Eti Wanzanzibar watapiga ya maoni wakiwa bara

Eti Wanzanzibar watapiga ya maoni wakiwa bara

Eliphaz the Temanite

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2010
Posts
3,018
Reaction score
1,154
Nimesikia kwa masikitiko makubwa sana kuhusu sheria ya kura ya maoni itakayo tumika kwenye kupigia Katiba pendekezwa
1. Eti Wanzanzibar watapiga kura hata wakiwa bara? Nani atawatambua, je kutakuwa na masanduku special ya Wanzanzibar. Je sheria ya kura ya maoni ya zanzibar inayomtaka mzanzibari kuwa na kitambulisho cha ukaazi na kuwa awe ameishi miaka isiyopungua 3 itapumzishwa kwa mda?
2. Sheria inataka uwepo mda usio pungua miezi 3 kufikia wananchi kupiga kura. Kwanza wananchi kuelimishwa, pili kupiga kampeni kwa kambi ya HAPANA na Ndiyo huo mda uko wapi?
3. Eti kambi za ndio na HAPANA zitatuma maombi kisha kukubaliwa ama kukataliwa uuuuwi fisi umpe nyama???
4. Hata kura ya HAPANA ikipita /ikishinda yatafanyika marejeo kisha ipigwe kura tena baada ya siku 60
5. Kwa kuwa tume ya Warioba imevunjwa nani ataratibu marejeo hayo... Nani atapeleka bungeni kwa nini tumeikataa!??

Yaani kwa ufupi, 6 na kundi lake la Maescrw mnaiua nchi hii
 
Kilicho fanywa na sita Ndani ya Bunge ndio kitafanyika tena zitangaliwa Zanzibar zimepigwa Ngapi na huku bara ndio kitaengezwa ili ifikiwe idadi inayotakiwa ,uwezekano upo wa kupigwa kura Zanzibar halafu tume ikasema Wazanzibar waliopo zanzibar wamepiga italetwa kama hivi ifuatavyo Zanzibar Ndio 45 hapana hapana 46 then watasema zikijumuishwa na wazannzibar waliopiga bara za Ndio 35 hapa 10 Ngoma juu
 
Hii ni shida, Hii inaonekana syndicate ya kutaka kuipitisha kwa namna yeyote ..........
 
Kuna uwezekano mkubwa watu wa NDIYO wakaomba (kwa sababu maalum) na wakachomekwa kwenye kambi ya HAPANA ili kufanya kampeni za kichovu na kujaribu kudhoofisha juhudi.

Kama nia ni nzuri hili halihitaji yote hayo kwani vinara wa kila kambi wanajifahamu na wanafahamika. Ni suala la kuwasiliana, uratibu na kugawana majukumu tu.
 
Back
Top Bottom