Eti Ikulu imesema kuwa yaliyosemwa na Dk Ulimboka ni upuuzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti Ikulu imesema kuwa yaliyosemwa na Dk Ulimboka ni upuuzi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kinyongo, Oct 19, 2012.

 1. k

  kinyongo Member

  #1
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Nchini, Dkt. Stephen Ulimboka, kusisitiza kwamba alitekwa na mtu anayefanya kazi Ikulu, Ramadhan Ighondu, Ikulu imehamanika na kujitetea kwamba madai hayo ni ya kipuuzi.

  *Tafadhali bofya hapa kurejea kuisoma nakala ya taarifa kamili aliyoitoa Dkt. Ulimboka.

  Jana Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu, alisisitiza: “Ikulu iliishajibu. Tulisema haihusiki, na Rais Jakaya Kikwete amepata kuzungumza juu ya jambo hili mara nyingi.”

  Rweyemamu, bila ya kufafanua zaidi alisema, “Naomba uninukuu; haya madai ni upuuzi… hiki kitu kilishajibiwa.”

  Alipoulizwa kama anamfahamu Ramadhan Ighondu, Rweyemamu akisisitiza kuwa Ikulu haihusiki naye.

  Mwandishi akamwuliza Rweyemamu ni hatua gani ambazo Ikulu itamchukulia Ighondu kama mfanyakazi wao.

  Swali hilo lilionekana kumkera Rweyemamu aliyejibu kwa ukali, “Kama Ikulu haihusiki, hatuna cha kufanya juu ya jambo hilo; mnakaa mnalea maneno ya kipuuzi… Ikulu imwajibishe kuhusu nini? Haihusiki!”

  Alipobanwa zaidi alisema kama kuna watu wanasema hivyo waende wakaripoti polisi.

  Kauli ya jana ya Rweyemamu ni ya pili kutolewa na Ikulu kuhusu Dkt. Ulimboka. Mara ya kwanza, ilipotolewa na Rais Jakaya Kikwete alipokutana na baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, akasema, “Dk. Ulimboka ana nini mpaka Ikulu imteke? Tumteke ili iweje?”

  Kikwete alikwenda mbali zaidi na kusema hata Dk. Ulimboka mwenyewe alipokwenda Ikulu akiwa na viongozi wenzake alinyamaza kimya tu na kwamba waliokuwa wakizungumza ni wengine.

  Hata hivyo, kwa kuwa Ikulu imesema haihusiki, na Dk. Ulimboka mwenyewe ametamka kwamba anamjua aliyemtesa, na kwamba anafanya kazi Ikulu, ni juu ya umma kuamua nani anasema ukweli.

  Wakati Ikulu ikisema hayo, Jeshi la Polisi ambalo lilimtia mbaroni raia wa Kenya na kumpeleka mahakamani kujibu tuhuma za kumteka na kumtesa daktari huyo, nalo limesita kubainisha kama litamkamata na kumhoji Ighondu, ambaye ametajwa rasmi na shahidi wa kwanza halisi katika suala hili, Dkt. Ulimboka.

  Maofisa wa jeshi hilo wametupiana mpira kila mmoja akidai hahusiki na suala hilo.

  Kwa upande wa polisi, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alijitetea akisema suala hilo liko kwa mkubwa wake wa kazi, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Maanumba, na kwamba atafutwe kwa ajili ya kulitolea ufafanuzi, “Gazeti lenu juzi nililisifia sana nikalitolea mfano mzuri; watu hawawezi kutuchezea tu na kutishia mamlaka iliyopo kama hakuna sheria. Lazima kila mmoja afuate sheria. Hilo suala liko kwa DCI na sisi polisi tuna nidhamu ya kazi. Suala likiwa kwa mkubwa wako huwezi kulizungumzia. Tambua faili lipo kwao na mimi sina uwezo wa kulizungumzia,” alisema.

  Alipobanwa zaidi kuwa Dkt. Ulimboka ameshamtaja aliyemtesa na kwamba yuko tayari kuwapa ushirikiano na kutoa ushahidi mbele ya tume huru, Kova alisema, “Hivi wewe unanitafuta nini? Nimekwambia sina uwezo nalo; au hutaki ushirikiano na mimi? Hilo swali lako ni sawa na kumuuliza kipofu pale unapaonaje!?”

  Naye DCI Manumba alipopigiwa simu, alijibu kwa kifupi akisema aulizwe msemaji wa jeshi hilo. Akakata simu.

  Msemaji wa jeshi hilo, Advera Senso, alipoulizwa alisema suala hilo liko kwenye uchunguzi, hivyo hawezi kulitolea ufafanuzi. Senso alipobanwa zaidi, alisisitiza, “Tafadhali, sina maelezo zaidi ya hayo. Kukiwa na kitu kipya tutaandaa.”
   
 2. Myocardial Stunning

  Myocardial Stunning Member

  #2
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 19, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ulimboka ni upepo tu ushapita.... hana jipya! amesababisha vifo vya watanzania wengi kwa ule uchochezi wake.... nashangaa ponda wamemkamata kwa uchochezi jhuyu ulimboka yupo mtaani ..

   
 3. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,019
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  upuuzi ni upi ?kwamba ramadhani ighondu sio mfanyakazi wao?
  wamtumie ighondu akazime maasi ya waislam sasa.
   
 4. bysange

  bysange JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 4,378
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Shiiiii!wanaunda Tume ya kuchunguza uwezo wa akili wa ulimboka,coz ya kipigo.
   
 5. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Mkuu meningitis, hawa ndo wakupewa Insulin 100 IU akikatiza EMD for any complaint tuwapoteze kabisa... Liwalo na liwe!!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Miongoni mwa vihele hele wa kwanza kupelekwa ICC ni huyu mwandishi mchumia tumbo Salva Rweyemamu, majibu anayotoa huwezi amini yanatoka IKULU na ameendelea kukumbatiwa pale
   
 7. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145


  Unataka IKULU Iwake MOTO? Sasa hivi wako NDANI WAKIDADISI Jinsi ya Kutoa Tamko kwa Wananchi wa Tanganyika & Zanzibar kuhusu MATATIZO yanayoikabili NCHI YETU; Halafu kwenye hiyo HABARI au TAMKo Wanatakiwa Wongee LUGHA Safi na Murua kufurahisha MABALOZI wa NCHI TAJIRI na Pia Wafanyakazi wa KIGENI

  Sasa Halafu Unawataka Wawake MOTO walijibu Suala la Dr. na Imeshajulikana it is an ANIMAL within the ADMIN??? Of Course they will brush it OFF for now...
   
 8. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  ''Join Date : 19th October 2012''
  Location : Ligament Of Treitz
  Posts : 12
  Rep Power : 303
   
 9. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,477
  Likes Received: 784
  Trophy Points: 280
  Ndugu mbona unakurupuka kutoa maelezo yasiyo na kichwa wala miguu, hivi unaweza kufananisha suala la mgomo wa madaktari na suala la kina Shehk Ponda kweli?
   
 10. b

  bob giza JF-Expert Member

  #10
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nasikia jamaa wanakusubiri hospitali, ukiumwa hata kichwa tuu utajua....
   
 11. ethicx

  ethicx JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 314
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  naona akili yako ina funyo, hivi mtu anaefanya uchochezi na anayesababisha vifo vya watu unafikiri nani wakufunguliwa mashtaka? Km wew ni mtumzima mwenye akili basi unam matatzo sio bure.
   
 12. moto2012

  moto2012 JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 2,168
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  Myocardial stunning acha akili za kuambiwa hizo!
   
 13. ethicx

  ethicx JF-Expert Member

  #13
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 314
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  naona akili yako ina funyo, hivi mtu anaefanya uchochezi na anayesababisha vifo vya watu unafikiri nani wakufunguliwa mashtaka? Km wew ni mtumzima mwenye akili basi unam matatzo sio bure.
   
 14. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #14
  Oct 19, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Sio kila mtu anapenda hizi Soap Opera za wenyeviti wa jumuia.
  Uli mwenyekiti wa jumuya, Ponda mwenyekiti wa jumuiya.......mwendelezo wa tamthilia zisizo na msisimko wa kimaendeleo.
   
 15. E

  ESAM JF-Expert Member

  #15
  Oct 19, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 962
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Wakati mwingine huwa akili za Salva Rweyemamu sijui huwa zinafanya kazi kweli au ni kulewa cheo? Yaani mtu anadai atendewe haki yake wewe unaita upuuzi, hata bila aibu. Si angeongea tu lugha nzuri tu. Huyu mhaya kweli kalewa cheo alicho nacho.
   
 16. mzamifu

  mzamifu JF-Expert Member

  #16
  Oct 19, 2012
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 3,496
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  hivi hakuna uwezekano wa kumstaki huyo afisa wa ikulu?
   
 17. T

  Ti Go JF-Expert Member

  #17
  Oct 19, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 361
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 60
  Nadhani bosi wake (SALVA) angejua kuwa siyo mtetezi wake mzuri angemfuta kazi haraka iwezekanavyo. Wakati anachagua alifikiri atakuwa msemaji mzuri kumbe hovyo. majibu yake yanatia kichefuchefu
   
 18. L

  Lwesye JF-Expert Member

  #18
  Oct 19, 2012
  Joined: Sep 29, 2012
  Messages: 5,297
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Una laana ya kuzaliwa unajifanya kipofu huyu KIkwete mshangaa makasri ya wenzake mbona humsemi fedha zote za hazina yeye anatumia kuzurula dunia nzima eti kumbembea badala ya kununua dawa na vifaa mahospitalini na kuboresha sekta ya afya huyo ndio wa kutiwa ndani bila kesi
   
 19. Myocardial Stunning

  Myocardial Stunning Member

  #19
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 19, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mgomo wa madactari lilikuwa zito zaidi walikufa kina mama.. watoto.. na maskini... !! ulimboka mikononi ana damu ya watanzania.. kwa uchochezi alio fanya! ...
   
 20. B

  Buluki Member

  #20
  Oct 20, 2012
  Joined: Jul 4, 2012
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uko sahihi kaka maana kazi aliyoifanya ponda na huyu kaifanya ila hawamgusi.....dah serikali hii ina mambo!
   
Loading...