EU kuzipa asasi mamilioni ya miradi ya mazingira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

EU kuzipa asasi mamilioni ya miradi ya mazingira

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Nov 23, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280


  [​IMG]
  Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU)nchini, Tim Clarke


  Umoja wa Ulaya (EU) kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha, umezindua mchakato kwa Taasisi na Asasi zisizo za Kiserikali kutuma maombi ya mchanganuo kwa ajili ya kupata msaada wa kugharamia miradi ya mazingira utakao gharimu kiasi zaidi ya Sh. bilioni mbili za Kitanzania.
  Akizindua mchakato huo, Balozi wa Umoja huo nchini, Tim Clarke, alisema anafuraha kubwa kuzindua mchakato huo na EU imekua

  ikisaidia utunzaji wa maliasili na wanyama ,kwa miongo kadhaa nchini Tanzania, na mradi huo mpya una lengo la kuisaidia jamii nchini kulinda na kuhifadhi mazingira.


  Afisa Muidhinishaji wa Mfuko wa Maendeleo wa Ulaya (EDF), Samuel Marwa, alisema Tanzania na EU zina ushirikiano wa muda mrefu na umoja huo umetoa fedha hizo kwa ajili ya miradi ya kutunza mazingira.


  Marwa aliongeza kuwa mchakato huo utahusu wale ambao tayari wana miradi ya kutunza mazingira hasa katika utunzaji wa misitu, wanyama na masuala ya uvuvi.

  Msaada huo utawezesha jamii ya Watanzania kutunza maliasili ambayo inatishiwa na ongezeko la watu, matumizi mabaya ya ardhi na uchimbaji wa madini.
  Mchakato wa kuwapata washindi unatarajiwa kuchukua miezi miwili na mwisho wa kupokea maombi ni Januari 31, 2012.  CHANZO: NIPASHE


   
Loading...