Exclusive. Hatimaye Nabii Frank afichua Kiini cha Mauaji ya Kibiti na Rufiji

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,216
Akizungumza mapema asubuhi ya leo na Kituo cha Luninga cha Channel Ten na Magic fm Radio Nabii anayekuja kwa Kasi nchini Nabii Frank leo amefunguka na kueleza mambo makuu mawili ambayo ndiyo chanzo cha mauaji yanayoendelea Kibiti na Rufiji na amezitaka Mamlaka husika kuyafanyia Kazi ili kumaliza mauaji.

Amesema kwamba mauaji hayo yanatokana na sababu za Harakati za Kidini ( yaani kuna dini moja inataka kuwa ndiyo inayoaminika na kukubalika katika huo Ukanda hivyo wanaua Watu hasa wa dini fulani ili kuwatisha na wakimbie au wahame hayo maeneo na wabaki wao tu ) na sababu ya pili kasema kwamba Mfumo wa Kiuchumi wa Watu wa hayo maeneo umeharibiwa hivyo Wauwaji wameamua sasa kuwauwa wale wote ambao wanahisi ndiyo chanzo cha Mfumo wao huu kuharibiwa. Na inasemekana kwamba Mfumo mkubwa wa Kiuchumi au uingizaji Kipato kwa asiimia kubwa ya Watu wa hayo maeneo ni Mkaa na kama tunavyojua Serikali imepiga marufuku huku ikiweka Sheria kali dhidi ya wale watakaokamatwa.

Nawasilisha.
 
Mpaka sasa waliouawa ukiangalia kwa majina wengi ni wa dini moja, ambayo ni wengi maeneo hayo , sasa sijui anasemaje Nabii Wetu....

"Wanaosadikiwa kupoteza maisha ni Hamid Kidevu,Yahaya Makame na Moshi Machela" - Usiku wa jana 8/6/2017
 
Mpaka sasa waliouawa ukiangalia kwa majina wengi ni wa dini moja, ambayo ni wengi maeneo hayo , sasa sijui anasemaje Nabii Wetu....

"Wanaosadikiwa kupoteza maisha ni Hamid Kidevu,Yahaya Makame na Moshi Machela" - Usiku wa jana 8/6/2017
Wa dini gani!??
 
nimecheka sana kwa huu Uzi wako kwamba Nabii Anaekuja kwa kasi kumbe Nabii anakuja kwa kasi haaaa,haaaaaa
 
Back
Top Bottom