Eti wanaulizwa: Mnataka Maji au Maandamano? Wananchi: Tunataka maji, tunataka barabara!

Nape nauye anawauliza wanavijiji ati

katiba inawaletea madawa hospitali....hapana
katiba inawaletea chakula..................hapana
katiba inawaletea maji...................hapana
kadhalikakadhalika

nilivyokuwa najua mimi ni kwamba, katiba yetu ikiwa bora kutakuwa na accountability kwa viongozi hivyo hawataiba, na keki ya taifa itamegwa vizuri kwa maslahi ya wananchi wote.katiba ikiwa mbaya tutaendelea kuishi na serikali ya kifisadi milele na watu wachache watanufaika wakijijini ndio hawatapata kitu kabisa. sasa nape anaposema katiba haiwezi kuleta maji, au madawa, ana maana katiba haina faida? sasa kule dodoma wanafanya n ini sasa? na kwani katiba ikiwa nzuri hela zile ambazo wangeiba mafisadi si ndio zingewanunulia wananchi madawa na kuwaletea maji? hivi kwanini viongozi wa ccm wanawachukulia watz poa sana? miaka yote wamekuwa wakiwapiga changa la macho wanavijiji kwasababu hawana uelewa mzuri. Mungu ataisaidia Tanzania na kuiokoa na mkoloni huyu wa Tanzania.
 
Yaani sidhani kama Nape ana akili sawa wasa! eti wananchi hawahitaji katiba, wanahitaji huduma muhimu, je watapataje huduma nzuri bila kuwa na sheria mama iliyo imara?
 
huyu nape ni taahira. lakini simlaumu sana, nalaumu huyo aliyewafanya watanzania kuwa mambumbumbu kiasi cha wao kuitikia kuwa katiba haina umuhimu
 
cha msingi amefanya kwa waccm hapo ndo watajua uelewa wao ndo maana wanaenda kwenye mkutano
 
Unataka uhaidiwe kupeleka setilaiti mwezini? Ahadi zitaendelea kuwa hizi hizi hadi hapo zitakapokamilika..hakuna miujiza nchi hii tutaijenga wote...!

nina mashaka na upeo wa ubongo wako nisije kuwa najibishana na kasuku aliyemeza cd ya anayotakiwa kusema ndo maana nikasema tanganyika inahitaji uhuru wa akili ya kujua jema na baya
 
Namuunga mkono nape hata mimi sioni kama katiba ni ishu sana kagame kila siku anavunja katiba nani anamuuliza mahitaji ya watanzania ni maendeleo wala siyo katiba mnaweza kuwa na katiba nzuri ila kama hakuna viongozi waadilifu kazi bure.
 
6.jpg


Watu wenyewe ndio hawa unategemea watajibu nini ndugu?
 
Asante Mungu mtakatifu kwa kuwapiga upofu ccm, na kuwafunulia mambo haya makuu chadema na wananchi..... katiba ndiyo roho ya taifa, huwezi kuzungumzia maji au umeme bila katiba
 
kwanza mpaka mtu unaenda kwenye mkutano wa nape lazima ujitathimini
 
Namuunga mkono nape hata mimi sioni kama katiba ni ishu sana kagame kila siku anavunja katiba nani anamuuliza mahitaji ya watanzania ni maendeleo wala siyo katiba mnaweza kuwa na katiba nzuri ila kama hakuna viongozi waadilifu kazi bure.

Nafikiri hata katika mpira wa miguu cha muhimu ni wachezaji 22 uwanjani na magoli yafungwe vyiovyote. Wachezaji wala refa hawahitaji sheria 17 si muhimu. Au vp Simiyu Yetu
 
yaani leo nimeendelea kumuona nape anamawazo madogo sana kwa Siasa na Uzalendo wa taifa pia nikaona wale wasambaa wa CCM kule handeni hawana kitu kumkichwa etii hawajui katiba sasa kura ya maoni ya rasimu ya ccm watapiga vp ndo maana nasema kuwa hawa watu wa mafiC.EM 2015 yatapata kura chache kwa hao vilaza km hao wa Handeni Tanga.
 
khaki yA mungu nimemsikia nape na wananchi kwa kutoelewa kwao wakawa wanamshangilia roho imeniuma sana
 
Huyu kijana NAPE NNAUYE siyo siri ana laana!Leo akihutubia kwenye ziara zao wanazoendelea nazo kwenye mikoa ya watu waliokoseshwa elimu na CCM nimemsikia akiropoka kuwa katiba siyo kipaumbele cha watanzania,pia kasema katiba haileti maji,afya,chakula n.k
Swali langu ni je,kama katiba siyo kipaumbele chetu mchakato ulianzishwa ili iweje?Au ilikua ni muendelezo wa kula pesa zetu watanzania na kutugeuza kuwa ni wajinga?Kama katiba haileti chakula wala afya, je kwanini wanamshambulia Warioba na kumtaka akae kimya?huku mashambulizi kwa Warioba yakiongozwa na mvivu wa fikra kapteni Komba.
Ndugu yangu NAPE watanzania tumebadilika sana,kauli zako zote ziko kwenye hansard zetu watanzania mnaotubeza,tuna hasira kali sana nanyi.Sikutishi ila endelea kuropoka lakini ni suala la muda tu unaweza kujikuta unahukumiwa The Hague hivihivi,chunga sana ulimi wako.Mwenzako Mwigulu alikuwa mropokaji sana zaidi yako wewe ila ameshtuka mapema na kutambua kuwa njia anayokwenda nayo siyo,na hatimaye siku hizi kiwastani anachunga sana ulimi wake.
VIONGOZI WENZAKO WANAOKUCHEKEA USIDHANI WANAKUSHANGILIA BALI WAO WANACHEKELEA POSHO WATAKAZOVUNA KWA KUHUDHURIA HUO MKUTANO WENU.
NI USHAURI TU,KAZI KWAKO WAWEZA ENDELEA NA UPUUZI WAKO WA KUTUTUKANA WATANZANIA
 
nina mashaka na upeo wa ubongo wako nisije kuwa najibishana na kasuku aliyemeza cd ya anayotakiwa kusema ndo maana nikasema tanganyika inahitaji uhuru wa akili ya kujua jema na baya

Weka hoja mezani acha kurukaruka kama kitenesi...unataka uhaidiwe nn? Miujiza?
 
Nafikiri hata katika mpira wa miguu cha muhimu ni wachezaji 22 uwanjani na magoli yafungwe vyiovyote. Wachezaji wala refa hawahitaji sheria 17 si muhimu. Au vp Simiyu Yetu

Mara ngapi sheria 17 zinavinjwa kwa sababu za kibinadamu au vinginevyo na matokeo yanabaki kuwa vilevile..umeangalia mechi ya Man U na West Ham jana jioni?
 
Kaanza zile siasa zake za maji taka,si ni juzi tu alikashfu wazee,Nape kwanini hajirekebishi?watoto wa Lumumba tabu sana
 
Back
Top Bottom