nilitumia Mastercard ya Standard Chatered kutoa pesa Exim, nilipokwenda siku nyingine kuangalia salioa nikakuta salio limepungua.
Nikajaribu tena kutoa siku nyingine tatizo likajirudia. Nikawasiliana na account manager wangu kule Standard Chatered akaniambia inabidi nirudi katika Branch ya Exim nilipotolea hela ili ni file complains nao waangalie.
Nikaomba nitumiwe record yangu ya kutoa na kuingiza pesa (sijui mnaitaji kwa lugha ya kibenk au Kizungu), sikuona popote ambapo hela ninayoidai ikionyesha kutolewa.
Just imagine unagundua tatizo ukiwa Nairobi, Branch yako ipo Mbeya, ulipotoa hela mara ya mwisho ni Milmani City, how can one afford such a disturbance?