Naomba niulize maswali yangu mawili mapema, kwakuwa sijui kama nitabahatika kuungana nanyi hapa siku ya j1:
1. Kwa uzoefu wangu wakufuatilia nakujua mifumo ya uundaji katiba ktk baadhi ya mataifa ambayo sisi hupenda kuakisi ni kuwa, katiba hutengenezwa na chombo kiitwacho BARAZA LA KATIBA, Je Mh waziri, mfumo wetu wakutumia TUME unatuaminishaje kuwa tume hii itatuletea Katiba ya kiraia/umma?
2. Kwamujibu wa sheria ya kutunga katiba mpya iliyosainiwa kabla ya uundwaji wa tume husika, moja ya mambo muhimu inampa rais wa nchi mamlaka ya:
(a). Kuteua tume ya katiba, (b). Hadidu za rejea zitapelekwa kwake, (c). Atakaa na rais wa Zanzibar nakuamua kuitisha kura ya maoni.
Kwakuzingatia sheria hiyohiyo, Je inampa rais wa nchi mamlaka kupendekeza na kuingiza mawazo/matakwa yake kwa ukomo gani? na nani anasimamia uingizaji wa mawazo hayo ya rais wa nchi kwenye mchakato huu wa katiba?