Eti ni dhambi kuapa kitu alafu hujakitekeleza?

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
3,245
4,405
Habari waungwana,

Naomba kuuliza eti naweza kupata dhambi ikiwa nimeapa kuacha kitu fulani kwa wakati fulani lakini kwa bahati mbaya au nzuri sikutekeleza nilichokiahidi? Naomba maelezo yenu wakuu pia unapojibu toa na sababu niweze kuwafundisha watu wengine.
 
Soma Amri ya Pili ya Mungu. Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako, maana Bwana hatamuhesabia kuwa na haki mtu alitajae bure jina lake.

Kuapa ni kuweka nadhiri, na nadhiri inakupasa uitekeleze......
 
Soma Amri ya Pili ya Mungu. Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako, maana Bwana hatamuhesabia kuwa na haki mtu alitajae bure jina lake.

Kuapa ni kuweka nadhiri, na nadhiri inakupasa uitekeleze......
Sawa je kama nataka kuacha lakin nilisema mda huu lakin nikashindwa ila nna mpango huo je nitaandikiwa dhambi?
 
(MUHUBIRI 5:1-5)1 Jitunze mguu wako uendapo nyumbani kwa Mungu; Maana ni heri kukaribia ili usikie, Kuliko kutoa kafara ya wapumbavu; Ambao hawajui kuwa wafanya mabaya.
2 Usiseme maneno ya ujinga kwa kinywa chako, wala moyo wako usiwe na haraka kunena mbele za Mungu; kwa maana, Mungu yuko mbinguni, na wewe upo chini, Kwa hiyo maneno yako na yawe machache.
3 Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno.
4 Wewe ukimwekea Mungu nadhiri, usikawie kuiondoa; kwa kuwa yeye hawi radhi na wapumbavu; basi, uiondoe hiyo uliyoiweka nadhiri.
5 Ni afadhali usiweke nadhiri, Kuliko kuiweka usiiondoe.
 
Back
Top Bottom