Eti hatutaki "level seat"

Eti hatutaki "level seat"

GREAT ZILLA

Member
Joined
Mar 26, 2020
Posts
13
Reaction score
37
Baada ya Tangazo la amri ya kudhibiti na kuzuia daladala kujaza watu kama magunia, wakaibuka watu wanalalamika kwamba level seat ni jambo lisilowezekana! Wanataka kuendelea na utaratibu wao waliouzoea ili wapate faida.

Nikawa najiuliza, licha ya hatari ya maambukizi ya corona katika hali hiyo, kuna hatari ambayo ni kubwa zaidi inapotokea ajali na gari kupinduka! Watu kujazana vile, kuna mtu anatoka salama kweli?

Safety measures za barabarani ni mpaka tupate corona?

Ukitizama jinsi watu wanavyoshambuliana kwenye usafiri wa umma unaweza kupigwa na butwaa! Ni kundi zito la watu wanaosukumana mpaka kupanda kwenye madirisha! Ndani ya gari ni kama rundo la siafu walionatana.

Hivi hii kitu ndio utaratibu wa nchi? au liwalo na liwe tu?

Kuna mtu kweli nchi hii aliyekabidhiwa jukumu la kusimamia usalama wa abiria ndani ya magari?

Na baada ya hii corona kuisha, utaratibu wa kushindilia watu kwenye magari utaendelea?

What is the long plan?
 
Back
Top Bottom