Eti Kanali Mstaafu Haruni Ramadhani kajitoa kafara

Magufuli bora urudi kijijini kwenu ukachunge ng'ombe. Huwezi kuongoza Tanzania ya 2016 kwa kuwaogopa mafisadi, wezi, wala rushwa na huku ukibaka demokrasi nchi kwa kiwango cha juu kabisa na kutaka kuongoza kwa sera za kukurupuka.

~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*

*Asema atabanana na wala rushwa kila kona

*Aeleza yuko tayari kuchunga ng’ombe kijiji

NA ESTHER MNYIKA, DAR ES SALAAM

RAIS Dk. John Magufuli amesema wazee ndiyo wameharibu nchi hadi ilipofika sasa.

Amesema yuko tayari kurudi kijijini kwao akachunge ng’ombe kuliko kuwavumilia wala rushwa nchini.

“Wazee tukitoka tuacha nchi safi, sisi wazee ndiyo tumeharibu nchi hapa tulipofikia,”alisema Rais Dk. Magufuli

Rais alisema kutokana na uozo uliojaa serikalini, lazima ataendelea kuwachukulia hatua wanaokiuka taratibu za utumishi hadi watendaji watakapobadilika.

Aliyasema hayo alipofungua mkutano wa Bodi ya Wakandarasi Tanzania, Dar es Salaam jana.

Alisema watendaji wa Serikali yake ni lazima wabadilike akisisitiza kuwa suala la utumbuaji majipu kwake siyo la muda mfupi na hatalibadili kamwe.

Kiongozi huyo wa nchi, alisema atahakikisha anaongeza vijana wengi katika Serikali yake kwa sababu hawapendi rushwa ingawa kuna watu wamekuwa wakiwachukia.

Alisema atahakikisha anajenga nidhamu ndani ya Serikali kwa kuwa na watumishi wenye kujituma kwa maslahi ya nchi na watu wake.

“Kazi hii nilipewa na Mungu sikupewa na mtu yeyote, nipo tayari kutoa sadaka mwili wangu kwa ajili ya watanzania wanyonge.

“Huo ndiyo mwongozo katika utendaji wangu kamwe sitabadilisha, nitawashughulikia kweli kweli,” alisema Rais Magufuli.

Akizungumzia changamoto ndani ya Serikali, alisema pamoja na hali hiyo bado anafahamu umuhimu wa sekta ya ujenzi katika maendeleo.

Rais alisema serikali yake ipo tayari kuwapa kipaumbele wakandarasi wa Tanzania inapotangazwa zabuni za miradi ya ujenzi.

Lakini amewataka kujirekebisha kwa kupanga viwango vinavyostahili vya gharama za ujenzi wa miradi hiyo ambavyo serikali itaridhika.

“Nawatolea mfano… idara ya mahakama imetangaza kujenga mahakama za mwanzo na za wilaya, kwenye bajeti wana Sh bilioni 24.

“Makadirio ya kitaalamu yanaonyesha kila jengo lisizidi Sh milioni 200, wakandarasi wazalendo walipoomba katika nyaraka zao wametaka jengo moja lijengwe kwa Sh bilioni moja na Sh milioni 400!

“Sasa nakuuliza Mheshimiwa Mwenyekiti na ndugu wakandarasi, hata kama una upendeleo, upendeleo huo utapasua moyo. Hata kama utakuwa na upendeleo kiasi gani kwa wazalendo utashindwa.

“Sasa mimi niwaombe ndugu zangu wakandarasi, pamoja na nia nzuri ya serikali kuwasaidia wakandarasi wazalendo, ni lazima na ninyi muwe na nia nzuri ya kuisadia nchi,” alisema.

Rais aliwataka wakandarasi hao kuacha kutoa rushwa kwa watendaji wa serikali wanapoomba zabuni za ujenzi na badala yake watoe taarifa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru) watendaji hao wakamatwe na kuchukuliwa hatua za sheria.

“Mimi niwaombe wakandarasi, msikubali kutoa rushwa, na muwafichue watendaji wanaoomba rushwa.

“Atakapokuomba wewe rushwa hujui amewaomba wangapi, na utakapotoa rushwa huna hakika kama ile tenda utaipata.

“Wengine wameishia kutoa rushwa hapa, rushwa hapa, rushwa hapa, mpaka anafilisika… kazi huipati na rushwa umeitoa,” alisema.

Vilevile, amewataka wakandarasi hao kujipanga ipasavyo waweze kupata zabuni katika kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi nchini ikiwamo ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima Uganda hadi bandari ya Tanga, ujenzi wa Reli ya Kati na ujenzi wa viwanda.

“Sina uhakika mmejipangaje wakandarasi wa Tanzania katika kuhakikisha hiyo kazi mnaipata, ya kujenga bomba kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga.

“Nitasikitika sana kilometa zote 1,410 pasiwepo mkandarasi hata mmoja wa kutoka Tanzania.

“Wenzetu wanajipanga, na ninavyoona wakandarasi wa Tanzania wameendelea sana, lakini nashindwa kuelewa kuna tatizo gani linatufanya kutojua changamoto zinazotukabili.

“Tumejipanga kujenga reli ya kati ya Standard Gauge kwenye bajeti ya mwaka huu tunaanza na kilometa 100.

“… lakini kuna fedha nyingine zitatolewa na serikali ya China, tutajenga zaidi ya kilometa 1,200 Standard Gauge, Central Corridor itakayounganisha Mwanza, Kigoma, Burundi na Rwanda. Wakandarasi wa Tanzania mmejipangaje?” alisema na kuhoji Rais Magufuli.

Alisema kwa sasa sekta ya kilimo ambayo karibu ya watanzania asilimia 80 wanaitegemea huwezi ukawaacha wakandarasi kwa sababu dhana wanazotumia wengi kwenye kilimo zimetengenezwa na wakandarasi.

Rais Dk. Magufuli alisema kuna sekta nyingi zinategemea wakandarasi ikiwamo sekta ya uvuvi ambayo imekuwa ikichangia pato dogo kwa Taifa.

Alisema sekta ya madini ambayo Tanzania imebahatika kuwa na madini mengi, karibu madini yote yanayopatikana duniani, na Tanzania yapo kwa asilimia kubwa.

“Madini hayo ambayo ni Tanzanite, Diamond Uranium na gram fight hadi gesi ambako tuna quebic feet zaidi ya trilioni 59 za ujazo, kwa sasa zipo Tanzania.

“Vitu hivyo vinagusa wakandarasi ukizungumzia suala la miundombinu kwa sasa kutakuwa na miradi mikubwa katika nchi hii,”alisema Rais Dk.Magufuli.

Alisema imepangwa bajeti karibu asilimia 40 ambayo zaidi ya trilioni 10 zitakwenda kwenye miradi ya maendeleo na asilimia 46 zitakwenda kwenye Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilano.

RUSHWA

Rais Dk.Magufuli alisema miradi hiyo inaweza kumalizika kwa Sh milioni 200 ‘lakini unajua kabla hujamaliza lazima upeleke asilimia kwa mtu fulani’.

“Hiyo inaweza kuwa ni sababu na kama hiyo ni sababu tuna chombo chetu, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na kwa nini hamkitumii? Kwa nini mnaungana na wale wanaomba rushwa?” alisema.

Alisema kila mahali wanapokwenda kuomba zabuni wanaweka maslahi ya asilimia kwa ajili ya kuchukua rushwa.

“Nimemleta hapa Mkurugenzi wa Takukuru japo hakualikwa kwa sababu ni mtu ninayemwamini.

“Inawezekana mnaowapelekea kesi nao ni wala rushwa. Huyu namwamini, kama kuna tatizo la rushwa peleka taarifa kwa Valentino,” alisema.

Akizungumzia madeni kwa wakandarasi, alisema pamoja na kuwapo tatizo la kuyalipa, Serikali itahakikisha inayalipa kwa wakati.

Kama ni tatizo la kulipa madeni yao sasa limekwisha na Waziri wa Ujenzi, Uchuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amekwisha kulipa Sh bilioni 650, alisema.

Makombora

Rais Dk.Magufuli alisema changamoto kwa wakandarasi ni kutokuwa na ushirikiano na ubinafsi ambao ni ugonjwa unaotakiwa kuombewa.

Alisema changamoto nyingine ni wakandarasi kutumia majina ambayo siyo yao.

SOURCE: Mtanzania
 
Yaani kweli kabisa unajiuliza swali la "sijui akitajiwa mashahara wa Rais atanufaika nini?"

Hujui atanufaika nini? Hujui wewe utanufaika vipi? Hujui kuwa watanzania watanufaika vipi?.......ni wazi unafikiri kuwa "kunufaika huku" ni kupata senti kidogo kutoka ktk mshahara wa Rais!!....

Pole kama wafikiri hivyo maana utakuwa hujui, wastahili kujulishwa!!

Manufaa yetu sisi sote kwa hatua hii atakayochukua ni kuuona uwazi (transparancy) wa Rais wetu. That's all - nothing more, nothing less!!

Kwani kuna sababu yoyote ya msingi kwa nini mshahara na posho au marupu rupu ya Rais kufichwa, kuwa siri?? Yeye si mtumishi wa umma nambari one, au?? Na kwani analipwa kwa fedha toka ktk familia yake huko Chato? Si ni kutokana na kodi ninayolipa mimi na wewe na yule au??
Povu hilo...
 
Duh! Lowasa amevuruga siasa za Upinzani Tanzania....Ninachomshukuru Lowasa ni kufakiwa kutuonyesha watanzania unafiki wetu hadharani.!
Hata mimi ninamshukuru Lowassa kwa kutuwezesha kuwafahamu wanafiki ambao walituaminisha kwa muda mrefu ni wazalendo.

Huyo jamaa ukizisoma komenti zake za nyuma alikuwa haachi kutaja RICHMOND na jina la fisadi Lowassa lakini kwa sasa kutaja RICHMOND na jina la Lowassa imekuwa kwake kama kunywa sumu kali.

Huwezi kuona anaandika tena RICHMOND au Lowassa fisadi.

Unafiki at its best!
 
Magufuli bora urudi kijijini kwenu ukachunge ng'ombe. Huwezi kuongoza Tanzania ya 2016 kwa kuwaogopa mafisadi, wezi, wala rushwa na huku ukibaka demokrasi nchi kwa kiwango cha juu kabisa na kutaka kuongoza kwa sera za kukurupuka.

~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*
Unataka Rais Magufuli akachunge ng'ombe ili Lowassa apitie mlango wa nyuma na kuwa Rais wa Tanzania?

Mwambie mgombea wako Lowassa hawezi kununua wananchi wengi hata kama Rais Magufuli akienda kuchunga ng'ombe. Hawezi kuwa Rais wa Tanzania kwa kutumia pesa ya ufisadi. Never.

Mwambie Lowassa atimize ahadi yake aliyotuambia wakati wa uchaguzi kuwa ataenda kuchunga ng'ombe Monduli.
 
Kama kajitoa kafara ataje mshahara wake, uwe wazi kwenye tovuti ya Ikililu, ataje marupurupu yake yote, yawe wazi kwenye tovuti ya Ikulu. Ama awe anatoa wuarterly report ya mapato yake kupitia magazeti, ili tufahame naye analipa kodi kiasi gani. Na kubwa ya yote ni naye apunguze mshahara wake pamoja na marupurupu.
Hata akifanya vyote ulivyoviorodhesha bado utakuja na madai mapya na pengine utataka makazi yake yahamie Tandale ili afanane na watu wa Tandale.
 
Ulipendelea wapinzani wamsifie na pale bungeni wapitishe hoja zote za serikali ya Magufuli kwa sauti kubwa ya ndiooooooooo?
sio lazima kusifu lakini kwa mwenye akili atagundua kuwa aina ya ukosoaji na upinzani unaofanywa bungeni haulengi kuisaidia serikali,

upinzani wenye lengo la kuisaidia serikali huja na majibu mbadala ya matatizo ya wananchi na pia pale mazuri yanapofanyika husifia.
 
kuna nyoka humu anapondwa na kusiginwa kichwa lakini wapi anaponda kichwa kinaota kingine mkiani na anaendelea mbela bila kujali
BAK
 
Ningemsikiliza lakini aliposema amesoma Urusi nikajua ametumwa toka kwenye kitengo
Mbona wengine tumesoma Urusi na tumetulia tu, japo hoja zake ninakubaliana naye. Issue siyo Urusi ila ukweli na uharisia wa mambo
 
upinzani wenye lengo la kuisaidia serikali huja na majibu mbadala ya matatizo ya wananchi na pia pale mazuri yanapofanyika husifia.
Braza unaweza kutoa mfano mmoja tu wa serikali sikivu ya CCM kuchukua ushauri wa wapinzani na kuufanyia kazi? Mnyika alienda Bungeni na mswada wa maji, maCCM yakaupiga chini. Mbatia alienda na hoja ya kuboresha mfumo wa elimu Tanzania, wakamkejeli na kuipiga chini hoja yake. Kafulila alikuja na hoja ya Escrow, akahujumiwa. Wapinzani wameshashauri sana juu ya ku-regulate upangaji wa nyumba ambao kodi uwa hazilipwi kabisa, maCCM yakaziba masikio. Na kubwa kabisa, wapinzani walipigania katiba ya wananchi, maCCM yakaizika.

Upinzani katika siasa kazi yake ni kutafuta maeneo ambayo serikali iliyo madarakani inaonyesha udhaifu. Wanafanya hivyo na kutoa namna ya kukabiliana na udhaifu huo ili kuonyesha wananchi kwamba wanaweza kufanya nini wakipewa kuongoza nchi. BTW, unataka serikali isifiwe kwa kutekeleza wajibu wake??? Walioomba kura na kupewa dhamana na wananchi walisema yale watakayoyafanya, hivyo wakifanya wanakuwa wanatimiza wajibu wao. Sasa hapo unataka wasifiwe nini? Na kwa ukubwa zaidi, hivi utasifia nini kwa serikali za CCM ilhali nchi bado ni maskini wa kutupwa?? Ebu taja eneo moja tu la maendeleo ambalo serikali za CCM imelikamilisha kwa asilimia 100!
 
Ahahaha:
a)Kanali Anautaka Ukuu wa Mkoa!?
b)Anasema Yeye Sio Mwanasiasa,sasa mbona anaongea siasa mwanzo mpaka mwisho?
c)Anasema Magufuli ana Uchungu na Nia ya Nchi yake,na Uso wake unaonesha hivyo anapo uhubiri ukafara wake,je amempima na chombo gani akathibitisha kuwa uzalendo huo kweli moyoni?
d)Kanali amekuja kuokoa jahazi la Magufuli?Maana naona jamaa amepoooa!
Kasema yeye ana uchungu na nchi yake aliyoitumikia for over 30years, je wewe unayetoa comments zako huku na wewe ni mwanasiasa?
 
Braza unaweza kutoa mfano mmoja tu wa serikali sikivu ya CCM kuchukua ushauri wa wapinzani na kuufanyia kazi? Mnyika alienda Bungeni na mswada wa maji, maCCM yakaupiga chini. Mbatia alienda na hoja ya kuboresha mfumo wa elimu Tanzania, wakamkejeli na kuipiga chini hoja yake. Kafulila alikuja na hoja ya Escrow, akahujumiwa. Wapinzani wameshashauri sana juu ya ku-regulate upangaji wa nyumba ambao kodi uwa hazilipwi kabisa, maCCM yakaziba masikio. Na kubwa kabisa, wapinzani walipigania katiba ya wananchi, maCCM yakaizika.

Upinzani katika siasa kazi yake ni kutafuta maeneo ambayo serikali iliyo madarakani inaonyesha udhaifu. Wanafanya hivyo na kutoa namna ya kukabiliana na udhaifu huo ili kuonyesha wananchi kwamba wanaweza kufanya nini wakipewa kuongoza nchi. BTW, unataka serikali isifiwe kwa kutekeleza wajibu wake??? Walioomba kura na kupewa dhamana na wananchi walisema yale watakayoyafanya, hivyo wakifanya wanakuwa wanatimiza wajibu wao. Sasa hapo unataka wasifiwe nini? Na kwa ukubwa zaidi, hivi utasifia nini kwa serikali za CCM ilhali nchi bado ni maskini wa kutupwa?? Ebu taja eneo moja tu la maendeleo ambalo serikali za CCM imelikamilisha kwa asilimia 100!
nakubaliana na wewe kuwa nchi yetu ni masikini, tena masikini sana.

lakini hatuwezi kutoka hapa tulipo kwa kulaumiana kutupiana vijembe na kuishia kunyosheana vidole.
na naamini bungeni si mahala pake.

tatizo kubwa lilipo kwenye nchi yetu ni siasa iliyopenya kila sehemu ambayo kwa kiasi kikubwa imeondoa ufanisi na taifa limeshindwa kusonga mbele.

kinachofanyika sasa hivi hakina tofauti na wapiga debe stendi.
"abiria anaweza kuwa amepanda gari zuri tena linalokwenda mwendo salama na kufika kwa wakati, lakini akitokea mpiga debe akamshawishi abiria kwa kumdanaganya kuwa gari alilopanda ni bovu na haliwezi mfikisha salama abiria kwa kutokujua anashuka na kuliacha gari zuli.

hiki ndicho kinachofanywa na upinzani kuwashusha watanzania kwenye gari la serikali ya awamu ya tano ambayo inaungwa mkono na wananchi wengi,

na hiki ndicho kanali mstaafu anachojaribu kufafanua.
 
Braza wewe neno 'siasa' unalielewaje? Pengine nafanya mjadala na ntu asiyefahamu maana ya siasa! Kwa sababu nashangaa unavyosema bungeni kusiwe na siasa!

Kuna jamaa mmoja juzi wakati wa Malumbano ya Hoja, ITV, alisema jambo moja la msingi sana. Kwa nchi kama Tanzania ambayo haina national agenda, nchi inaendeshwa kwa Ilani ya chama tawala, huwezi kuepuka siasa bungeni na wapinzani kuiponda serikali ya CCM na Ilani yake. Hili la kuwa na national agenda (tuna national vision 2025, hii ingefaa kuliongoza taifa, lakini Ilani ndiyo inatumika) wapinzani wameshalisema sana, lakini wapi!!

Vilevile kwa 'demokrasia yetu ya uwakilishi', bungeni ndipo mahala pa kupanga mustakabali wa taifa letu. Sasa kutupiana lawama na vijembe haviwezi kukosekana pale chama tawala kinapofanya sivyo.

Labda nikuulize braza, wewe unatakaje? Tufanyaje ili tutoke hapa tulipo?
 
mkuu kwa ufupi ni kwamba kati ya vitu vingi vilivyochangia nchi yetu na nyingi za afirica kuwa masikini mojawapo ni ufisadi,
tukiweza kudhibiti ufisadi,kufanya kazi kwa bidii na kufanikiwa kudhibiti kile kinachokusanywa kisipotelee mikononi mwa wajanja wachache taifa litapiga hatua.

tanzania imempata raisi anayepiga vita ufisadi kwa maoni yangu aungwe mkono ili kulivusha taifa letu,

itikadi ziwekwe pembeni.
 
Ufisadi upi anaoudhibiti? Vipi kuhusu Escrow? EPA? Richmond/Downs/Symbion? Lugumi? DSM Ferry? Nyumba za serikali? UDA? Pride?

Udhibiti wa ufisadi hauitaji kupata Rais anayepinga ufisadi tu! Hauitaji one man army! Unahitaji uwepo wa mfumo unaofanya kazi bila kumtegemea Rais. Mfumo ambao hadi sasa miezi 7 ya Rais Magufuli sijaona ukijengwa.
 
unajenga mfumo ndani ya miezi saba na kutekelaza yote uliyoeleza?

sidhani kama haya yanaweza kutekelezwa ndani ya miezi saba.

vuta subira mambo mazuri yanakuja.
 
unajenga mfumo ndani ya miezi saba na kutekelaza yote uliyoeleza?

sidhani kama haya yanaweza kutekelezwa ndani ya miezi saba.

vuta subira mambo mazuri yanakuja.
Kwani tumepata uhuru lini? Na chama gani kimekuwa madarakani toka uhuru? Kwani Magufuli kachukua nchi kutoka wapi?
 
Back
Top Bottom