eTurboNews: Tanzania not a place to invest in Africa...

TIC yainadi Tanzania mbele ya nchi 160
Kongamano la Kimataifa la Uwekezaji (World Investment Forum) limefunguliwa tarehe 22 Oktoba 2018 Geneva, Uswisi na Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD) Dkt. Mukisa Khitui na litaendelea mpaka October 26,2018.
Kauli mbiu ya kongamnao ni ‘Uwekezaji kwa maendeleo endelevu’ (investing for sustainable development) ambapo majadiliano yatajikita kwenye changamoto za uwekezaji katika mazingira mapya ya utandawazi na mapinduzi ya viwanda (Globalization and Industrialization)
Balozi Dkt. James Msekela (wa tatu kutoka kulia) na Mkuregenzi wa TIC Bw. Geoffrey Mwambe (wa ili kutoka kulia) wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa uwekezaji Geneva,Uswisi.
Kongamano hilo la aina yake huandaliwa kila baada ya miaka miwili na UNCTAD kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa masuala ya Uwekezaji. Takribani washiriki zaidi ya 5,000 wanashiriki kutoka nchi 160 duniani ikiwemo Tanzania na ujumbe wake unaongozwa na Balozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa Geneva, Dkt. James Alex Msekela.
Washiriki wa kongamnao hilo ni kutoka katika nyanja mbalimbali za umma na sekta binafsi ikiwamo Wakuu wa nchi, Mawaziri Wakuu, Mawaziri, Makatibu Wakuu na Wakuu wa Taasisi za Uwekezaji. Wengine ni Watendaji wa Makampuni ya Kimataifa na Ushirikiano wa Hisa, Wasimamizi wa Mifuko ya Fedha, Wakurugenzi Wakuu wa Mashirika ya Sekta Binafsi, Wataalam wa eneo la Uwekezaji wa Kimataifa,Wabunge,Wawakilishi wa Vyama vya Kiraia, Wasomi Maarufu, na vyombo vya Habari vya Kimataifa

Mkurugenzi TIC Mwambe kuinadi Tanzania mbele ya nchi 160 – Millardayo.com
TIC wanafanya kazi kubwa sana kwa maendeleo ya Taifa letu lakini kuna watu wachache wanawadharau na hii ni mbaya sana ila najua Rais wangu mpendwa JPM anafahamu mchango wa TIC
 
Tanzania itajengwa na watanzania wenyewe,, lakini tunawahitaji wawekezaji zaidi ili nchi iweze kupiga hatua kimaendeleo.....
 
Wako wengi tu lakin investors wachache niwataje. Warren buffet, george soros, raymond dalio, thomas petterfy,steven cohen , ronald perelman, jeff bezoz, bilgates.

Hawa.ndio investors top pale america. Thats why serikal ya america inawalinda, ukiwagusa hawa uchum wa america unatikisika.
Nijibuni swali moja tu kwamba ni mwekezaji yupi aliyeineemesha Marekani?
 
Viwanda 200 vyasajiliwa mwaka mmoja

KATIKA kutekeleza azma ya Tanzania ya viwanda, serikali imesajili viwanda zaidi ya 200 ndani ya mwaka mmoja wa serikali ya Awamu ya Tano, chini ya Rais Dk John Magufuli.
 
Unaelewa maana ya investor? Hata ccm ni investor pia ila imewekeza ujinga katika Taifa na results zake ndio majinga kama wewe.

Mo Dewji ni muwekezaji na familia ilitowa Ulmitum msipomuachia mpaka kufikia tarehe 20/10/2018 wangesimamisha production ndio mngeelewa kwa vitendo investor ni nani?

By the way serikali imeajiri Watanzania wangapi?

Mashoga wako salama Tanzania.
unahisi serikali haijaajiri?
 
Hafla ya Standard Chartered yabainisha viwanda 200 vya China kujengwa Tanzania
katika kipindi cha miaka mitatu ijayo inatarajia kuwekeza katika viwanda 200 nchini Tanzania vitakavyokuwa na uwezo wa kuajiri moja kwa moja Watanzania laki mbili.Kwa sasa uwekezaji wa China nchini Tanzania umetoa fursa za ajira za moja kwa moja 150,000 na zisizokuwa za moja kwa moja 350,000.Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mh. Charles Mwijage katika hafla ya chakula cha jioni kwa wawekezaji kutoka China.
hatuja sahau bado
 
Msimamo wangu mimi ni bora waje wawekezaji wazungu mana wanakuja na mitaji yao na kuna waafrika wanabshatika kupata mishahara mikubwa mpaka mil.50 kwa mwezi.

Nachukia huu uwekezaji wa wanasiasa hasa wa wana CCM wachache ambao wamashika viti ,walioifanya hii nchi kuwa kampuni lao wakati hawajaingia na mtaji wowote zaidi ya kofia na tisheti za kijana na kusifiana.

Wanyonyaji na mabwanyenye wa CCM wanafukuza watu waliowekeza mitaji yao wakati wao ndio wanyonyaji na makupe wakubwa wanaopora kodi toka kw a wauza vitumbua ili wajilipe kuanzia mil.7 mpaka 12 kwa mwezi bila kuwekeza au kuzalisha chochote ndani ya mwezi mzima zaidi ya kutembembelea magari mazuri,nyumba nzuri,ulinzi na madaraka makubwa kama maCEO wa nchi hii.

Kwa sasa wanapiga vita sana watu na mitaji yao eti kwa kujifanya ni wazalendo wanaolinda mawe yaliyofichwa huko ardhini na Mungu.

Hawa maCEO walijibinfshia nchi wakiulizwa mbona wao hawafanyi biashara kama wanafikiri biashara ni kuiba tu wanabaki kurukaruka kama maharage jikoni kwa sababu wanajua kuwa ni matapeli na wanapata mabilioni ya pesa bila kuwekeza chochote zaidi ya kuwajengea chuki wawekezaji wa kweli wenye mitaji yao na wananchi.

Tuwakatae kwanza wanyonyaji tunaowashangilia na kuwalipa mamilioni wakati hawajawahi kuwekeza chochote nchini na wengine hawalipi hata kodi kwenye mishahara yao.
Very well said!

God willing!
 
Hafla ya Standard Chartered yabainisha viwanda 200 vya China kujengwa Tanzania
katika kipindi cha miaka mitatu ijayo inatarajia kuwekeza katika viwanda 200 nchini Tanzania vitakavyokuwa na uwezo wa kuajiri moja kwa moja Watanzania laki mbili.Kwa sasa uwekezaji wa China nchini Tanzania umetoa fursa za ajira za moja kwa moja 150,000 na zisizokuwa za moja kwa moja 350,000.Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mh. Charles Mwijage katika hafla ya chakula cha jioni kwa wawekezaji kutoka China.
hatuja sahau bado
 
Tanzania haiwezi kuendelezwa na Investors...Tuache hadaa!

Na hili ndio jambo mhimu kuliko kila kitu ambacho viongozi wetu wanatakiwa wakizungumzie kwa ufasaha na kuweka mikakati wanayojua italiendeleza taifa hili.

Nakupa 'like'; nadhani ya pili mwaka huu kwa kuliona jambo hili, lakini hufafanui chochote cha kutusaidia sisi tunaokusoma tuelewe ni jinsi gani Tanzania itajiendeleza, na isiwe kuwategemea 'investors.'

Tunasikia kelele nyingi tu za ujenzi wa viwanda, kwa mfano. Nani anajenga viwanda hivi, sio 'investors'?
Serikali inajenga viwanda vya aina gani, kama nayo inashiriki?

Sera ipo, na mikakati ya utekelezaji tunayo? Ni nani wanayaelewa yaliyomo kwenye sera hizo na mikakati hiyo? Wafanya kazi serikalini kwenye wizara husika tu?

Rais Magufuli anawataka wawekezaji toka Israel waje wawekeze kwenye viwanda vya kutengeneza dawa. Hawa sio investors?

Serikali imefanya/inafanya nini kuhakikisha Tanzania nayo inakuwa na mkondo wake wa kuwa na uwezo wa kutengeneza dawa. Uwezo wetu sisi wenyewe bila ya kutegemea waIsrael waje kuwekeza.

Kama tumekuwa na wataalam wa upasuaji mioyo kwenye taasisi ya Kikwete tunaoweza kuwategemea kufanya kazi hiyo kwa uhakika; ni vipi tushindwe kujiwekea uwezo wetu wenyewe kwenye nyanja nyingine muhimu kama kutengeneza dawa, kuanzisha viwanda vya kutengeneza chemikali mbalimbali, ikiwemo hizo za kutengeneza dawa,n.k.

Kwa nini serikali isiweke mkazo zaidi katika kujijengea uwezo wetu sisi wenyewe katika nyanja maalum tutakazoona nchi yetu ina nafasi nzuri zaidi ya kufanikiwa?

Maswali ni mengi, lakini najua naandikiana na 'jingalao', mwenye uwezo wa majibu ya mkato bila ya ufafanuzi wowote juu ya anachokiandika!
 
Hafla ya Standard Chartered yabainisha viwanda 200 vya China kujengwa Tanzania
katika kipindi cha miaka mitatu ijayo inatarajia kuwekeza katika viwanda 200 nchini Tanzania vitakavyokuwa na uwezo wa kuajiri moja kwa moja Watanzania laki mbili.Kwa sasa uwekezaji wa China nchini Tanzania umetoa fursa za ajira za moja kwa moja 150,000 na zisizokuwa za moja kwa moja 350,000.Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mh. Charles Mwijage katika hafla ya chakula cha jioni kwa wawekezaji kutoka China.
hatuja sahau bado
Hizi habar vijana wa ufipa huwa hawapendi kuzisikia na usishangae ndio hao wameamua kuichafua nchi kwa sababu wamebanwa hatar
 
Hafla ya Standard Chartered yabainisha viwanda 200 vya China kujengwa Tanzania
katika kipindi cha miaka mitatu ijayo inatarajia kuwekeza katika viwanda 200 nchini Tanzania vitakavyokuwa na uwezo wa kuajiri moja kwa moja Watanzania laki mbili.Kwa sasa uwekezaji wa China nchini Tanzania umetoa fursa za ajira za moja kwa moja 150,000 na zisizokuwa za moja kwa moja 350,000.Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mh. Charles Mwijage katika hafla ya chakula cha jioni kwa wawekezaji kutoka China.
hatuja sahau bado

Taarifa hii ilitolewa lini? Mwijage ni "comical Ali" wa Saddam wa Iraq. Hakuna analosema likawa na ukweli wowote.
Kenya wanadai weshavuka hiyo 200 ya waChina hadi mwaka huu wa 2018.
 
Back
Top Bottom