Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,499
Wakati wa kujadili hotuba ya Rais Samia, Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini (CCM), Ester Bulaya, kwenye Bunge la Kumi na Tatu, Mkutano wa Pili, Kikao cha Kwanza Januari 27, 2026, amepongeza juhudi na dhamira kubwa ya Rais Samia katika kujenga Taifa.
===
Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ester Bulaya, leo Januari 27, 2026, ametoa mwito kwa vijana nchini kote kuamka na kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi zilizoelezwa kwenye hotuba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akichangia mjadala wa hotuba ya Rais wakati wa ufunguzi wa Bunge la 13, Bulaya amesisitiza kuwa Rais Samia ameandika historia kwa kuwataja vijana zaidi ya mara tano kwenye hotuba yake, akionyesha kuwa kundi hilo ndilo "moyo" wa mipango ya serikali. Bulaya amesema Rais Samia amedhamiria kutengeneza mabilionea vijana kupitia dirisha maalum la uwekezaji.
Ametaja baadhi ya maeneo ya kipaumbele kuwa ni pamoja na fedha zilizotengwa mahususi kwa ajili ya vijana wajasiriamali, wakiwemo Wamachinga, ili waweze kusimama kiuchumi, Mpango wa kuanzisha kampasi za vyuo vikuu katika kila mkoa na kuongeza bajeti ya mikopo ya elimu ya juu na ujenzi wa vyuo vya VETA katika kila wilaya ili kuandaa mafundi watakaoendesha viwanda kwenye kanda maalum za kiuchumi.
Kuhusu vurugu na madhila yaliyotokea wakati wa uchaguzi wa 2025, mbunge huyo amesema Rais ameshaonesha njia ya uponyaji kwa kuunda Tume ya Uchunguzi. “Wote Watanzania tulikubaliana yaliyotokea sio mazuri…Rais ameonesha nia ya kutatua kwa kuunda tume na amesema bayana tume ikileta majibu kama kuna taasisi kuna maeneo ilifanya makosa atachukua hatua”, ameeleza.