Tukijadili mada na kuachana na wake wa Chiluba, tutaona kuwa Zambia ipo njiani kutengeneza mustakabali wao. Hii ni nchi ambao haikuwa na tofauti kubwa sana kiuchumi ikilinganishwa na Tanzania, na pia sera zao zilifanana kwa kiasi kikubwa. Nadhani mweno hata wa GPD-per capita yao uko juu ya kwetu.
Wazambia wametushinda kwa kitu kikubwa kimoja tu, wameamini kuwa yeyote sio lazima awe UNIP anaweza kuongoza nchi, waliweza kubadilisha utawala kutoka chama kimoja kwenda kingine, ambapo huu unaweza kuwa urithi mzuri walioupata. Ikumbukwe kuwa Chiluba alitokea kwenye chama cha upinzani, na ndiye aliyekuwa wa kwanza kumwandama Kaunda!
Ninachojaribu kusema hapa sio kulipiza kisasi, ila ni mageuzi ya kwanza kutokea kuweza kumwandama Rais aliyekutangulia pale ambapo alifanya madudu.
Naamini haya yamewezekana Zambia kwa sababu wanachi walithubutu kubadilisha serikali, na alieingia tayari alikuwa na ile kitu tunaita kuthubutu, kwakuwa kwanza tayari alikuwa ashapata sulubu nyingi kabla ya kupata nafasi ya kuongoza nchi.
Tukichukua mfano mwingine, ni ukweli usiopingika kuwa kama Tzavingirai angekuwa rais wa Zimbabwe, basi angewawajibisha kina Mugabe na wengine walioiharibu nchi ile, lakini kama angetokea kiongozi mwingine ndani ya ZANUPF ingekuwa vigumu kuwawajibisha kwakuwa tayari nao walikuwa sehemu ya mfumo. Sisemi kuwa haiwezekani, ila ni mara chache sana na ni kwa watu wachache ambao hawatabiriki, sijui kama Mkuu wetu wa Kaya anaweza kuwa mmoja wao.
Lakini jambo la kufurahisha ni kuwa huu umeanza kuwa mwendo mzuri, wameanza Zambia, wako Malawi, kwa hiyo huu unaweza kuwa upepo wa kisulisuli, siku moja hata hapa kwetu unaweza kuwepo. Wakati huo ndio wote wanaopewa au kuomba madaraka watakuwa na moja tu, nalo ni NINI WATAWAFANYIA WATANZANIA.
Hoja yangu sio kuwa ni kuiondoa ccm madarakani, la hasha, hoja ni kuwa nayo ccm pamoja na uma ufahamu, uamini na kukubali kuwa yeyote anaweza kuongoza dola! Wakifikia hapo, mabadiliko makubwa yataonekana Tanzania kwa kasi ya ajabu.