Hivi TCRA wapo wanafanya kazi? makampuni ya cm yanaibia watu kwa kutoa matangazo kuwa unatuma PESA bure kupitia Mpesa wakati ni uongo na jamaa wa TCRA wanakwenda kazini kila siku nao wanapokea hizo SMS? kwakweli ningeomba wawekezaji dunia nzima wanaotoka kupata faida kwa KUIBIA WATEJA waziwazi waje katika JAMHURI YA MUUNGANO WA (t)DANGANYIKA.
-re-enw[wmm sana
TCRA-Tanzania Communications Rotten Authority
Kwa airtel chini ya laki moja ni bure kweli sema mawakala wengi wanagoma kufanya izo transactions za airtel as wana-claim hazina faida kwa mfano jana nilikuwa kariakoo imagine nilitembea kwa mawakala zaidi ya 9 wote hawana airtel ni voda na tigokama airtel
Makampuni hya yanafanya yakatavyo kwa kuwa hakuna WATCH DOG wa kuwakemea au kuratbu nyenendo zao, TCRA hiko likizo kabisa - familia yangu imekwisha honja joto la jiwe kutokana na mambo haya ya kutuma pesa kupitia Airtel - tulimtumia mtu laki tatu kumbe hela hazikwenda kunako husika na wenyewe wanakili kwamba walifanya makosa, lakini mpaka sasa hivi tunapo zungumza hela hizo hatujarudishiwa tunaingia mwezi wa nne, tunapigwa danadana TU.TCRA-Tanzania Communications Rotten Authority
Mkuu jamaa wa TCRA nilisha wavulia kofia kabisa, ukiangalia kwa umakini utaona kana kwamba wana woga fulani wa kuwakemea makampuni haya ya simu, yanafanya yanatavyo. Kinacho udhi zaidi ni pale wanapo taka kuamua kitu au kuweka sheria fulani za kuzibana kampuni za simu wanagwaya sana, kabla hawaja fanya uhamuzi wowote lazima waite kampuni hizo za simu eti ziwashauri wafanye nini, raia wana lalamika kutumiwa ujumbe ambao mtu haja subscribe na wakati mwingine kulazimilka kusikia sauti za matangazo kabla huja kuwa connected na client mwenzako, ukiwa na emegency call unaweza kukwama vibaya sana kwa kulazimishwa kusikiliza matangazo na mambo mengine ya kipuuzi ya kupoteza muda, kwani vipeperushi kazi yake ni NINI? Mtu unaweza kufikili labda hakuna watu wenye ujuzi wa tekinolojia ya mawasiliano, wapunguze makongamano yasiyo na TIJA kwa Taifa letu, wawe wakali na makampuni haya yasiachwe kuliweka Taifa letu kwenye rehani.hapa Tz kuna taasisi zingine huwa najiuliza uwepo wake unamaana gani kama hawa TCRA bajeti wanapewa vitendea kazi wanavyo hadi ushaidi ambao ni unajitosheleza upo sasa nini wanasubiri ili wafanye kazi au amri ya raisi au waziri husika na sekta hiyo nae mpiga deal wao nn maana inachosha sasa yani nobody is there for anybody kwenye hizi matatizo but ingekuwa ni maswala ya kura hapa fasta hii ingekuwa vice versa nobody is there for anybody
Mkuu jamaa wa TCRA nilisha wavulia kofia kabisa, ukiangalia kwa umakini utaona kana kwamba wana woga fulani wa kuwakemea makampuni haya ya simu, yanafanya yanatavyo. Kinacho udhi zaidi ni pale wanapo taka kuamua kitu au kuweka sheria fulani za kuzibana kampuni za simu wanagwaya sana, kabla hawaja fanya uhamuzi wowote lazima waite kampuni hizo za simu eti ziwashauri wafanye nini, raia wana lalamika kutumiwa ujumbe ambao mtu haja subscribe na wakati mwingine kulazimilka kusikia sauti za matangazo kabla huja kuwa connected na client mwenzako, ukiwa na emegency call unaweza kukwama vibaya sana kwa kulazimishwa kusikiliza matangazo na mambo mengine ya kipuuzi ya kupoteza muda, kwani vipeperushi kazi yake ni NINI? Mtu unaweza kufikili labda hakuna watu wenye ujuzi wa tekinolojia ya mawasiliano, wapunguze makongamano yasiyo na TIJA kwa Taifa letu, wawe wakali na makampuni haya yasiachwe kuliweka Taifa letu kwenye rehani.