Eti Kanali Mstaafu Haruni Ramadhani kajitoa kafara

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,119

Sasa iweje mtu aliyejitoa kafara aogope kupambana na ufisadi wa Escrow, Lugumi, UDA, PRIDE, Boti bovu la kwenda Bagamoyo? Hao watu wenye nguvu ni akina nani? Na hizi nguvu wanazitoa wapi? Wana nguvu kuliko vyombo vya dola polisi, jeshi na mahakama? Na kwa nini wanaogopwa kutajwa hao wenye nguvu?

Kuna juhudi za kumpandisha chart huyu maana credibility yake inaanguka kwa kasi ya kutisha.
 
mambo yanatakiwa polepole, figisufigisu kila kona
nao wanajipanga na familia zao, kwani wanaotumbuliwa vinawauma
angalia sukari, tunaiona kabisa ghalani na tunaambiwa kesho itasambazwa
mara hamadi haionekani hata ya vumbi ila ya Brazili ya 5,000/ @kg
haya mambo mtu mmoja bila ushirikiano hayaendi BINADAMU SIO WATU
 
Eti credibility ya Rais inashuka, kwani wewe ndiye uliipandisha.

Kuna baadhi ya watu mnahitaji msaada kifikra.

Huyu hapa chini kama ulivyosema ndiye haogopi RICHMOND kwa sababu amejitoa kafara kupambana kwa sababu ni tumaini la mafisadi!
Lowassa ni tumaini la mafisadi, wezi, wahuni, majangili na magaidi na wauza unga nchini. Haiwezekani kiongozi mzuri mwenye sifa za kuiongoza nchi aanze kampeni zake kwa kutoa rushwa ya mamilioni katika nyumba za ibada halafu akadaiwa eti ni "tumaini la Watanzania"
Siku hizi hutaji tena neno RICHMOND kwenye post zako kwa sababu siku za nyuma ulikuwa husahau kuweka neno hilo na imekuwa ni kama sumu kulitaja jina la Lowassa.

Wanafiki mna kazi kweli kweli.
 
Kama kajitoa kafara ataje mshahara wake, uwe wazi kwenye tovuti ya Ikulu, ataje marupurupu yake yote, yawe wazi kwenye tovuti ya Ikulu. Ama awe anatoa wuarterly report ya mapato yake kupitia magazeti, ili tufahame naye analipa kodi kiasi gani. Na kubwa ya yote ni naye apunguze mshahara wake pamoja na marupurupu.
 
Kuonyesha kama unachokiandika hakina mantiki au hufahamu mantiki yake ni pale unapotaka ataje mshahara wake halafu hapo hapo unasema apunguze mshahara wake.

Mtu anayetumia mantiki atafahamu unaposema apunguze mshahara wake ina maana unaufahamu mshahara wake.

Mbaya zaidi, unaandika katika mlengo wa kukariri kwa sababu hakuna sheria inayosema ukijitoa mhanga lazima utaje mshahara wako na marupurupu yako.

Hivi hizi fikra mnazinunua wapi ambako wengine hatuzipati?
 
Ahahaha:
a)Kanali Anautaka Ukuu wa Mkoa!?
b)Anasema Yeye Sio Mwanasiasa,sasa mbona anaongea siasa mwanzo mpaka mwisho?
c)Anasema Magufuli ana Uchungu na Nia ya Nchi yake,na Uso wake unaonesha hivyo anapo uhubiri ukafara wake,je amempima na chombo gani akathibitisha kuwa uzalendo huo kweli moyoni?
d)Kanali amekuja kuokoa jahazi la Magufuli?Maana naona jamaa amepoooa!
 
Kuonyesha kama unachokiandika hakina mantiki au hufahamu mantiki yake ni pale unapotaka ataje mshahara wake halafu hapo hapo unasema apunguze mshahara wake.

Mtu anayetumia mantiki atafahamu unaposema apunguze mshahara wake ina maana unaufahamu mshahara wake

Braza kaka, ninaposema apunguze mshahara wake haina maana (kimantiki) kwamba mshahara wake ni mkubwa! Vilevile, kama aliweza kusema atatoa shilingi milioni 6 kwenye mshahara wake ili achangie ununuzi wa madawati Dar, hakika mshahara wake utakuwa mkubwa tu. Hata tu-assume milioni 6 ndiyo mshahara wake, yeye anapewa kila bure, mshahara wa milioni 6, bado waweza punguzwa hata kwa half, na bado akaishi.

Msingi wa hoja yangu ni yeye kama Rais kuonyesha mfano. Anasema serikalini hakutakuwa na mshahara zaidi ya milioni 15, hii angepaswa aonyeshe mfano kwa kupunguza naye mshahara wake. Na kama unatumia hata common sense, utafahamu kwamba pale atakapopunguza, basi ataweka wazi kiasi alichokuwa akipata awali. Na suala la pili ni la yeye kuonyesha mfano katika kulipa kodi. Anasema watanzania tupende kulipa kodi, je, yeye analipa kiasi gani? Na hapa tena, kama unatumia common sense, utafahamu kwamba akionyesha kiwango cha kodi anacholipa, basi ataweka wazi pia kiasi anachopata.

BTW, ni yeye mwenyewe aliyesema ataweka wazi mshahara wake. Hivyo mimi ninamkumbusha tu, na sitochoka kumkumbusha.

NB: asisahau pia kutangaza mali zake hadharani na alivyozipata. Si anapenda publicity? Basi aweke hadhaharani kwa press release, halafu Garson Msigwa apatie media zote. Afanye hivyo na siku anaondoka Ikulu.
 
Kuonyesha kama unachokiandika hakina mantiki au hufahamu mantiki yake ni pale unapotaka ataje mshahara wake halafu hapo hapo unasema apunguze mshahara wake.

Mtu anayetumia mantiki atafahamu unaposema apunguze mshahara wake ina maana unaufahamu mshahara wake.

Mbaya zaidi, unaandika katika mlengo wa kukariri kwa sababu hakuna sheria inayosema ukijitoa mhanga lazima utaje mshahara wako na marupurupu yako.

Hivi hizi fikra mnazinunua wapi ambako wengine hatuzipati?
Mkuu umewakilisha mawazo yangu, kuna watu hawaelewi nchi inaendaje, sijui hata akitajiwa mshahara wa rais atanufaika nini, hapo hapo tena anataka mshahara wa Rais upunguzwe sijui kajuaje kwamba ni mkubwa mno.
 
Braza kaka, ninaposema apunguze mshahara wake haina maana (kimantiki) kwamba mshahara wake ni mkubwa! Vilevile, kama aliweza kusema atatoa shilingi milioni 6 kwenye mshahara wake ili achangie ununuzi wa madawati Dar, hakika mshahara wake utakuwa mkubwa tu. Hata tu-assume milioni 6 ndiyo mshahara wake, yeye anapewa kila bure, mshahara wa milioni 6, bado waweza punguzwa hata kwa half, na bado akaishi.

Msingi wa hoja yangu ni yeye kama Rais kuonyesha mfano. Anasema serikalini hakutakuwa na mshahara zaidi ya milioni 15, hii angepaswa aonyeshe mfano kwa kupunguza naye mshahara wake. Na kama unatumia hata common sense, utafahamu kwamba pale atakapopunguza, basi ataweka wazi kiasi alichokuwa akipata awali. Na suala la pili ni la yeye kuonyesha mfano katika kulipa kodi. Anasema watanzania tupende kulipa kodi, je, yeye analipa kiasi gani? Na hapa tena, kama unatumia common sense, utafahamu kwamba akionyesha kiwango cha kodi anacholipa, basi ataweka wazi pia kiasi anachopata.

BTW, ni yeye mwenyewe aliyesema ataweka wazi mshahara wake. Hivyo mimi ninamkumbusha tu, na sitochoka kumkumbusha.

NB: asisahau pia kutangaza mali zake hadharani na alivyozipata. Si anapenda publicity? Basi aweke hadhaharani kwa press release, halafu Garson Msigwa apatie media zote. Afanye hivyo na siku anaondoka Ikulu.
Kuna mambo mengine hayana hata maslahi kabsa changamoto ziko nyingi wewe unakomaa na mshahara wa rais mara alipe kodi, majukumu aliyonayo ni kodi tosha, tatizo lenu ni chuki za hali ya juu dhidi ya rais zinawasumbua, wala hakuna hoja za msingi za kumuandama zitakazoleta maendeleo.
 
Back
Top Bottom