Kuna suala lilizua mjadala mahali kwamba,woaji sikuhizi hawapatikani wengine wakasema no!waoaji wapo ila waolewaji wamekua na vigezo vingi mno kumchambua huyo muoaji ndio maana suala la relationship na relationship zinazoishia kwenye ndoa linaonekana kama gumu siku hizi au hata hizo ndoa hazidumu sijui mnaonaje hili??

Ni kweli, binadamu wa sasa wamekuwa too selective hasa pale anapopata multiple choices. Si mwanamke wala mwanaume.
Kuna kipindi fulani EATV muda kidogo uliopita, mtaalam mmoja (mwanamke) wa saikolojia na mahusiano alielezea upande wa wanawake wengi wa mijini kutaka kuolewa na mwanaume ambaye tayari ana maisha mazuri au ana future nzuri ya maisha hasa kiuchumi. Na wanaume wa aina hiyo wanahesabika kuliko wanaume wengine.
Mi nadhani ni mabadiliko ya kiuchumi duniani pia yanachangia ambapo wanawake wengi, mbali na suala la mapenzi ya dhati, pia wangependa kupata mwanaume ambaye atasaidia familia kiuchumi kwa kiasi kikubwa kuliko mwanaume ambaye anategemea pato la mwanamke zaidi.
Kumchambua huyo muoaji unamaanisha nini?
Mbona wanawake wengi sana siku hizi ni "niangusage"?
Kumchambua huyo muoaji unamaanisha nini?
Mbona wanawake wengi sana siku hizi ni "niangusage"?
Ndoa ni jambo linaloweza kubadili uelekeo wa maisha yako kabisa,hivyo uchambuzi ni muhimu ili kupata mwenzi mwenye dira na uelekeo wako ili kuepusha janga la migongano huko mbeleni ambayo huishia separation na kukwaza familia wakati muda nao ushapotea hata kuanza upya haiwezekani tena.
Inawezekana wadada ni wachambuaji maana hata mimi
lazima nichague na naamini hiyo ipo kwa wote.
Lakini wanaume hatuwaelewi wanataka nini, anaweza
kuwa na mpenzi miaka halafu ghafla anamuacha na ndani
ya muda mfupi anatangaza ndoa na mwingine!
Sasa kwa hili sijui nani mwenye choice zaidi.