Wana Bodi salamuni.
Naomba kuwasilisha kuwa, Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama mkoa wa Mwanza,
Mhandisi Evarist Ndikilo, yuko katika wakati mgumu kutokana na yeye
kushiriki kikao cha usuluhishi ambacho badala ya kuamua mambo kwa
kuzingatia sheria za nchi, alitumia ukuu wake wa mkoa kuamua jambo
lililokuwa mbele yake.
Jijini Mwanza, kumefukuta mgogoro wa kidini kati ya WAISLAM na WAKRISTO.
Mggogoro huo ulianzia pande za IGOMBE-KAYENZE, ambako mchungaji mmjoa
wa kanisa la kipentecoste alichinja ng'ombe kwa ajili ya kitoweo kwa
watu waliofika kuhani msiba. Kwa kuwa msiba ni suala la kijamii,
linawajumuisha WAKRISTO, WAISLAMU na dini nyingine, waislam walisusia
chakula kile kwa kudai kuwa aliyechinja hakua muislam. Na wakapitisha
maazimio kuwa, wao watakuwa wanashiriki misiba tu lakini vyakula vya
msibani hawatakula kwa kuwa vinaandaliwa na makafiri.
Mchungaji yule alipata misukosuko lakini kwa kuwa hakuna sheria ya
kumshitaki, aliachiwa huru huku kukiwa na bifu kati ya waumini wa dini
hizi mbili.
Ndipo migogoro mingine imeibuka, na katika juhudi za kuitatua, Mkuu wa
Mkoa alijikuta akisahau kutumia katiba ya nchi na sheria zake kwa
kutamka mbele ya hadhara iliyokuwepo, kuwa WAISLAM ndio wenye jukum la
kuchinja. Tamko hili liliwatifua na sasa wanahamasihsana waweke watu wao
kule machinjioni na wafungue bucha waandike kabisa bucha ya
mkristo.