Huyu Lukindo kuna mambo ameongea vizuri sana na kapotoka kwa kinana tu.
Ameongea mazuri
- Walafi wa mali katika uongozi walifanya makosa makubwa kugawana/kuuza viwanda vyote, bila kuzingatia serikali inahitaji vitegauchumi kujimudu kiasi kwamba sasahivi haina kitu imebaki ombaomba.
-Ameeleza sio sahihi kufanya mashamba ya mkonge tanga kuwa ni ya watanga peke yao na kuwaacha kuyagawana ovyo ovyo bila kufuata misingi bora ya raslimali za taifa kwa faida ya watanzania
-Ameeleza kwamba serikali imeshindwa kuwekeza kwa vijana wanamaliza vyuo vikuu hawana pakwenda maana kila kitu kimeuzwa
na kwamba suala la viongozi kuhubiri kutengeneza ajira majukwaani kwa maneno matupu bila vitendo haikubaliki
-Ameitaka serikali pia kufufua viwanda na kuvisimamia maana nikwamaana hiyo ajira ya kweli kwa vijana itapatikana
-Amehoji pia kwanini National Insurance imedumaa ikishindwa na Zanzibar insurance ilosaamba bara na visiwani kwanini? kama sio usimamizi mbovu wa viongozi? Amehoji utendaji wa baadhi ya mabenki na kuendehswa kwa hasara nk
Ameongea mengi mazuri ya kuichallenge serikali.
Kabobo na propaganda.
Huyu mzee kila challenge aloitoa kwa serikali lazima aseme Kinana anafaa na anadhan ndio tiba na suluhisho la matatizo.
hapa naungana na mleta hoja sion ukweli wa kumpigia debe Kinana kama nabii aliyekuja na hakuwepo serikalini Kama mmoja wa
washauri wa Rais, vipi leo aonekane muarobaini na sio feki maana siku zote anazunguuka humohumo chamani ccm? Hapa nahisi
labda kaandaliwa kuja kuhadaa watanzania, why KINANA TODAY AND NOT ALL THOSE DAYS?