Ewe mwanachuo jipange

Ni kweli usemayo,yatamsaidia aliyepo humu kama ataona inafaa kufungua uzi huu.
 
Mimi sina demu lakini BOOM huwa halikai yaan, hata sielewagi kwa kweli...
Hata mimi nilikua kama wewe ila nikakaa chini nikadadavua mambo nikagundua mimi ndo tatizo. Tatizo langu nililigundua ni kushindwa kuweka bajeti yangu katika usawa na uhalisia, toka nikiwa mwaka wa kwanza nilikua na bajeti nzuri sana mfano:
Total income: 2M
total expenditure: 1.1M
saving: 800k
Income after expenses: 100k

NB: bajeti nzuri kulingana na maisha yalivyo kwangu binafsi

Kusema ukweli sikuiweka katika uhalisia bajeti yangu ya mwaka mzima wa masomo nilipoteza vingi japo sijilaumu maana sijapotea (naungana na mtoa mada). Naingia mwaka wa mwisho nikiwa na hali mpya, nguvu mpya na kasi ya ajabu kuelekea uhalisia wa bajeti yangu na nimepata njia mbadala kuweza kutatua tatizo langu la kutumia “saving". Njia mbili ninazo;

1. Kuwekeza kila pesa ninayotunza moja kwa moja kila baada ya kupokea fedha ya kujikimu. A.K.A boom
NB: hapa itakua savings ya awamu mbili ya fedha ya kujikimu.

2. Kufungua akaunti nyingine ili niweke pesa za “savings" ili nikimaliza chuo niwekeze mazima.

Kutoka moyoni nakuunga mkono kama sio hoja mtoa mada ni wakati wetu sisi tuliovyuoni kujiandaa kimwili na kiakili kupambana na mazingira na uhalisia.

" We must have a backbone not a wishbone"
 
Asante sana aiseee,umenipa kitu fulani hapa.
 
Waambie mkuu maisha huku sivyo kama wazaniavyo usipokua makini utamaliza chuo na pc tu ambayo itabidi uiuze pindi ukimliza chuo ili upate hela ya kuzungukia maofisi mbalimbali kutafuta ajira

Hahahaha mkuu umenikumbusha mbali, mi hapa nilimalza nikajikuta nina flash tu miaka hyo hata pc sina hahaha
 
Kuna wenzako hata huo mkopo hawana.
 
Kazi iliyo baki mtahani ni moja tu .kubet kwahiyo waambie wajipange maana uku kanji ana masiala kabisa ata mia tano anachukua ukiingia kwenye mabanda ya kupetia usishangae unakutana na dada yako pamoja na mjomba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…