Ewe mwanaume, hupendwi kama unavyodhani

Jack Daniel

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
4,975
Reaction score
19,843
Salaam jamiiforum.

Muangalie huyo mkeo,muangalie vizuri kabisa halafu tafakari,kisha tingisha kichwa kukubali kuwa yupo na wewe.😂

Kuna namna yupo na wewe Kwa mambo mawili tu,

👉Alikosa pakwenda.

Yaani alikuwa na machaguo yake muhimu na anayoyapenda lakini hayo machaguo hayakuwa tayari Kwa mapenzi na mahusiano ya kudumu ikawa hakuna namna zaidi ya mkeo kuwa na wewe uliye tayari.

👉Alihitaji msingi na maisha mazuri.

Siyo Siri ukijituma sana ni rahisi kuweka ndani mwanamke ambaye si saizi yako,ila tu kwakuwa Una uwezo wa moja Kwa moja kutoa huduma zote muhimu.

Lakini je upendo uko wapi?
masilahi ya mapenzi yako wapi?

Kama unapendwa kwasababu ya kitu,vipi hicho kitu siku kikikosekana?

Kama unapendwa kwasababu hana chaguo,vipi siku akipata mtu sahihi?

Sikia ewe mwanaume,

Mapenzi ni hisia,yaani kuna siku unaweza kukaa na mkeo sebuleni,wewe uko busy na mambo yako lakini yeye Yuko busy kukutazama,akitafakari kipi kilimvutia kutoka kwenye mwili wako kama ni ndevu, garden love,na uhandsome wako mithili ya jogoo,na hapa ndipo hamasa na vichocheo vya mwili huja.,unakuta mkeo anatamani mfanye tendo la ndoa mara Kwa mara haijalishi amechoka,ila kwakuwa yupo emotional na wewe wala atajiburudisha Kwa kadri atakavyo.

Yaani hata wewe mwanaume unaweza kuchelewa kulala ukaamua kukaa kitandani ukimuangalia mkeo Uzuri na urembo wako,kule jandoni tulifunzwa nyakati pekee za kutambua Uzuri wa mwanamke ni akifumba macho,na akitoka kuamka,yaani ile Sura akitoka usingizini..

Lakini je,tunatambua vipi na kuenjoy kupendwa,
KUPENDWA RAHA SI MWANAMKE WALA MWANAUME yaani Unakuwa huru na mwenye nuru iwe kazini na popote.

Lakini chaajabu ndoa na mahusiano mengi anayeteseka ni mwanaume,anaishi Kwa kumfurahisha mtu ili asiachwe,mbaya zaidi mademu nao wamegundua Hilo Acha watutese😂
 
Tuwe wakweli kila mtu anaingia kwenye mahusiano kwasababu, huenda umependa tabia ya mtu,upole wake,ucheshi wake au uzuri wake

Au umependa yupo smart kichwani au ana hela,au hana mambo mengi

Kwa vyovyote itakavyo kuwa, ila kuna sababu ya kupelekea uhusiano wenu uwepo

Ila

Kibaya ni mahusiano ya pesa kupitiliza,yani mtu kufanywa Atm machine!
 
Hebu mtupe hizo hela acheni visingizio😂😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…