Ethiopian Airlines vs Kenya Airlines

and 300

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
26,325
36,121
Wadau, nikiri tu mimi kwetu hukoooo NGARA vijijini karibu na nchi ya RWANDA, mjini nimekuja na mbio za Mwenge na shule za kuunga unga a.k.a nimeresit mara 7.

Nimepata kazi kwenye N.G.O inayojihusisha na mambo ya Afya hivyo kusafiri kwa ndege ni NI KWA HISANI YA WATU WA MAREKANI sasa ndege ninazozijua ndo hizo hapa (ET vs KQ). Je nyie wajuvi wa mambo mliokwea hizo ndege nani zaidi kati ya ET vs KQ katika nyanja zifuatazo;
1. Reliable & Convinient booking system (including payment mode = mobile money, Credit card, CASH/local or foreign currency).
2. Kwenda na muda (wasioendekeza frequent cancellation, delays)
3. Ground Staff
4. Inflight services (First Aid, Entertainment, Meals)
5. Transfer Desk (Hotel in case of long layover)
6. Luggage handling.
Asanteni

 
Kwa kuwa sijapanda kenya ngumu kutoa ushuhuda ila ethiopia hamna kitu izo sifa mbovu almost zote wanazo sema tu waafrika bajet zetu ndio zinaoana hapo.
 
Kwa kuwa sijapanda kenya ngumu kutoa ushuhuda ila ethiopia hamna kitu izo sifa mbovu almost zote wanazo sema tu waafrika bajet zetu ndio zinaoana hapo.
Daah, haya mkuu, tuma salamu kwa mtu mmoja
 
Wanayo mema mengi sn ikiwemo bei zao ila kwa leo tunajadili maovu yao.
ni kweli mkuu hata mm waliniboaga nilipokuwa natoka LAGOS nimeingia kwenye ndege nna njaa sana maana Wanaija j2 hawafungui biashara sasa nikawaomba maji daah wakaninyima, nilifadhaika sana. Pili, Airport yao imekaa kimshazari sana mnarundikwa kama banda la kuku.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom