Ewe Mtanzania, tayari umeshasahau?

Ewe Mtanzania, tayari umeshasahau?

activisty

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
315
Reaction score
107
Nianze kwa kukuuliza ewe Mtanzania mwenzangu umeshasau? Hauna kumbukumbu au umelewa kifikra? Tegeta Escrow, Katiba Pendekezwa, Mauaji ya Albino, Utekwaji wa Katibu wa JKT, ongezeko la ajabu la Deni la Taifa, Raia kuuwawa na Polisi, Pesa zilizoko Uswizi, na kikubwa zaidi umasikini mkubwa wa Watanzania wengi. Sasa nauliza yote umeshayasahau? Haukumbuki hata kidogo?

Kila sehemu nikipita nasikia habari ya CHADEMA, CCM imepanda, CUF sijui imefanya nini ooh, habari ya Zitto Kabwe, na sisikii tena watu wakikemea Mauaji ya Albino, watu wakijiuliza kwa nini ajali zinaliandama taifa, huku tukishuhudia kila siku tukipoteza nguvu kazi ya taifa ambapo wengi ni vijana.T

umeshasahau Taifa linakabiliwa na janga kubwa la rushwa na ufisadi usio na mfano, deni la taifa ni kubwa kupita maelezo, mbele yetu kuna mchakato wa Kura ya Maoni ya Katiba Pendekezwa, lakina watanzania tumelewa siasa chafu za udaku, badala ya kuongelea masuala muhimu ya kitaifa, kwa kujiuliza tutaendelea kuwa masikini hadi lini, huku wanasiasa hawa hawa wanaofanya siasa udaku, wakitujaza fikra levi, huku wao wakisonga mbele kimaendeleo pamoja na familia zao na kutuacha mamilioni ya Watanzania masikini wakubwa.

Sasa najiuliza je ni kweli tumesahau au tumelala usingizi? Ewe Mtanzania mwenzangu ebu jiulize wewe na muulize jirani yako, juu ya kila jambo ulifanyalo au kulisema lina faida gani kwako na kwa taifa? Je, kweli CCM, CHADEM, CUF, NCCR, ACT ni muhimu kuliko taifa hili? Ni Muhimu kuliko familia yako ambayo inapata mlo mmoja kwa siku?

Je, kweli unashindwa kutenga muda wa kufanya masuala muhimu ya kimaendeleo, na kuziacha fikra zako zitawaliwe na siasa udaku?

Tuamke, tufanye mambo ya msingi kwa taifa hili na tuache kulewa siasa udaku za wanasiasa dhaifu.
 
Acha ubwege ww tunaangalia current ishu hzo unazosema ww n developing stories
 
Usituzingue. Watu tuna milioni 10 zetu za mboga unatuambia nn
 
toa bassi mwongozo, tufanye nini??
 
Taifa linaongozwa na nani? Mwanasiasa anaongoza nchi basi acha tujadili siasa,au ulitaka tukimbilie nyumba za ibada?
 
Hii ni zaidi ya hatari kwani hata walioichangia hoja hii wanajidhihirisha na kujitanabaisha uhusiano walionao na wala nchi. Soma maoni yao yatakuongoza.
Ukiyafuatilia matukio ya maafa yanayotokea nchi hii, mengi ni man made! Rejea kuzama kwa meli na kuanguka kwa treni ilikuwa ni nyakati za uchaguzi. Hata pesa zinazokwapuliwa nyingi hutumika kuwahonga wapiga kura. Tumejisahau au tumekata tamaa na kuiacha nchi iwe chini ya kikundi cha mafisadi wanaokaa na kuibua scandle na kutengeneza ajali ili kutuyumbisha kiakili. Wamegeuza mbongo zetu ziende kama pendilum. Dawa yao ni kutokuwapa kura zetu tena.
 
watanzania tuna akili za kuku. tulishasahau yaliyopita tunaganga yajayo.
 
watanzania sis ni watu wa kusahau mapema mno ndio maana kuna viongoz walikumbwa na ufisad miaka ya nyuma na ilitumika gharama kubwa sana kufanya uchunguz wa ufisad wao wakabainika but leo hao hao ndo wanagombea ubunge na wanakubalika majimbon mwao, wengine urais but tunawapenda na tunaimani kwamba walisingiziwa na tunawafuata tukiomba watuongozee nchi yetu tukiamin yaliyopita si ndwele tugange yanayokuja
 
Mleta mada nakupongeza sana,mimi upenda mtu anayeusisha matukio ya nyuma ili kujenga hoja hoja ya mbele na kuleta maendeleo au muafaka.
Tukiangalia matukio ya nyuma hasa ufisadi,uongo,uroho wa madaraka,usaliti na mauaji ya viongozi wetu na watu waliokuwa na malengo ya kuliletea taifa letu maendeleo,ndo tunapaswa kujifunza kuanzia hapo ili twende mbele,matukio uliyoyatajatukiongezea na ujinga na maradhi ndo tuna pata neno TANZANIA NCHI MASIKINI,kumbe sio kweli na haliakisi utajiri malighafi tulizonazo nchini mwetu.
Viongozi hawahawa ndo wanatuletea vitu vya kuharibu vijana wetu taifa lakesho wasiweze kuwa na uwezo wa kufikiri na kuamka,wanaingiza madawa ya kulevya,mirungi na viroba vijana wanashnda wamelewa ata ukileta mada ya ukombozi watakupinga kama walivyopinga hoja yako.
 
Mleta maada uko saw a ila kumbuka yote hayo yanaletwa na uongoz mbovu Wa ccm so nivigumu kuacha kui dis kas siasa sababu ndo kila kitu.kuhusu watanzania kusahau ishu mapema nipamoja nauongoz mbovu mfano skendo inatokea tena ya laivu watu same vuja hela zetu afu serikali kmya we we at a ukpga kelele kaz bile.nivzuri hawa jamaa tuendelee kuwa diskas ili kuleta mapinduz kukaa kmya hakuwez kumuondoa ccm madarakan umenisoma.
 
Taifa linaongozwa na nani? Mwanasiasa anaongoza nchi basi acha tujadili siasa,au ulitaka tukimbilie nyumba za ibada?

Tofautisha kati ya siasa na siasa udaku. Ukiweza kutofautisha ukija hapa utarudi na point ya msingi.lakini ukishindwa basi utaendelea kujadili udaku huku ukiamini ni siasa
 
Mleta maada uko saw a ila kumbuka yote hayo yanaletwa na uongoz mbovu Wa ccm so nivigumu kuacha kui dis kas siasa sababu ndo kila kitu.kuhusu watanzania kusahau ishu mapema nipamoja nauongoz mbovu mfano skendo inatokea tena ya laivu watu same vuja hela zetu afu serikali kmya we we at a ukpga kelele kaz bile.nivzuri hawa jamaa tuendelee kuwa diskas ili kuleta mapinduz kukaa kmya hakuwez kumuondoa ccm madarakan umenisoma.

Upo sahihi.nimekusoma mkuu
 
sawa kifanyike nini sasa useme ata upige kura vip ccm hao hao wana weza kua hapo hapo walipo tuombe mungu sana masanduku ya kura yalete majibu mazuri lenye mwanzo halikosi mwisho ccm ipo siku tu manake dah. so hard
 
ili maendeleo yapatikane lazima tuanze na mabadiliko katika siasa za nchi na tuwe uchumi safi... for over 50 years t shillings inazidi kushuuka thamani.

NAUZA KURA YANGU.
 
Back
Top Bottom