Evelyn!!! Siku saba ngumu zaidi nilizowahi kuzipitia maishani

Ila ulifanya vibaya sana! Wewe demu mara ya kwanza alikua anaishi maisha yake na hakutaka kuondoka kwenda kupanga sehem nyingine.Ukamshawishi hadi kwenda kumpangia bado ukamnyanyasa ukamtolea na vitu nje..Huu ni unyanyasaji
Yaa ii aiko poa, mi nkikosana na manzi silipizi kwenye vitu, akichepuka nachepuka afu maisha yanaendelea, visasi vya nini
 
Yaa ii aiko poa, mi nkikosana na manzi silipizi kwenye vitu, akichepuka nachepuka afu maisha yanaendelea, visasi vya nini
nilimkuta dem ndani amejitosheleza, so pale nilipomuhamishia, nilikuwa nina phase out na kuweka vyangu. Sasa mzee ulitaka tugawane? Au nimuachie?

ingawa, sikufanya sahihi kweli kumtolea vitu nje.
 
MAHUSIANO KUANZA.

Asubuhi ya siku hiyo nilimpigia simu kwa lengo la kusalimiana na nijue response yake itakuwaje. Kwa kweli alipokea simu fasta. Na kuniambia yuko salama. Nikamuuliza ratiba yake siku hiyo kama tunaweza onana. Akasema asubuhi hiyo ni kuwa anaenda Halmashauri kuonana na afisa utumishi kwa ajilo ya kushughulikia mikopo ya walimu fulani. Nilijifunza kuwa walimu wanakopa sana, si kwa sababu wanapenda, bali ni nature ya kazi yao, haina dili za hapa na pale kama kada zingine kama watu wa sheria au maliasili n.k. Basi tukakubaliana mchana tuonane pale pale bar.

Kwa kweli, penzi jipya huwa ni jambo la kuwa nalo makini wakati mwingine. Unaweza ukajikuta unafanya mambo kama mtoto. Usijari muda na kuzingatia misingi ya kazi. Hili nililistukia kichwani siku chache tu za mwanzo. Maana, nilimpa mtu anishikie gari kwa muda wa kama siku tatu. Nilikuwa natumia muda mwingi na Evelyn kila inapopatikana nafasi. Kwa muda wa siku tatu hizo, tulikuwa tukila pamoja. Jioni misele ya hapa na pale. Tulijenga ukaribu kwa kasi sana.

Nilimfahamu kwa kiasi fulani kitabia ndani ya muda huo. Kwanza alikuwa ni muongeaji sana kuliko mimi. Hakua mnywaji sana wa pombe kama mimi. Lakini pia yapo mambo yalikuwa yananipa ukakasi, mfano kutengeneza ukaribu na wanafamilia yake alikuwa akikwepa sana. Mfano kuna dada yake alikuwa pale kahama, hakutaka kabisa tufahamiane. Basi nikajua labda sababu ni mapema sana, nipunguze mzuka na mimi.

Baadae nilirejea kwenye gari na kuendelea na kazi. Sasa siku moja asubuhi alinipigia simu kuwa anataka kwenda Kwao mwanza kuna dharura.

Muda ananipigia mimi nilikuwa niko Hungumalwa. Nikamuambia panda gari ashukie pale Hungumalwa, jioni tuendelee na safari wote, maana niko hapo kuna mtu nina shida naye. Nikamuunganisha na mtu wa bus stand pale, akampa Tiketi. Mida ya saa akawa amefika.

Sasa muda huo nikampokea, nikampeleka kuna motel moja inaitwa Ndilima, lengo ale then nikimaliza issue zangu tusepe. Hapo ilitokea drama moja, ambayo mbeleni huko itakuwa na maana sana kwenye kisa hiki. Alikaa mida ya kama saa moja, akaanza simu mbona huji na vimaneno vya hapa na pale kulalamika kwenye message. Nikamwambia kuna mtu niko naye, nikimaliza nakuja na nitakuelezea.

Kufika hadi saa 12, sijarudi. Badi kuna sista pale muhudumu ni mshikaji wangu sana ndio nilimkabidhi. Anaitwa Jac. Watu wa safari, huwa na ufahamiano na watu kama hawa maeneo mengi.

Akanipigia:

"Bro wangu huyu dem wako yuko resi anataka kuondoka halafu kuna mtu anamipigia sana simu inaonyesha ndio anamuwahisha".

Nikamueleza hali halisi. Baada ya kama dakika 10, jac akanipigia tena kuwa dem wako amelipa bill anaondoka. Mh, nikaona hii kimeo.

Basi, ikabidi nitoke nilipokuwa nikafika nikakuta ametoka na mabegi yake pale barabarani anasubiri gani. Nikajieleza na kumplease hanielewi. Sasa akanituhumu kuwa nina lengo la kumchelewesha makusudi ili alale nipige.

Basi nikasema isiwe kesi. Ghafla akapigiwa simu, haikuwa na loudspeaker ila sauti inasikika. Sauti ya kiume, inamuuliza hujaondola tu.

"Nilipata emergency, napata gari niondoke hapa Mwigumbi". Ikajibiwa sawa na ikakatwa.

Sikumuuliza kitu, akawahi maelezo kuwa huyu ni kaka yangu. Kuna kikao cha muhimu cha familia leo jioni. Nikamjibu sawa.

Kuna kiprivate kikafika, nikamlipia nauli na kumrudishia ef 10 yake aliyolipia chakula, akasepa. Ila nikawaza sana huyo ni bro wake kweli? Kwanini aseme yuko mwigumbi wakati ni hungumalwa? "Labda alikosea"..niliwaza na kuhitimisha hivyo.
Ni kosa sana kupuuzia red flags
 
nilimkuta dem ndani amejitosheleza, so pale nilipomuhamishia, nilikuwa nina phase out na kuweka vyangu. Sasa mzee ulitaka tugawane? Au nimuachie?

ingawa, sikufanya sahihi kweli kumtolea vitu nje.
Ukitaka amani ya moyo.

Jitahidi sana umuombe radhi Evelyn kwa kitendo cha kumtolea vyombo nje kama mbwa.

Utu wa mtu una thamani kuliko wivu wetu.
Natamani ufike wakati mapenzi yaishe kama vile mteja ambaye mmeshindwana bei au terms za bishara tu
 
1
Ukitaka amani ya moyo.

Jitahidi sana umuombe radhi Evelyn kwa kitendo cha kumtolea vyombo nje kama mbwa.

Utu wa mtu una thamani kuliko wivu wetu.
Natamani ufike wakati mapenzi yaishe kama vile mteja ambaye mmeshindwana bei au terms za bishara tu
Kabisa mkuu jamaa hakufanya poa kabisa aisee.
Binafsi sipendi kudhalilishana mkishaachana.
 
1

Kabisa mkuu jamaa hakufanya poa kabisa aisee.
Binafsi sipendi kudhalilishana mkishaachana.
Mimi kuna binti alinitenda, kweli nilipoteza hisia naye 100% hadi leo, but sikuwahi hata kumsemesha vibaya hadi leo hata akipiga nitapokea but simpi nafasi tena hata ya kuonana.

Mapenzi ni mkataba huru, Kei ni yake.

Mkataba wetu utakua hai tu endapo kila mmoja atakuwa mwaminifu kwa mwenzie pande zote.

Ukienda kinyume mnavunja mkataba kwa amani tu
 
Ukitaka amani ya moyo.

Jitahidi sana umuombe radhi Evelyn kwa kitendo cha kumtolea vyombo nje kama mbwa.

Utu wa mtu una thamani kuliko wivu wetu.
Nikuhakikishie bro, Mwaka jana tulipoonana baada ya muda ya kupita katika 'pillow talks', nilimuomba radhi. And trust me, mawasiliano ya hapa na pale yapo, friendly kabisa. Mimi si mtu wa kuweka vitu moyoni.
 
Nikuhakikishie bro, Mwaka jana tulipoonana baada ya muda ya kupita katika 'pillow talks', nilimuomba radhi. And trust me, mawasiliano ya hapa na pale yapo, friendly kabisa. Mimi si mtu wa kuweka vitu moyoni.
Umenitia moyo.

Je hawajaachana na mlevi wake?
Ninaamini kwasasa ukimchukua atakuwa mtumwa wako kwa funzo ulilompa
 
Makonda wanapenda vibaya acheni tuuu,Kuna konda rout ya mbagala-gombs alinielewaga,nilimtesa yule mkaka, Mungu anisamehe tu,watu wanahonga wale balaa,ilifika mahala ikabidi nimblock tu maana akizidisha usumbufu aseee,cm hadi saa kumi na moja alfajiri umelala na ba chanja
Kwanini hukutaka kumuelewa konda wa watu dada
 
Kuna yule dogo ulimkabidhi gari wakati mnaenda msibani Kwa ndugu wa Everlyin akakwambia "broo ukitulia unitafute tuongee" Vp mkuu ulimtafuta ?
@Wildlifer natamani kupata jibu hili pia
 
Halloo hawa viumbe wamenipa elimu kubwa sana.
Ukizama sana kabla yeye hajazama utateswa hadi uvae nguo kichwani
Na wao wanatusema hivyo hivyo, kuwa wakizama wao kwanza, tutawatesa, sasa sijui nani aanze kuzama.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom