Mkuu hayo maisha walio wengi tumepitia, binafsi nilizaliwa mjini na nikaanza shule mjini pale uhuru mchanganyiko, chini ya kina mwalimu gumbo, mfaume , kingodi, njooka na wengineo kibao, lakini babu yangu akaja toka kijijini akalazimisha twende kusomea kijijini akisema mjini tutaharibikiwa hakika mara ya kwanza niliyoweka mzigo wa kuni kichwani nilimlaani yule babu vibaya mno, lakini baadae nikazoea maisha yakasonga na kwa kiasi fulani yamenifanya nimejifunza mambo mengi yanayoizunguka jamii hasa waishio vijijini, kama alivyosema mdau mmoja miundo mbinu ikiwekwa vizuri sio kubaya kama wengi wa mjini wanavyozani.