Ethiopian PM Meles Zenawi dies at 57 after illness

Ethiopian PM Meles Zenawi dies at 57 after illness

Hivi ni kigezo gani hutumika kumuita mtu dikteta?Mi wananikera sana!
 
Hivi ni kigezo gani hutumika kumuita mtu dikteta?Mi wananikera sana!

Mkuu,

Kwenye udikteta;

1. Kiongozi wa nchi yeye ndie mtu pekee wa kuongoza na hakutakuwa na wa kumpinga. Yaani hakuna upinzani na hata kama upo atatumia sababu na asasi zake mbalimbali kubinya ukuaji wa upinzani huo.

Mfano wa kiongozi kama huyo ni Robert Mugabe, Meles Zenawi na wengine wengi tu. Hawa wamepata madaraka kwa mtutu wa bunduki kwahio hawaoni sababu ya kuwaondoa kwenye madaraka waliyoyapigania.

2. Kwenye udikteta kiongozi au dikteta hazingatii katiba ya nchi katika kutawala watu wake- yaani katiba iliyopo inatosha na haina haa ya kuibadili, yupo juu ya sheria na hatambui kisheria uwepo wa upinzani juu yake, kwamba kuna wananchi ambao wana mawazo tofauti.

3. Kwenye udikteta uamuzi wa kiongozi ni wa mwisho (absolute power) na haupingwi na kila wakati huenda kwenye vyombo vya habari kuwakumbusha wananchi uwepo wake na kwamba wasisahu jambo hilo. Pia taarifa mbalimbali za propaganda hutayarishwa na kurushwa kupitia vyombo hivyo ambavyo vingi humilikiwa na serikali yake.

Taarifa na propaganda hizi hubeza, hukejeli, huponda, huzodoa na wakati mwingine kukashifu upinzani na kusema kwamba hakuna mwenye sifa za kuongoza jamii isipokuwa kiongozi huyo mtukufu.

4. Kwenye udikteta hakuna bunge, uchaguzi, na mara kwa mara huwepo amri ya kutotembeo hovyo hovyo mabarabarani, kutangazwa hali ya hatari muda wowote ule na madudu mengine mengi tu.

Sasa zipo aina mbalimbali za udikteta, mifano ni udikteta wa kikatiba, udikteta wa kijeshi, udikteta wa kijamaa (kama ilivyokuwa Yugoslavia na baadae hayati mwalimu Nyerere akaiga na kuleta vijiji vya ujamaa), udikteta wa kujiita mzalendo yaani kama ule unaotumiwa na Robert Mugabe kule Zimbabwe.

Mugabe anasema Afrika ni ya wafrika na ardhi ni yao na wana haki asilimia 90 ya umiliki na mgeni hana chake isipokuwa kama akiomba na kupewa kibali.

Udikteta wa kikatiba na kijeshi siku hizi unachanganywa na mifano ni Rwanda na Uganda ambapo maraisi Kagame na Museveni wanatumia mbinu hiyo kuongoza nchi hizo kwamba kukiwa na dharura wao wanatawala kijeshi ingawa katiba haiwapi nguvu zaidi lakini wakiwa wanajeshi wanatoa amri mbalimbali za kutawala kijeshi.

Kwahio mtu ataitwa dikteta kama atafanya mambo hayo na kwamba hatoweza kuruhusu mtu mwingine achukue madraka mpaka mauti yatakapomkuta au ugonjwa wa kupooza au kuondolewa kwa nguvu.

Basi mkuu nimejitahidi kueleza kwa kifupi lakini hili eneo ni pana na lina umuhimu kulifuatilia kwani limejaa elimu nzuri sana.
 
Jirani zangu hapa toka Ethiopia na Eritirea wana furaha kupita maelezo kufuatia kifo cha huyu dikteta. Juzi juzi pia kiongozi mkuu wa dini ya Othodox huko Ethiopia alikufa napo ilikuwa sherehe kwa wa-Ethipoia.

Huyu jirani yangu wa Ethiopia ananiambia kuwa kwenye mkutano wa G-8 uliopita Meles Zenawi alikuwa amekaa karibu na rais wa Ghana aliyekufa hivi majuzi. Kwahiyo kuna tetesi kuwa huenda wamepuliziwa sumu. Sasa sijuwi kama ni kweli ni kwanini.
Link Prime Minister Meles Zenawi G8 Summit at Camp David DireTube Video by News in Detail


link 2. africa
 
Nimeona asee kweli walikuwa karibu, sasa sijuwi hiyo assumption yao ni kweli ama ni koinsidensi tu.
Tungoje tuone kama na waalikwa wengine wawili kama wataumaliza mwaka.

Walikuwa wanne.
Pia inawezekana wawili hawa wamepewa angalizo tu kuwa wakijifanya wabishi watashughulikiwa.
 
Hailemariam Desalegn, Ethiopia’s New Prime Minister


Hailemariam.jpg

Ethiopian government officials say Hailemariam Desalegn, 47, will be the next Prime Minister of Ethiopia until elections in 2015 following the death of Meles Zenawi.

He is currently the acting prime minister and the foreign minister and will be sworn in as prime minister and run the country until 2015. He has served as deputy prime minister and foreign affairs minister since 2010.

Former Prime Minister Meles Zenawi died on Monday at age 57. His body was returned to Addis Ababa from abroad late Tuesday night.
 
Tungoje tuone kama na waalikwa wengine wawili kama wataumaliza mwaka.

Walikuwa wanne.
Pia inawezekana wawili hawa wamepewa angalizo tu kuwa wakijifanya wabishi watashughulikiwa.

Mkuu wa nne alikuwa nani? Maana ni hawa wawili walioondoka na JK
 
G8-SUMMIT2.jpg

Umemwona huyo mkulu mwenye uso kama umepigwa masumbwi,umevimba vimba...hakupata usingizo wa kutosha.
Analia au anacheka?
 
_62632952_62632951.jpg


Thousands of Ethiopians and dozens of foreign dignitaries came to pay tribute at the funeral of Ethiopian Prime Minister Meles Zenawi. Many joined a procession taking the coffin to Addis Ababa's Meskel square.


_62633372_62633371.jpg


Many dressed up to pay their respects for Mr Meles, who died in Brussels last month aged 57 after a long illness.



_62630278_62630277.jpg


The coffin moved slowly through the capital on a horse-drawn carriage, accompanied by a marching band.



_62630270_62630269.jpg


The coffin entered the square for the start of the ceremony, the country's first state funeral for one of the country's leaders for more than 80 years.
 
_62630171_62630170.jpg


Mr Meles is credited with bringing growth and development to Ethiopia, but critics say this was achieved at a cost of respect for human rights.


_62633488_62633487.jpg


After tributes from African leaders, mourners then made their way to the Holy Trinity Cathedral for the burial in heavy rain, among them Mr Meles' widow Azeb Mesfin, here comforted by her daughters.


_62632240_62632239.jpg


Members of the Orthodox priesthood stood in the rain as the burial took place
 
Back
Top Bottom