Eti kwa nini Sisi Yanga tunajaa kwenye mechi za Simba ! hili swali limenikwaza sana.

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,360
11,514
watanzania tulikuwa watu wenye mapenzi mema hapo zamani. ilikuwa hata kwenye krismass wakristo wanawalika waislamu na kwenye idi waislamu wanawaarika wakristo. ndo tulivyolelewa na misingi hiyo toka kwa mwalimu julius kambarage nyerere.

leo simba wameanza tabia ya kutubagua. wanatubagua sisi wanayanga .nimeumia sana mtu anauliza kwa nini sisi wana yanga tunajaa kwenye mechi za simba. hili swali la kipuuzi.swali la kipuuzih sana. ina maana sisi hatupendi burudani? sisi hatupendi kuona mpira ukitandazwa na wachezaji wenye uwezo? kwa nini wanasimba mnataka kuingiwa na roho mbaya na uchoyo?

mnataka mechi zenu muwe mna enjoy ninyi pekee tu? sisi ndo mnadhani tunapenda kuangalia mechi za matapu tapu? hizo ni roho mbaya. nasisi tunataka kuona mpira unaochezwa na akina chama, unaochezwa na akina okwi n.k tutakuja tu hata kama mtatutenga na kutufanyia fujo.hata kama mtatuteka..tutakuja tu.

potelea mbali semeni ya kusema ila kwenye mechi za simba tutatia timu. hata kama tutaangalia mechi kwa kuvizia au kuchungulia wacha iwe hivyo ila piga ua nasi tunataka kuangalia kandanda uwanjani. mkome kuuliza hili swali lina kera sana na kuumiza roho.hata sisi ni binadamu tunahitaji burudani na faraja.
 
Hahaha... Pole sana Mkuu kwa kutengwa.. Hao watakua ni mamluki wanaowafanyia hivyo.. Simba hatuna tabia hiyo. Karibuni.
 
nashukuru ndugu yangu.... mtani muongo ni mchawi. simba mpira mnacheza tuacheni masikhara... mwacheza wallah... magoli mwapata na burdani mwatoa kwa watizamaji. wallah mapata ushungu kama hii team ingekuwa ndiyo yangu ngekuwa nalipia kiingilio times 10 ... aaahh.. hawa wachezaji mnawafanyaje? wanachezaji na mpira utadhani miguuni wamevaa sumaku? wallah sitoacha kuja angalia mechi zenu. zinanisaidia kupunguza mawazo na kusahau machungu ya dunia hii.

wamemsajili Chama ..kwenye dirisha dogo wanamsajili striker hatari Chips snack's.....
 
Mbona wewe pasipo shaka yeyote ni shabiki wa simba acha kuchezea akili za watu wazima hapa. Hata sisi yanga tunatandaza soccer safi kabisa karibu sana mkuu.
Mkuu.. Mbona mnaanza kumtenga mwenzenu?? Huyu ni shabiki wa Yanga.. Ila kaamua kuongea ukweli, ili awe huru.
 
Jana niliamua kwenda Banda-Umiza mechi ya Simba ilikuwa inaoneshwa sambamaba na mechi ya elclassico Barcelona vs Madrid na man utd Vs Everton chaajabu Kwa soka lilivyotandazwa na akina chama ukumbi mzima ulisimama na kulazimisha Simba ioneshwa kwenye big screen 2 man utd ikatolewa!

Hakika Kwa simbaa hiii kuna timu watakuja kuweka Mpira kwapani walahii!
 
Kwa nini unamchagulia team wakat ashasema team yake,

Mbona wewe pasipo shaka yeyote ni shabiki wa simba acha kuchezea akili za watu wazima hapa. Hata sisi yanga tunatandaza soccer safi kabisa karibu sana mkuu.
 
watanzania tulikuwa watu wenye mapenzi mema hapo zamani. ilikuwa hata kwenye krismass wakristo wanawalika waislamu na kwenye idi waislamu wanawaarika wakristo. ndo tulivyolelewa na misingi hiyo toka kwa mwalimu julius kambarage nyerere.

leo simba wameanza tabia ya kutubagua. wanatubagua sisi wanayanga .nimeumia sana mtu anauliza kwa nini sisi wana yanga tunajaa kwenye mechi za simba. hili swali la kipuuzi.swali la kipuuzih sana. ina maana sisi hatupendi burudani? sisi hatupendi kuona mpira ukitandazwa na wachezaji wenye uwezo? kwa nini wanasimba mnataka kuingiwa na roho mbaya na uchoyo?

mnataka mechi zenu muwe mna enjoy ninyi pekee tu? sisi ndo mnadhani tunapenda kuangalia mechi za matapu tapu? hizo ni roho mbaya. nasisi tunataka kuona mpira unaochezwa na akina chama, unaochezwa na akina okwi n.k tutakuja tu hata kama mtatutenga na kutufanyia fujo.hata kama mtatuteka..tutakuja tu.

potelea mbali semeni ya kusema ila kwenye mechi za simba tutatia timu. hata kama tutaangalia mechi kwa kuvizia au kuchungulia wacha iwe hivyo ila piga ua nasi tunataka kuangalia kandanda uwanjani. mkome kuuliza hili swali lina kera sana na kuumiza roho.hata sisi ni binadamu tunahitaji burudani na faraja.

Nchi hii mashabiki wengi wa mpira ni Yanga...sasa kama unataka wasiingie uwanjani sawa kwani watakaokosa mapato ya mechi ni ninyi Simba...Yanga pia ndio wanunuzi wakubwa wa magazeti ya michezo ...wauulize wahariri wote kwenye vyumba vya habari vya magazeti watakwambia ukweli..Yanga ikishinda magazeti mengi hununuliwa ila Yanga ikifungwa ununuzi wa magazeti hudoda...Ndiyo maana Yanga ikiwa haifanyi vizuri wahariri hutafuta vichwa vya habari angalau vya kuvutia ili angalau kuwavuta wanunuzi....kwa ufafanuzi zaidi Yanga ni timu ya wananchi, wengi wao ni watu wa kawaida sana ingawa ni kweli mashabiki wake wengi ni mchanganyiko, lakini walio wengi ni mashabiki wenye kipato cha kawaida...Fanya utafiti katika watu kumi nchini...sita au saba lazima wawe ni Yanga... ...
 
nashukuru ndugu yangu.... mtani muongo ni mchawi. simba mpira mnacheza tuacheni masikhara... mwacheza wallah... magoli mwapata na burdani mwatoa kwa watizamaji. wallah mapata ushungu kama hii team ingekuwa ndiyo yangu ngekuwa nalipia kiingilio times 10 ... aaahh.. hawa wachezaji mnawafanyaje? wanachezaji na mpira utadhani miguuni wamevaa sumaku? wallah sitoacha kuja angalia mechi zenu. zinanisaidia kupunguza mawazo na kusahau machungu ya dunia hii.
Komeo la chuma bila shaka wewe ni mpemba!
 
swadakta .... mejuaje weye jambo hili? mi natokea pemba. nipo hapa dar nafanya biashara.karibu sana nyumbani yakhe.. nawe watokea pemba? mi nkazi wa chake chake..... siye ndugu ati. nawe nshabiki wa simba au yanga? kwa kweli mi naangalia sana game za simba hii team yacheza sana.... lakini simba waanza kutubania sisi wanayanga ati tusiende wanjani kuangalia games zao.hii mimi nshatesa sana leo nkaona bora nseme ili kama yeshe yeshe tu rohoni niwe na amani. mi shekhe nnapenda mpira sana hivyo.
Komeo la chuma bila shaka wewe ni mpemba!
 
Nchi hii mashabiki wengi wa mpira ni Yanga...sasa kama unataka wasiingie uwanjani sawa kwani watakaokosa mapato ya mechi ni ninyi Simba...Yanga pia ndio wanunuzi wakubwa wa magazeti ya michezo ...wauulize wahariri wote kwenye vyumba vya habari vya magazeti watakwambia ukweli..Yanga ikishinda magazeti mengi hununuliwa ila Yanga ikifungwa ununuzi wa magazeti hudoda...Ndiyo maana Yanga ikiwa haifanyi vizuri wahariri hutafuta vichwa vya habari angalau vya kuvutia ili angalau kuwavuta wanunuzi....kwa ufafanuzi zaidi Yanga ni timu ya wananchi, wengi wao ni watu wa kawaida sana ingawa ni kweli mashabiki wake wengi ni mchanganyiko, lakini walio wengi ni mashabiki wenye kipato cha kawaida...Fanya utafiti katika watu kumi nchini...sita au saba lazima wawe ni Yanga... ...
Naona unataka kujitetea kwamba mnavyoomba omba ni sawa kwa timu ka Yanga bingwa wa kihistoria kwa sababu ni ya wa kipato cha chini
 
ubishi usio na tija...ubishi usiojenga...ushabiki...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom