Hivi hamjui kama kupanda kwa bei ya mafuta, maji na umeme kunainufaisha EWURA? Kwa mfano EWURA inapata 1% kwa kila kiasi kinacholipwa na mteja wa TANESCO, bei ya umeme au mafuta ikipanda na wao mapato yanapanda kama wafanyabiashara. Hivyo naona hawa wanafanya mazingaombwe tu. Hizi hela zinawafanya watanue bila kufanya kazi yo yote ya maana kwa mwananchi wa kawaida. nashauri wapatiwe fedha za kuendeshea shughuli zao moja kwa moja toka kwenye bajeti ya serikali ndipo watakapoweza kudhibiti bei ya huduma hizo kikamilifu, vinginevyo bei za nishati zitaendelea kupanda kila siku na inawezekana wanashirikiana na waingizaji wa mafuta.