Espionage katika mapenzi

Espionage katika mapenzi

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,485
Kuchunguza,kuibiana taarifa kuhujumiana,kuharibiana,kupo kati ya nchi na nchi hasa zinazohasimiana,makampuni ya biashara yanayozalisha bidhaa zinazofanana,vilabu vya michezo,hasa mpira wa miguu,vinayohasimiana na mambo mengine.

Hata hivyo Espionage ipo zaidi kwenye ulimwengu wa mapenzi, tena huku ndio balaa.
Espionage ipo ya ndani kwa ndani,yaani kati ya wapenzi wawili, me na ke, pia espionage ipo kati watu wa nje na watu wa ndani, yaani watu wa nje kuchunguza na kupata taarifa za wapendanao au mmoja kati ya wapendanao, taarifa hizi kila mtu anazitaka kwa matumizi yake, hasahasa wivu, umbea, majungu n.k.

Espionage ya ndani kwa ndani
Mwanamke kumchunguza mwanaume kama ana michepuko, hapa hufuatilia kila kitu kila mahali na bila mwanaume kujua kama mwenzie anamchunguza. Huwa na maspy kazini na vijiweni kama ni lazima kufanya hivyo, simu hupekuliwa kila kitu bila mwanaume kujua, Mwanaume pia hufanya vivyo hivyo

Espionage ya ndani na nje
Hapa mwanaume na mwanamke hufuatiliwa na watu wa nje kujua tu mambo yao, wapenzi wa zamani pia hufuatilia mengi juu ya mmoja wa hawa wanaume na wanawake kwa sababu za wivu, ama kutaka kujua tu. Majirani na marafiki hutaka kujua tu,kwa sababu wanazozijua wao, pengine wivu,chuki,roho mbaya,kuiga na umbea. Kuna baadhi hupenda wapenzi hawa wahalibikiwe ndio furaha yao, wengine sivyo.

Michepuko
michepuko hufanya zaidi espionage ili kujua ni nini unakikosa kwake ili yeye aongeze ili kumkamata mwanaume au mwanamke wako, pia hufanya espionage ni nini unakipata zaidi ili yeye atoe zaidi yako ili kumkmata mpenzi wako.

Kwa hiyo wewe fanya ufanyavyo katika mapenzi kila kitu chako kinajulikana, hata ufanye usiku wa manane.
kama kuna mtu yuko katika ulimwengu wa mapenzi,haamini haya nampa pole, espionage ni kila sehemu ila mapenzi ni noma.
 
Back
Top Bottom