Ewe mtanzania mjinga fungua macho uone

Ewe mtanzania mjinga fungua macho uone

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2012
Posts
601
Reaction score
2,508
Fumbeni macho yenu na usingizi uwapitie. mbongo zenu zitulie ili kesho mfikiria ujinga mwengine zaidi, enyi watanzania weusi, alama halisi ya mwafrika wa kughushi aliyeharibiwa akili na ukoloni, hata naye awe mkoloni kwa wenzake.

Ambao, mkipewa mbegu mtazipika na kuzila kwa uroho, halafu mkaombe tena. Kwakuwa matumbo yanataka zaidi huku mbongo zenu zinataka kidogo.

Usingizi uwapitie, ili angalau sasa, huko ambako jua linachomoza, viumbe wateule waendelee kujidhihirishia uteule wao.
Usingizi uwapitie; Enyi wenye maradhi, masikini na wajinga!
Na msidhani kama mtaamka mkiwa tofauti, Bado sana.

Mtabaki watumwa wa watu wa Ulaya Asia na Amerika. Hata watoto wenu na watoto wa watoto wao wataendelea kuwa vijakazi wa watu wengine, wateule.

Kwa kuwa nimeshindwa kujitaabisha kwa faida yenu wenyewe, mtataabika kwa faida ya wengine.

Usingizi uwapitie, ili dunia sasa ipumzike baada ya kuvumilia ujinga wenu mchana kutwa.

Kesho! Tunatarajia kusikia ujinga mwingine zaidi.

Ex Afrique Semper, Aliqui Novi
 
Mshikamano wa kizalendo siyo katika mfanano wa rangi ya ngozi, bali katika matendo ya kiutu na heshima kwa haki za binadamu. Mtanzania alishasema BINADAMU WOTE NI NDUGU ZANGU!. Haijalishi mtu awe wa njano, mweupe au hata wa kijani, kama anaheshimu utu huyo ni rafiki wa kweli!
 
Je mkuu huu utawala wa awamu ya tano una hizo sifa ulizoziainisha?
 
Kwanza ungemuubilia mungu mtu ili ayasikie ameshikwa akili na nchi jilani wamemfanya kama roboti wanampeleka anavyo taka
 
Lakini takwimu rasmi zinasema kuwa katika katika kipindi cha miaka miwili kumekuwepo na ongezeko kubwa la wajinga, rate imepanda kwa kasi kubwa sana!
Hao wajinga wanalishwa na mama yako? utamwitaje mtu mjinga anayejitafutia chakula chake na kujilisha wenyewe? Iwe kwa mujibu wa takwimu koko au wewe
 
Hao wajinga wanalishwa na mama yako? utamwitaje mtu mjinga anayejitafutia chakula chake na kujilisha wenyewe? Iwe kwa mujibu wa takwimu koko au wewe
Kujitafutia chakula na kujilisha mwenyewe hakuondowi ujinga wako,kwani wapo wajinga wengi tu wanaojitafutia chakula na kujilisha wenyewe na bado wanaishi na ujinga wao.
 
Fumbeni macho yenu na usingizi uwapitie. mbongo zenu zitulie ili kesho mfikiria ujinga mwengine zaidi, enyi watanzania weusi, alama halisi ya mwafrika wa kughushi aliyeharibiwa akili na ukoloni, hata naye awe mkoloni kwa wenzake.

Ambao, mkipewa mbegu mtazipika na kuzila kwa uroho, halafu mkaombe tena. Kwakuwa matumbo yanataka zaidi huku mbongo zenu zinataka kidogo.

Usingizi uwapitie, ili angalau sasa, huko ambako jua linachomoza, viumbe wateule waendelee kujidhihirishia uteule wao.
Usingizi uwapitie; Enyi wenye maradhi, masikini na wajinga!
Na msidhani kama mtaamka mkiwa tofauti, Bado sana.

Mtabaki watumwa wa watu wa Ulaya Asia na Amerika. Hata watoto wenu na watoto wa watoto wao wataendelea kuwa vijakazi wa watu wengine, wateule.

Kwa kuwa nimeshindwa kujitaabisha kwa faida yenu wenyewe, mtataabika kwa faida ya wengine.

Usingizi uwapitie, ili dunia sasa ipumzike baada ya kuvumilia ujinga wenu mchana kutwa.

Kesho! Tunatarajia kusikia ujinga mwingine zaidi.

Ex Afrique Semper, Aliqui Novi
Viongozi wetu wameharibu umoja wa nchi yetu.
Eti wa kimara mbomolee na wa mwanza muache.
Na hawa wa kimara walienda mahakamani kutafuta haki yao na mahakama ikaweka stop order lakini serikali hii isiyojali utu wala sheria haikujali ikabomoa.
Je huyu rais mweusi ni mweusi kweli au kibaraka wa kuharibu Tz. Je tuwakimbilie wazungu?
 
Upo sahihi mkuu, inabidi tuendelee kulala usingizi mkubwa kabisa na kujipendekeza kwa hao weupe, tulijitanabaisha na kujipa matumaini kwa 100% kuwa tutajiendesha kwa bajeti yetu wenyewe, hatutakopa Bali tutawakopesha wao, tuna kila kitu tunaweza kujitegemea.

Lakin hatimae deni la taifa linazid kukua mtoa mada tumuulize tunaposema tuna uwezo wa kuwakopesha na tuna uwezo wa kujitegemea sasa hilo deni la taifa linaongezeka vip??

Wacha tuendelee kufumba macho yetu na usingizi utupitie mkuu tukistuka tukute wanakuja na makapu kuomba msaada kwetu kama tulivyojitanabaisha na kujigamba kuwa tuna uwezo kuliko wao.
 
ambao mkipewa mbegu mtazipika na kuzila kwa uroho "halafu mkaombe tena. wakati matumbo yenu yanataka zaidi na mbongo zenu zinataka kidogo" ,.......(asante sana mkuu)
 
Back
Top Bottom