Eti wasanii wamesahau mchango wa Sugu Bungeni!

Eti wasanii wamesahau mchango wa Sugu Bungeni!

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,096
Nilishawahi kuuliza swali hili; Msanii anajisikiaje kutumiwa kama daraja? Watu wanakuhitaji pale mtu wanapotaka kufanikisha mambo yao. Baada ya kufanikiwa hawatakukumbuka tena.

Tatizo siyo kusahaulika, hoja hapa ni kwamba kumbe umuhimu wako unatambulika lakini unapuuzwa. Inakuwaje anayekufanya daraja anatambua nguvu yako lakini hazingatii mahitaji yako?

Asiyekutetea inakuwaje wewe umpiganie kufanikisha anachopambana kukipata? Ina maana wewe ndiye tu mtengeneza njia, mpitaji akishapita hakukumbuki tena mpaka siku akitaka tena kukugeuza lifti.

Kimsingi wasanii wetu wa Bongo wananivunja sana moyo. Tabia zao hazina tofauti na kuku anayeumwa sotoka au mdondo, yaani kuku wa kideli! Huna haja ya kumkimbiza, utamkuta amelala na utamkamata bila purukushani.

Hawajui ni kipindi gani cha kuringa wala kile cha kujitoa kwa bei rahisi. Wakipigiwa simu tu wanakimbia mbio na kutimiza mahitaji ya wakubwa. Tatizo siyo wao, ni jinsi wasivyojitambua.

Taifa linaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu. Ni kipindi kigumu mno kwa wanasiasa na zaidi kwa vyama vya siasa. Mnyukano unaendelea, wanachama wa vyama walishatoa adhabu kwa viongozi walioshindwa kutimiza matarajio yao na sasa inakwenda zamu kuu ya wananchi.

Wasanii ni tabaka kubwa kwenye jamii yoyote ile. Mshangao kichwani kwangu ni kuwa pamoja na ukubwa wao lakini ndiyo wasiojitambua, mjomba wangu anayetembelea mjini kwa mgawo ana afadhali kubwa mno. Sijui kwa nini?

Walivyo utadhani hawajui haki yao, kwa hiyo hawana ufahamu ya kile wanachokosa, hivyo hata ambacho wanakihitaji hawakifahamu. Ukiendelea kuwaita wasanii wa Bongo ni kioo cha jamii, hilo ni kosa lako mwenyewe.

Unahitaji uthibitisho wa hilo? Jinsi walivyojigawa makundi kipindi hiki ni wazi kuwa hawana umoja. Kitendo cha kugawanyika ni kilelezo kinachopima udhaifu wa ubongo wao.

Kweli ni Tanzania peke yake, wasanii fursa pekee ya kifedha ni kampeni za uchaguzi. Nyimbo na filamu zao zinauzwa mitaani kinyemela, badala ya kupambana serikali idhibiti wizi ili watajirike kwa kipato chao halali, wao wanatosheka na kampeni. Tena zaidi wanagombana!

Wajasiriamali wahuni kila siku wanafungua vistudio uchwara, wanauza nyimbo na filamu za wasanii wa Kibongo utadhani zao. Mtu ana kompyuta yake moja, inaendesha maisha yake na ajira anatoa. Mwenye kazi zake ni msanii ambaye hata hajui ni kiasi gani anapoteza kwa wizi huo.

Filamu za nje zimemwagwa kariakoo, Ubungo na Mwenge, bei ni shilingi 1,000 tu! Wala siyo biashara ya kujificha, ukipita unasikia spika zinatangaza "buku buku", badala ya kuona kama biashara hiyo ni jini linaloua soko lao, wao wanagombana wao kwa wao.

Kazi zako zinaibiwa na hujaonesha utayari wa kupambana kuzitetea lakini unaamua kugombana kwenye kampeni na wasanii wenzako pamoja na wateja wako kwa ajili ya mchuzi mbuzi wa kampeni.

ETI WAMESAHAU MCHANGO WA SUGU
Maswali mawili tu! Ni yupi amewahi kuwa mzuri kwao? Ni nani mwenye malengo bora kwao? Kama maswali hayo yangekuwa na majibu yanayofanana maana yake wasanii wasingetofautiana. Wangesimama pamoja kwa maslahi yao wote.

Miaka mitano ya Mbunge wa Mbeya Mjini anayetetea kiti chake (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu', ilikuwa na maana kubwa katika maisha ya wasanii na sanaa kwa jumla.

Kabla ya Sugu, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania halijawahi kupata msemaji mpambaji wa maslahi ya wasanii na sanaa kwa jumla.

Leo hii kuna mafanikio makubwa katika sanaa. Japo siyo kwa kiwango tunachoamini ndicho kinafaa lakini tukubali kuwa kuna afadhali kubwa.

Hivi, wasanii wamesahau juhudi za Sugu bungeni? Alivyokuwa akitoa sauti mpaka inakauka kutetea sanaa na wasanii?

Tumesahau Sugu alivyotengeza maadui kwa sababu ya kupambana na wale wanaoitwa wanyonyaji wa kazi za sanaa?

Ni kelele za Sugu ndizo zilisababisha Rais Jakaya Kikwete kufungua macho na kuamua kufanya vikao na wasanii mbalimbali, kujua nini hasa mahitaji yao na changamoto zao.

Kama msanii wa kawaida leo anaweza kutengeneza shilingi milioni mbili mpaka tano kwa mwezi, huku wengine wakivuna milioni 10, 20 na kuendelea kutokana na soko la nyimbo zao kupitia miito ya simu (Ring Back Tunes ‘RBT'), wasanii wanawezaje kushangilia hili bila kupata msemaji wa uhakika?

Kazi za kurasimisha kazi za wasanii zimekuwa na mafanikio makubwa kiasi. Angalau msanii anajua kazi yake inapita katika sura halisi ya kibiashara kwa mujibu wa sheria za nchi. Kazi za wasanii wote kabla ya kuingia kwenye mzunguko wa kibiashara zinabandikwa stempu za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Wadau waliokuwa wanawanyonya wasanii kwa kuwalipa fedha ndogo na kuingiza faida kubwa, walibadili tabia ghafla.
Nilikutana na wasanii wengi na walikiri mbele yangu kuwa maslahi yao yaliboreshwa kwenye maonesho ya muziki baada ya kelele za Sugu bungeni.

Leo hii wasanii wamemtenga Sugu, yupo ‘bize' na kampeni zake na wanataka akishinda tena, aende akawatetee kwa mara nyingine.

Hii ndiyo sababu nimesema hawajui walichokosa wala wanachohitaji. Unaweza kujiuliza ni lini Dk. John Pombe Magufuli amewahi kuwa mwema kwao? Ni siku gani ilitokea Edward Ngoyai Lowassa akawa mtu mzuri kwa wasanii?

Magufuli pamoja na kwamba ni mkali wa kupiga tumba lakini hajawahi kujipambanua kama mtu mwenye mapenzi na sanaa. Hajawahi kuonesha dalili zozote kuwa anapenda kuona maisha ya wasanii yanaimarika.

Amekuwepo kwenye Baraza la Mawaziri kipindi chote cha uongozi wa Rais Benjamin Mkapa katika Awamu ya Tatu na amedumu chini ya Dk. Jakaya Mrisho Kikwete. Ni lini Magufuli amewahi kuwa rafiki wa wasanii?

Urafiki wa Lowassa na wasanii umeanza lini? Huyu mtu alipata mpaka kuwa waziri mkuu na kipindi chake hakuwahi kufanya jambo lolote kuonesha kwamba yeye ni mkombozi wa sanaa. Leo wanaomkimbilia wanalenga nini?

Kwa nafasi ambazo Lowassa ameshakamata na nguvu kubwa ya ushawishi aliyonayo, kama angekuwa rafiki wa wasanii, leo hii mambo yangekuwa yameshabadilika. Alijua umuhimu wao lakini aliwaona wa nini, wasanii wameshindwa kumuona wa kazi gani.

Kumbe sasa rafiki wa kweli wa wasanii anajulikana. Nilimuona Sugu, vilevile Zitto Kabwe, wengine walichukulia siyo suala muhimu lenye kuhitaji kipaumbele bungeni.

Sikatai wasanii kupanda jukwaani kuwafanyia kampeni Lowassa na Magufuli, najua huko wanafuata fedha lakini ningeona mshikamano wao kuhakikisha Sugu anarudi bungeni. Hii ni nje ya vyama vya siasa na fedha wanazolipwa.
Ningeona ubora wa wasanii kama wangekuwa wanavuna wanachopata kutoka kwa akina Magufuli na Lowassa kisha wanamchangia Sugu na pengine Zitto. Kumwacha Sugu apambane peke yake ni kuonesha kuwa wasanii hawakumbuki fadhila.

Natambua kuwa mfumo ulishawagawa wasanii siku nyingi. Hawatakuja kuwa na kauli ya pamoja mpaka wasahihishe nyendo na nafsi zao. Walishakubali kugawanywa na kutawaliwa, kwa hiyo popote walipo wanaoneana wivu kwa vitu vidogovidogo.

SUGU ANAHITAJIKA KUREKEBISHA HAYA
Sanaa ya Tanzania bado inakabiliwa na matatizo chungu nzima. Kuna janga la rushwa, yaani mpaka leo ni Tanzania peke yake ndipo msanii badala ya kulipwa mrabaha (royalty) kutokana na kazi zake kuchezwa redioni, eti yeye ndiye analipa ili muziki wake uchezwe.

Kulipia wimbo wako uchezwe redioni ni rushwa ambayo inaitwa payola. Hili ni janga ambalo linawaumiza sana wasanii nchini. Ndiyo maana wanaotamba ni wale wenye uwezo na utayari wa kulipa payola, wenzangu na mimi ni mihangaiko na mateso.

Soko la sanaa limefinywa sana hapa nchini. Yote hayo yangekuwa ajenda ya pamoja kwa sababu siyo kweli kuwa hakuna asiyeumia, kila mmoja anapigika. Tena yule anayejiona anapata fedha nyingi ndiye ananyonywa zaidi.

Lazima kuweka hilo wazi kwa sababu kuna wanaodhani kwa sababu wanapata 200 za kubadilishia mboga, magari na nyumba, wanadhani wao hawanyonywi. Kumbe wao ndiyo waathirika wakubwa, kwani mzunguko ni mzuri mpaka wanaachiwa za kununua mchele.

Wanasahau kuwa wanamuziki wameshindwa kabisa kusambaza kazi zao kutokana na kunyonywa, matokeo yake wameamua kususa hata kurekodi albam. Sidhani kama hili wanasubiri Luqman awakumbushe kupigana Sugu arudi bungeni aendelee kutengeneza njia!

Je, wanataka Sugu awape fedha wasanii ili wakamfanyie kampeni? Kwa hili la wasanii kumtenga Sugu pamoja na kazi kubwa aliyofanya, ipo siku historia itawahuku. Na waache kuamini kuwa urahisi uliopo umejileta wenyewe. Sugu amefany kazi kubwa na anahitajika zaidi kuendelea kuisemea sanaa ya Tanzania.

By Luqman Maloto
 
Ccm itashindwa vibaya sana na hawa wasanii wataona aibu sana , lakini sisi hatutalipa kisasi , tutawasamehe na tutaanza kumwombea msamaha shilole basata , mtoto akinyea mkono usikate .
 
Hivi ni Sugu yupi huyu aliesemaga mi sio mbunge wa wasanii.. Mi mbunge wa mbeya mjini Au sugu gani
 
Wasanii dzain ya shilole.wema utawaambia nn wale zaid ya kuwapuuza tu
 
Kweli Sugu alisema yeye ni Mbunge wa Mbeya sio mbunge wa wawasanii.

alisema kweli, kwani ni uongo? alikuwa mbunge wa Mbeya mjini na kama suala la kutetea wasanii linakuja basi alifanya hivyo , kwa hyo nafikiri kauli yake ime nyooka!
 
Prof jay yuko mikumu pekeyake anahangaika,akifanikiwa utasikia wasanii wakilalama,kwamba hawasemei bungeni..
 
Hatutafuti rais wa wasanii bali rais wa Watanzania wote...
 
Wasanii limekuwa kundi la watu wasio na elimu kabisa.

Ndio maana wanapelekeshwa vibaya sana.
 
Back
Top Bottom