Ethopia yakiri kutungua ndege ya Kenya nchini Somalia

Ethopia yakiri kutungua ndege ya Kenya nchini Somalia

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Posts
8,633
Reaction score
16,601
Ethiopia yakiri kutungua ndege ya Kenya katika ardhi ya Somalia

Askari wa jeshi la Ethiopia wamekiri kuwa walitungua kimakosa ndege ndogo ya Kenya iliyokuwa imebeba misaada na vifaa vya kupambana na janga la corona katika mji wa Bardale, kusini mwa eneo la Bay nchini Somalia.

Askari hao wa Jeshi la Taifa la Ulinzi la Ethiopia (ENDF) wanaolinda uwanja wa ndege wa Bardale wamesema waliitungua ndege hiyo wakidhani kuwa ilikuwa mikononi mwa magaidi waliokuwa na lengo la kuiangusha katika angatua hiyo ndogo.

Ripoti ya awali ya uchunguzi wa tukio hilo imewanukuu askari hao ambao wanasisitiza kuwa hawakuwa na taarifa yoyote kuwa kulikuwa na ndege ndogo ya kiraia iliyotazamiwa kutua katika uwanja huo wa ndege.

Hata hivyo imebainika kuwa, askari hao wa Ethiopia waliotungua ndege hiyo kwa roketi Jumatatu iliyopita si miongoni mwa wenzao waliopo chini ya mwavuli wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM.

Ndege hiyo ya binafsi ilikuwa imebeba misaada ya kibinadamu inayohusiana na janga la corona wakati ilipoanguka ikikaribia kutua katika uwanja wa ndege wa Wilaya ya Bardale kusini mwa Somalia, yapata kilomita 300 kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Katika tukio hilo, marubani wawili raia wa Kenya walipoteza maisha pamoja na raia wengine wanne wa Somalia. Ndege hiyo binafsi ni ya shirika la African Express Airways yenye makao makuu yake katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi

4bv9562c36f0781neus_800C450.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo imedunguliwa makusudi,maana iyo ndege sio ya kivita useme ni tishio kupita katika anga lao.ila wao walichofanya kwakuwa walikuwa hawana taarifa ya ndege hiyo wakaamua tu kwa utashi wao kuiangusha
 


Ethiopia admits to shooting down a Kenyan cargo plane by "mistake"
 
aisee mbona kuna taratibu za kuwasiliana na rubani kabla ya kutua anatakiwa kujitambulisha na kuna radio call mule ukiita lazima wasikie
 
2SOM.png


1SOM.png


The flight was permitted by the Somalia Civil Aviation Authority
 
Back
Top Bottom