Eti mzee Kinana kuwa mu-arobaini wa mapinduzi ya Uchumi?

Sep 28, 2012
87
32
Kuna Mzee anaitwa Lukindo? ITV kipindi cha kumekucha eti anasema kuwa yeye anamuamini mzee Kinana sana kama alivyokuwa Sokoine na ndiye pekee atakayeleta mapinduzi ya viwanda na uchumi kwa ujumla. So far ameshamtaja Kinana nadhani zaidi ya mara 12 kama mkombozi wa Taifa kuleta mapinduzi ya viwanda.

Hawa ndio wanaotumwa kujaribu ku-brainwash watu. Katika karne hii huwezi kuja ukatutamkia mtu ambaye amekuwa kwenye system muda wote wakati hayo mashirika yanabinafsishwa; amekuwa mmoja wa washauri wakuu na Meneja kampeni wa Rais kipindi kilichopita sasa ana nini kipya? JF amkweni muangalie TV muone anachoongea. Kinana ni Mtu wa kawaida kama wengine na nasema hana tofauti kuliko mzee Mkama. Mapinduzi yanaletwa na wananchi wote na viongozi wao wote kwa utashi wa maendeleo, uzalendo na kupambana na mafisadi sio mtu mmoja eti kuwa mu-arobaini nakataa kata kata!!.
 
Huyu Lukindo kuna mambo ameongea vizuri sana na kapotoka kwa kinana tu.

Ameongea mazuri

- Walafi wa mali katika uongozi walifanya makosa makubwa kugawana/kuuza viwanda vyote, bila kuzingatia serikali inahitaji vitegauchumi kujimudu kiasi kwamba sasahivi haina kitu imebaki ombaomba.

-Ameeleza sio sahihi kufanya mashamba ya mkonge tanga kuwa ni ya watanga peke yao na kuwaacha kuyagawana ovyo ovyo bila kufuata misingi bora ya raslimali za taifa kwa faida ya watanzania

-Ameeleza kwamba serikali imeshindwa kuwekeza kwa vijana wanamaliza vyuo vikuu hawana pakwenda maana kila kitu kimeuzwa

na kwamba suala la viongozi kuhubiri kutengeneza ajira majukwaani kwa maneno matupu bila vitendo haikubaliki

-Ameitaka serikali pia kufufua viwanda na kuvisimamia maana nikwamaana hiyo ajira ya kweli kwa vijana itapatikana

-Amehoji pia kwanini National Insurance imedumaa ikishindwa na Zanzibar insurance ilosaamba bara na visiwani kwanini? kama sio usimamizi mbovu wa viongozi? Amehoji utendaji wa baadhi ya mabenki na kuendehswa kwa hasara nk

Ameongea mengi mazuri ya kuichallenge serikali.

Kabobo na propaganda.
Huyu mzee kila challenge aloitoa kwa serikali lazima aseme Kinana anafaa na anadhan ndio tiba na suluhisho la matatizo.

hapa naungana na mleta hoja sion ukweli wa kumpigia debe Kinana kama nabii aliyekuja na hakuwepo serikalini Kama mmoja wa

washauri wa Rais, vipi leo aonekane muarobaini na sio feki maana siku zote anazunguuka humohumo chamani ccm? Hapa nahisi

labda kaandaliwa kuja kuhadaa watanzania, why KINANA TODAY AND NOT ALL THOSE DAYS?
 
Tangu sokoine aingie kaburini hakuna hata mmoja aliyekuja na msimamo dhabiti kama wake.
Huyo mzee kaamua kumtukana hayati Sokoine.
 
mi kanikera sana. mapinduzi gani ya uchumi wakati vijana wanaotegemewa wanazidi kutopea katika ujinga! Elimu hii mbovu ya tanzania itatupelekaje kwanye mapinduzi ya uchumi! Wenzetu malaysia na indonesia waliwekeza kwanza kwenye elimu na utafiti. Sisi shule zetu watoto bado wanakaa chini miaka 50 baada ya uhuru. Kitabu kimoja wanatumia watoto 10! Shule hazina walimu wa kutosha na walioandaliwa vizuri. Bajeti ya serikali kwenye elimu haizidi 12%. Katika mazingira haya mapinduzi ya uchumi yataanzia wapi? Viwanda alivyoanzisha Nyerere mmeuza, ardhi mnagawa kama njugu kwa wageni. Madini mmewapa wageni wajichukulie. Kila kiongozi pamoja na huyo kinana wameshajichukulia vyao na wamekuwa mawakala na wawekezaji na mafisadi. CCM hawaliwezi hili. Wawaachie wengine wafanye
 
Waswahili husema NJIA YA MUNGU NI FUPI, wananchi msipoteze muda kumjadili Kinana kwa sababu utajulikana punde.
Kwanza yeye ni katibu wa chama tu si mtendaji wa serikali na si Raisi wala mwenyekiti wa hilo chama.
Je ana ubavu wa kumfukuza mtu yeyote kwenye chama au serikalini ?
Yeye ni mtendaji wa chama na si wa serikali atakuzaje uchumi wa nchi ?
Ngoja tusubiri tuone
 
Kinana wizi mtupu, alikuwa wapi muda wote kumshauri mwenyekiti wake atumie uwezo alionao kuweka mambo sawa leo aje yeye alafu aitwe mwarobaini, tuliwaona akina Nepi na Mukama walianza kwa mbwembwe lakini wapi! tutamuona tu kwani kikubwa ni uzima.
 
Nadhani huyu mzee, anatamani atokee mtu kama Sokoine. Kama kinana ni mwarobaini, basi ulishadunda haufai tena kwa tiba.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom