Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani kufanyika nchini Tanzania, mgombea ubunge wa Bunda Mjini mkoani Mara kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Esther Bulaya ameendelea na kampeni zake licha ya mvua kunyesha.
Bulaya akiwa kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika jana Jumatano, Oktoba 22, 2025 katika Mtaa Mabanzuni, Kata ya Balili, alinadi sera za chama hicho kwa wananchi wa jimbo hilo huku akiwahakikishia kuwa, endapo watampa ridhaa ya kuwa mbunge wao, atashirikiana na Serikali kuhakikisha ujenzi wa ofisi za Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa) Kanda ya Magharibi unafanyika hususan katika Kata ya Balili.
Soma: Bulaya, Esther Mathiko washindwa kung'ara kura za maoni
Amesema uwepo wa ofisi hizo utasaidia kudhibiti uharibifu unaosababishwa na tembo ambao wamekuwa changamoto kubwa kwa wakulima wa eneo hilo.