Hapa akina Nyamayao,Agika,WOS,MJ1,Joyceline,Chaku,BelindaJacob na wengineo wengi mtanipa 5 nimeichomoa hukooo uswazi.
Aksante sana Fidel leo of all the days umenifurahisha. Umesomeka vilivyo sina cha kuongeza ila tu hapo kwenye gubu sina la kusema maana mh
Kama ulikuwepo Fidel! Umejuaje?Unajua dada WOS umepotea sana sijui mzee amekuchimba mkwala usiingie JF tunakumiss dada michango yako ni muhimu sana akina Nyamaya,MJ1,Agika,Chaku wanasubili sana nashukuru kwa comment.
jamani tena ukikutana na mwanaume mwenye Gubu ,ndio hatari,unless uwe na Yesu moyoni
Well said dada!..... yaani umenifumba mdomo vibaya mno maana nilishaanzakuandika na macho kabla ya vidole fidel anapotuelekezea shutma sie wanawake tu wakati na wao wanaume wanazo hizo tabia hapo zooote na zaidi na hilo gubu ndo usiombe , yeee mwenyewe hapa jamvini ana gubu ile mbaya sembuse huyo mwenza wake (MWJ1) mtarajiwa sijui itakuwaje.Fidel umesomeka ndugu yangu....
1.Haya ni mambo ya kawaida sana kusemwa kama ngonjera..ila kwa vile na wewe umeinukuu hukooo unakojua siwezi kuanzisha mdahalo....
2.Ningependa labda kuongezea kuwa hizo kero ni msumeno ukatao kotekote...bila kujali mtenda ni mwanamke na mtendewa ni mwanaume.Hakuna binaadamu apendae maudhi, gubu, fitina, usaliti,uchafu wala uvivu.Sote tunapenda raha na hatupendi karaha.
kwa kifupi ni kwamba ...ili penzi lishamiri inabidi kufuata the golden rule:
DO UNTO OTHERS WHAT YOU WOULD LIKE THEM TO DO TO YOU....
USIMTENDEE MWENZIO LILE AMBALO WEWE LITAKUUMIZA.
3.Binadamu kwa ubinafsi tuliokuwa nao mara zote atataka yeye tu ndio atendewe mema ilhali yeye yu mwepesi kumtendea mwenzake yaleyale asiyopenda kutendewa.Ni mpaka hapo watu watakapojaaliwa kuwa na moyo usio wa ubinafsi ndipo kutakuwa na mapenzi ya kweli yasio na chungu ya aina yeyote ile.Kama hili linawezekana ama la SIWEZI KUJIBU kwa maana inahitaji mtu mkamilifu 100%.Kama yupo binadamu wa aina hiyo tufahamishwe ili tumtumie kama role model wa "YES IT IS POSSIBLE CAMPAIGN!"
mhhhh weee nawe? akuuu nikapike ftari mie nisiharibu saum yanguWIVU
wivu nao mkuu ni sumu mbaya, ongezea hapo,
usichukue uamuzi wa ghafla pasipo kufanya uchunguzi, umeona mkeo/mumeo kasimama na mtu huulizi unaanza kuwaka, labda ndugu yake je?
UBINAFSI
usijipende wewe mwenyewe, show love kwa mwenzako bana hata kama anakipato kikubwa au kidogo.
kingine kwenye malovedavee mpe raha mwenzako nae akupe!!, sio watu mko kama magogo raha unajipa mwenyewe tu, ala.
Usaliti mamiii unaona si mchezo , bora hayo mengine unaweza umwache abwatuke mwenyewe lakini usaliti huna jinsi ya kukimbia maumivu .Mungu atunusuruWOS kamaliza yote, hayo mengine unaweza vumilia kidogo lakini kwangu mie inapofikia swala la usaliti nachoka kabisaaa....
Usaliti mamiii unaona si mchezo , bora hayo mengine unaweza umwache abwatuke mwenyewe lakini usaliti huna jinsi ya kukimbia maumivu .Mungu atunusuru
weeee fidel weeee temea mate chini kaka, usaliti haujalishi kama mwanzo mlikuwa mnapendana au vipi ni shetani tu anapoamua kufanya kazi yake kuwaingilia wenye ndoa, ukitaka kujua ukweli weee tafuta unayempenda na kuamini na wewe anakupenda atleast utakuwa sured kwa upande wako halafu talk to me baada ya miaka miwili ya ndoa, tena nyie wanaume ndio kwenye hili hamna muamana kabisaaa hata mtu kama MWJ anapojikusulu kukupa mapenzi yote lakini bado utamsaliti, sababu za usaliti ziko nyingi tena complex inategemeana tu na mazingira waliyopo wanandoa wale.Usaliti nafikiri unakuja pindi mtu amekuoa/kuolewa kwa kulazimishwa na hakuwa na namna anaamua kudondokea kwenye ndoa ambayo hakutarajia matokeo yake ndo haya sasa mnaanza kusalitiana.
weeee fidel weeee temea mate chini kaka, usaliti haujalishi kama mwanzo mlikuwa mnapendana au vipi ni shetani tu anapoamua kufanya kazi yake kuwaingilia wenye ndoa, ukitaka kujua ukweli weee tafuta unayempenda na kuamini na wewe anakupenda atleast utakuwa sured kwa upande wako halafu talk to me baada ya miaka miwili ya ndoa, tena nyie wanaume ndio kwenye hili hamna muamana kabisaaa hata mtu kama MWJ anapojikusulu kukupa mapenzi yote lakini bado utamsaliti, sababu za usaliti ziko nyingi tena complex inategemeana tu na mazingira waliyopo wanandoa wale.
kesho tutajadili zaidi saa hizi naenda kupika ftari. na hassa nataka kuongelea lile la usafi maana japo linatuhusu wote mwanamke na mwanamme anaeplay big part ni mwanamke.