'Kitu gani nyie?' Aliuliza rais Samia. Nadhani rais aliwakusudia Watanzania. Marais wa Afrika ni simba kwa wananchi wao, lakini ni fisi kwa Wakoloni!
Ndiyo maana niliposikia swali hilo moja kwa moja nikajua rais hamaanishi mabeberu wa dunia hii kwamba hawana umuhimu wowote.
Kama kweli anaona Tanzania iko kimo kimoja na Marekani afanye jambo moja tu linaloonesha yuko tayari kusimama macho kwa macho na Trump.
Fidhuli huyu tRump, juzi tu aliwapiga marufuku Watanzania kuingia nchini Marekani, kwa sababu za kipuuzi kabisa zinazoweza kutatuliwa kiidara. Eti wanapitisha muda wa visa zao! Hii haihitaji kabisa kuipiga marufuku nchi nzima ya watu 70 milioni.
Hii ni dharau ya wazi, Kwa kweli tRump anazidharau mno nchi za Afrika, na hawa wanaojifanya kutunisha misuli wako kimya kama maji ya mtungi.
Katika kipindi chake cha mwanzo aliziita 'shithole'- maliwato....kimyaaaa! Katika nchi 39 alizozipiga marufuku 28 ni za Afrika!
Sasa ngoja nikiuambie viongozi waliosema 'who are you' na wakamaanisha Marekani na si wananchi wao.
Ni nchi za Burkina Faso, Mali, Niger na Gabon, ambazo zimechukua hatua hizo hizo na kupiga marufuku Mmarekani yeyote, hata viongozi, kuingia nchi hizo hadi ibadilishe sheria hiyo ya kibaguzi na ya kiburi.
Katika International Relations kuna kitu kinaitwa 'reciprocity', yaani 'akutendae mtende' Sidhani kama Wanadiplomasia wetu msonge wanaijua hii!
Misri kwa mfano, ni nchi tuliokubaliana kuwa wananchi wao na wetu waingie bila visa, lakini Mbongo ukifika Cairo utafurushwa (sijui sasa, imenitokea miaka 3 iliyopita), Wala hawajali, kazi kupiga beer zao tu!
Sasa, kama mama kweli alikusudia kutunisha msuli, basi na awaambie Wamarekani komeni!
Aanze na maafisa wa Barrick wakifika Julius Nyerere tu awaambie hakuna kuingia! Thubutuuu! Watasema oooh tutakosa msaada, pesa, wawekezaji....lakini hivyo vina thamani kubwa kuliko heshima ya nchi, national dignity? (Binafsi sijaona senti moja ya hawa Barrick, kupe tuu).
Najua watasema ni wa Canada inagaje wanahisa wakuu ni Wamarekani.
Ndiyo maana naamini 'who are you' tumeulizwa sisi, maana sisi hata kura yetu haihitajii!