EU:Hatutoruhusu Marekani iingilie uhusiano wetu na Iran

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
11,180
Reaction score
24,564
Mogherini: EU haitairuhusu Marekani iingilie uhusiano wake na Iran
Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesema Marekani haiwezi na haipaswi kuitwisha EU sera zake na kwamba umoja huo wenye nchi wanachama 28 hautairuhusu Washington iufanyie maamuzi juu ya uhusiano wake wa kibiashara na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Tovuti ya Livemint imemnukuu Federica Mogherini akisema hayo katika mahojiano na gazeti la Arab News la Saudi Arabia yaliyochapishwa Jumanne na kuongeza kuwa, EU imejitolea kwa dhati kuendelea kufungamana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, licha ya Marekani kujiondoa kwenye mapatano hayo ya kimataifa.
Amesema, "Tunafanya kazi kwa pamoja kama umoja wa nchi 28 na kwa ushirikiano wa jamii ya kimataifa ili kuyanusuru makubaliano ya nyuklia ambayo hadi sasa yametekelezwa kikamilifu na kuidhinishwa mara 13 katika ripoti ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki. Sehemu ya ushirikiano huu ni kuhakikisha kuwa mashirika ambayo yanataka kufanya biashara halali na Iran yanaruhusiwa na kupewa dhamana. Hili ndilo jambo ambalo tunalishughulikia kwa sasa."
Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya amekariri kuwa, anatumai kuwa mfumo maalumu kwa ajili ya mabadilishano ya fedha kati ya Iran na Ulaya kwa kifupi SPV utazinduliwa hivi karibuni.
Amesisitiza kuwa, EU haitaruhusu uingiliaji wa madola ajinabi hata yawe ni waitifaki wa karibu wa umoja huo, kuvuruga biashara halali kati yake na Iran.
Itakumbukwa kuwa tarehe 8 Mei mwaka uliomalizika, Rais wa Marekani, Donald Trump aliitoa nchi yake katika mapatano hayo ya JCPOA na kutangaza kuirejeshea Iran vikwazo vyote vilivyoondolewa baada ya kufikiwa mapatano hayo.
 
Umoja wa Ulaya Kwa Miaka mingi umekuwa Kama Mkia kufuata fuata sera Za nje Za America Matokeo yake imeathirika mbaya

Trump alishajitoa kwny Mkataba wa Kinnyuklia Na Iran lakin Kila Siku Bado anafuatilia Iran kujua Kama anatimiza Masharti ya Mkataba ule Au laa
 
Bora sisi tuna magobore!!!! Nyuklia ya nn kisiwa cha amani?

sent from this unknown device
 
Kuna vitu vingine matekani kasababisha mwenyewe watu kuanza kuwa na kiburi, hivi kweli ufaransa anaweza kumsikiliz marekani wakati airbus imepewa kandarasi ya kuwauzia mashirika ya Irani ndege zaidi ya 100? Kosa kulinda maslahi ya marekani ambayo wao hawanufaiki nayo, wakati marekani anaiwekea vikwazo urusi, ufaransa alikuwa na kandarasi ya kuwauzia manowari za kivita mbili na zilikuwa hatua ya mwisho ati kisa tu ugomvi wa marwkani na urusi ile kandarasi ilisitishwa, sidhani kama wanataka kuendelea na ujinga huo, ulaya wamejifunza juzi tu hapa kwenye ishu ya saudi arabia na mkasa wa Jamal kashogi ambapo shinikizo lilitolewa hata na bunge la marekani pamoja na ulaya kuwa saudi arabia wawekewe vikwazo, serikali ya matekani ikasema inamaslahi mapana na Daudi arabia haiwezi kuwawekea vikwazo, hapo yawezekana walijisemea kimoyo moyo ahaaaa kumbe sisi marekani huwa hajali maslahi yetu...
 
Kumbe adi urus nayeye uwa ananua manoar nchi nyingine da hii kali!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikipata muda nitakufahamisha sababu za kutaka kununua hiyo meli ya kubebea helkopta za kivita toka Ufaransa.ni sababu rasmi kutoka msemaji toka Wizara ya Ulinzi ya Urusi.Wala sio kwamba hawawezi kutengeneza.
 
Mogherini: EU haitairuhusu Marekani iingilie uhusiano wake na Iran
Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesema Marekani haiwezi na haipaswi kuitwisha EU sera zake na kwamba umoja huo wenye nchi wanachama 28 hautairuhusu Washington iufanyie maamuzi juu ya uhusiano wake wa kibiashara na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Tovuti ya Livemint imemnukuu Federica Mogherini akisema hayo katika mahojiano na gazeti la Arab News la Saudi Arabia yaliyochapishwa Jumanne na kuongeza kuwa, EU imejitolea kwa dhati kuendelea kufungamana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, licha ya Marekani kujiondoa kwenye mapatano hayo ya kimataifa.
Amesema, "Tunafanya kazi kwa pamoja kama umoja wa nchi 28 na kwa ushirikiano wa jamii ya kimataifa ili kuyanusuru makubaliano ya nyuklia ambayo hadi sasa yametekelezwa kikamilifu na kuidhinishwa mara 13 katika ripoti ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki. Sehemu ya ushirikiano huu ni kuhakikisha kuwa mashirika ambayo yanataka kufanya biashara halali na Iran yanaruhusiwa na kupewa dhamana. Hili ndilo jambo ambalo tunalishughulikia kwa sasa."
Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya amekariri kuwa, anatumai kuwa mfumo maalumu kwa ajili ya mabadilishano ya fedha kati ya Iran na Ulaya kwa kifupi SPV utazinduliwa hivi karibuni.
Amesisitiza kuwa, EU haitaruhusu uingiliaji wa madola ajinabi hata yawe ni waitifaki wa karibu wa umoja huo, kuvuruga biashara halali kati yake na Iran.
Itakumbukwa kuwa tarehe 8 Mei mwaka uliomalizika, Rais wa Marekani, Donald Trump aliitoa nchi yake katika mapatano hayo ya JCPOA na kutangaza kuirejeshea Iran vikwazo vyote vilivyoondolewa baada ya kufikiwa mapatano hayo.
hizo zote ni hasira za kibiashara,baada ya trump kuwapandishia kodi,bidhaa zao zinazoingia marekani inawauma sana,mbona miaka yote mlikuwa kimbelembele kumuunga mkono kwa kila jambo,mwanaume ni russia tu,yeye ni jeshi la mtu mmoja......
 
Kuna vitu vingine matekani kasababisha mwenyewe watu kuanza kuwa na kiburi, hivi kweli ufaransa anaweza kumsikiliz marekani wakati airbus imepewa kandarasi ya kuwauzia mashirika ya Irani ndege zaidi ya 100? Kosa kulinda maslahi ya marekani ambayo wao hawanufaiki nayo, wakati marekani anaiwekea vikwazo urusi, ufaransa alikuwa na kandarasi ya kuwauzia manowari za kivita mbili na zilikuwa hatua ya mwisho ati kisa tu ugomvi wa marwkani na urusi ile kandarasi ilisitishwa, sidhani kama wanataka kuendelea na ujinga huo, ulaya wamejifunza juzi tu hapa kwenye ishu ya saudi arabia na mkasa wa Jamal kashogi ambapo shinikizo lilitolewa hata na bunge la marekani pamoja na ulaya kuwa saudi arabia wawekewe vikwazo, serikali ya matekani ikasema inamaslahi mapana na Daudi arabia haiwezi kuwawekea vikwazo, hapo yawezekana walijisemea kimoyo moyo ahaaaa kumbe sisi marekani huwa hajali maslahi yetu...
uko sawa kabisa,alafu kawapandishia EU kodi bidhaa zao zinazoingia USA,hii imewauma sana...
 
Kumbe adi urus nayeye uwa ananua manoar nchi nyingine da hii kali!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna nchi inayoweza kila kitu haoa duniani, pia ni njia ya kuhamisha technolojia kutoka kwa aliyekuzidi kuja kwako, mfano wewe unaweza kuwa unafuga kuku anataga mayia 20 kwa mwezi lakini ukaona jirani yako kuku zake zinataka mayai 100 kwa vyovyote vile utaenda kununua mbegu ya huyo kuku na kumleta kwako
 
Na hii kitu siyo kwamba uwa anapenda ila huwa analazimika tu maana yeye njini zake huwa hazifanyi vizuri.
Sio kweli. Hawajatengeneza hizo "Rocket Engines", wanatarajia kuanza kizitengeneza 2022 na kuachana na za Russia. Jaribu kusoma vema between the lines ndio utajua.
 
Back
Top Bottom