Ester Matiko ashindwa nguvu na madiwani wake

Ester Matiko ashindwa nguvu na madiwani wake

Derimto

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
1,307
Reaction score
325
Katika hali isiyo ya kawaida kikao cha madiwani kimevunjika huku baadhi ya madiwani wakitaka kushikana mashati wakipingana kile wanachokiona kuwa ni utaratibu mbovu wa uchaguzi baada ya kutaka kupitisha jina la mwenyekiti wa halmshauri ambaye siyo chaguo la madiwani bali ni maelekezo ya mbowe na timu yake.

Madiwani wasusa kikao na kutoka nje na kurushina maneno makali mbele ya majengo ya ofisi za halmashauri ya wilaya ya Tarime walikopewa hifadhi ya ukumbi wa kufanyia kikao chao wamegawanyika makundi mbalimbali kwenye eneo la halmashauri huku mbunge Ester Matiko na wapambe wake wakijibanza pembeni ya ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Tarime huku akionekana na hasira za kutosha kwa madiwani wake.
 
Huko ndio Tarime bana, chochote kinaweza tokea, lete source
 
Huko ndio Tarime bana, chochote kinaweza tokea, lete source

Source mimi mwenyewe niko eneo la tukio nashindwa kutupia ka picha maana nikionekana napiga picha hasira zote naweza kuangushiwa mimi.
 
Source mimi mwenyewe niko eneo la tukio nashindwa kutupia ka picha maana nikionekana napiga picha hasira zote naweza kuangushiwa mimi.

Acha uongo mulisya..Mi nipo hapa polisi central mbona sion chochote hapo kwa mkurugenzi
 
Ni kweli kuna mgogoro kati ya Esther na madiwani wake, chanzo ni mh mbunge kutaka kuweka mwkt wa halmashauri anaemtaka yeye, toka jana vikao vimekaa na wameshindwa kuelewana.
Kuna shinikizo toka makao makuu kumsuport esther na vitisho juu, but madiwani wamegoma wanataka waweke mtu watakaemchagua wao sio Esther.
 
tuliambia Tarime mfumo dume umekwisha, sasa atudhihirishie hilo.
 
Msimamizi wa uchaguzi kapokea barua mbili, moja inatoka wilayani ikimthibitisha Hamis Nyanswi kuwa ndie atakaegombea uenyekiti wa halmashauri, na nyingine toka makao makuu ikitaka Sauti athibitishwe kugombea.
Msimamizi wa uchaguzi kawambia kisheria barua anayotambua ni kutoka uongozi wa wilaya na sio Taifa so uapishwaji wa madiwani ndio unaendelea sasa.
 
Mkuu asante kwa taarifa yako nzuri!
 
Acha uongo mulisya..Mi nipo hapa polisi central mbona sion chochote hapo kwa mkurugenzi

Ukiwa lofa na nyumbu huwezi kuelewa halmashauri ya wilaya na ya mji na ofisi ya mkuu wa wilaya
 
Ni kweli kuna mgogoro kati ya Esther na madiwani wake, chanzo ni mh mbunge kutaka kuweka mwkt wa halmashauri anaemtaka yeye, toka jana vikao vimekaa na wameshindwa kuelewana.
Kuna shinikizo toka makao makuu kumsuport esther na vitisho juu, but madiwani wamegoma wanataka waweke mtu watakaemchagua wao sio Esther.

Nisaidie kuwaelewa kamanda maana hali ilivyokuwa masaa mawili yaliyopita hali ilikuwa mbaya maana hapakuwa na heshima ya demkrasia na haikuwa siri tena na baadhi yao walitaka kushikana pale karibu na maegesho ya magari
 
Ndugu, nlichosema ni kuwa kama pana mgogoro ni vyema ukasuluhishwa kwa vikao vyetu vya chama kulikoni kuja kutangaza hapa jf....

Kama mlitaka kusuhisha kwenye vikao vya ndani yale makelele na matusi mliokuwa mnajaza hapa halmshauri na kuwaita baadhi ya vijana wa bodaboda ilikuwa ni kwa ajili ya nini? acha kutumia masaburi kuongea badala ya kinywa.
 
Haina haja ya kutukanana, ila kwa hali ilivyo Esther ana hii miaka mitano tu
 
Haina haja ya kutukanana, ila kwa hali ilivyo Esther ana hii miaka mitano tu

Ni kweli kamanda ila sidhani kama ni maamuzi ya Esterpeke yake bali inavyoonekana ni marlekezo kutoka uongozi wa juu maana yeye mwenyewe anaonekana kama haridhiki na hali hiyo.

Kinachokera hapa ni kuona baadhi ya watu wananitukana kwa kulizungumzia suala hili wakati hii ni nchi ya ki demokrasia.
 
Back
Top Bottom