Ewura haina mgao wa bajeti?

mbasamwoga

Member
Jul 6, 2011
70
12
Tanzania ina mamlaka kadhaa zikiwemo tfda, tcra, sumatra, ewura n.k
lengo hasa la hizi mamlaka zilikuwa kuhakiksha mtanzania anapata ubora na unafuu katika maeneo husika ya hizi mamlaka. Lakini badala yake hizi mamlaka leo zimegeuka mzigo kwa watanzania.......
Chukulia mfano ewura....

Kila ukinunua umeme kwa luku wanakata asilimia 20 ya hela yako. Mfano ukienda kununua umeme wa 10,000/ wanakata 2,000/
jamani ewura.......
Kila lita moja ya mafuta wanaongezea tsh. 200/ yaani badala ya dizeli kuuzwa 1700 itauzwa 1900 ili ewura wapate mgao
bado kwenye maji mchezo uko vilevle
bado kwenye gesi mchezo uko vilivile

yaaaaaani nasikia hasira. Hivi hii ewura haina mgao wa bajeti serikalini?????????????? kwanini inawanyonya watanzania?????


nimechoka na huu utawala niliwapa kula yangu kwa makosa sana, eee mungu nisamehe.......................

Hebu wataalamu mnisaidieni kweli ewura wanategemea hivi vijisenti.......... Au wanatafuta za kuchangia mpitisho wa bajeti???????

Nataka majibu wadau mnafanya mpaka mzuka unapanda niipasue laptop yangu......
 
Mbasamwoga,

Pole sana kwa kutooelewa unacholipia, ingawa unaelewa lengo la kuanzisha mamlaka za TCRA, SUMATRA, FCC, EWURA na kadhalika. Kwanza kabisa, si kweli kuwa matunda bora ya kuwa EWURA huyaoni. TANESCO ilipoomba nyongeza ya bei za umeme ya asilimia 36 na Serikali kubariki ombi hilo, EWURA ilikataa na kuruhusu ongezeko la asilimia 21.7 tu. Mwaka jana TANESCO iliomba ongezeko la asilimia 65, EWURA ikaruhusu ongezeko la asilimia 18.5 tu. Unachokiona kwenye bili yako ya umeme ni asilimia 18 ya Kodi ya VAT kwa TRA na asilimia 1 tu ya huduma za EWURA. Mathalani, ukilipa TShs 10,000/= basi TShs 8,403.36 kni mali ya TANESCO kwa kukupatia huduma ya umeme, TShs 1,512.61 hulipwa TRA ikiwa kodi ya VAT, na TShs 84.03 hulipwa EWURA kwa huduma wanazozitoa (mbona kiasi hiki ni kidogo). DAWASCO imegalagazwa mara nyingi tu wakitaka kutuuzia UPEPO badala ya MAJI.

Kwenye mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa, EWURA hulipwa TShs 6.70 (kwa kila lita ya petroli), TShs 6.10 (kwa kila lita ya dizeli) na TShs 3.40 (kwa kila lita ya mafuta ya taa). Kumbuka kazi liyofanywa na EWURA mwezi Januari 2009 (wauza mafuta walipogoma kuteremsha bei za mafuta kwa miezi 6 baada ya pipa la mafuta ghafi kushuka kutoka Dola za Marekani 140 hadi 40 kwa siku moja na kuendelea hivyo kwa zaidi ya miezi 10). EWURA ilipitisha kanuni ya kukokotoa bei na kuwalazimisha kuteremsha bei kisheria. Juzi EWURA iliposhusha bei kwa asilimia 9 tu (kisheria na kiuhalali), kilichotokea kama sio mgomo ni nini? Serikali ilijaribu kuwakaripia tarehe 3 Agosti, wadosi wakaipa shinikizo la saa 24 za kufyata mkia. Tulishuhudia EWURA ilivyowashukia mambo yakatulia. Kwa hivi karibuni, sijaona MAMLAKA imara kama EWURA. BP Tanzania kashika adabu yake, Mkurugenzi Mtendaji na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wanakabiliwa na kesi (kwa usahihi, KIFUNGO) kwa kukaidi amri hali ya EWURA.

Ndugu Mbasamwoga, nikukumbushe kuwa asasi na taasisi zinazopokea mshiko kutoka HAZINA mambo yake si shwari (kutembeza bakuli kwa sana, madudu matupu, huduma za ovyo). Waulize wanaofanya biashara za mafuta jinsi walivyokaliwa kooni na EWURA wakizima uchakachuzi wa mafuta, au TANESCO ambayo wangetamani kuongeza bei za umeme hata kama wanagawa GIZA. Mnyonge mnyongeni, bali haki yake mpeni. EWURA, tafadhali endelea kukaza kamba. Tunajua kuwa Wizara ya Nishati na madini inawaingilia (eti kusimamia mipango isiyotekelezeka) dai majukumu yenu ili mtuondolee mgawo na kuhakikisha kuwa hatubambikiwi gharama na rushwa. Aluta continua!
 
Back
Top Bottom